Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,446
- 829,812
Mada yangu moja ya mwezi May ilizungumzia hofu ya CCM juu ya UKAWA na Lowassa kwamba yeyote atakayeshika madaraka itakuwa ni kiama kwao.
Mwelekeo ulikuwa dhahiri kuwa mgombea na hatimaye rais atakuwa Lowassa kwa upande wa CCM huku UKAWA wakichukua viti vingi sana vya Ubunge Udiwani nk. Hapa ingetengenezwa colabo nzuri sana kwakuwa kuna mfanano na kushabihiana fulani kati ya Lowassa na UKAWA.
Hii imeendelea kuwa hofu kwa kundi la CCM maslahi, wameangalia mbele wakaona wazi nini kitatokea iwapo wawili hao wataukamata uongozi wa nchi.
Fitina ikatengenezwa na 'KITENGO' kwanza kumpiga chini Lowassa kwa namna yoyote ile kisha kufitinisha upinzani wafarakane ili nguvu ipungue.
Wamefanikiwa kwa Lowassa japo kwa sasa, wanaweza kufanikiwa upinzani japo kwasasa lakini mwendo wao huu hauwapeleki barabara iliyonyooka bali wanachanja mbuga kuingia chaka wasilolijua.
Lowassa ana nguvu ana haiba ya uongozi, ana rasilmali watu ya kutosha, upinzani nao hivyohivyo, kutaka kuyadhoofisha na hatimaye kuyauwa kabisa haya makundi mawili na ukabaki salama sio kitu cha mchezomchezo tu...kuna kubwa tena baya kabisa litatokea.
Lowassaa yuko kimya kwasasa, sio mpuuzi na si kama kashindwa mapambano anajipanga, anatafakari anajiweka vizuri ana kundi kubwa mno linalosubiri kauli yake atakachosema ndicho watakachotenda liwe baya liwe zuri.
Upinzani nao sio wa kudharau kuna kundi kubwa sana la wananchi waliochoshwa na CCM wana imani kubwa na upinzani, wanataka mabadiliko hawako tayari tena kuona CCM inarudi madarakani wamewekeza nguvu na rasilmali zao pale, CCM wasione hiii ni segere la yamoto bendi.
Hicho 'KITENGO' Kiache ujuha kitaiangamiza nchi kwa ajili ya kulinda maslahi ya wachache ambo hata hivyo hawajai yutong tano....! Huu ni mustakabali wa taifa wafanye upuuzi wao lakini amani na ustawi wa Taifa visiathirike .
Pesa waliyowekeza kufitinisha upinzani ni wendawazimu mtupu mabadiliko yanapofika hakuna wa kuyazuia hata awe nani yaliyotokea mashariki ya kati na kwingineko Afrika hayashindwi kutokea hapa.
Tutafakari.