Ccm mna ukosefu wa kinga ya ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm mna ukosefu wa kinga ya ufisadi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by environmental, Apr 29, 2012.

 1. e

  environmental JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,054
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  CCM MNA UKOSEFU WA KINGA YA UFISADI

  kumbu kumbu zangu na kusoma historia Tanzania imekuwa na maspika Adam Sapi Mkwawa [1] 1964 November 19, 1973Erasto A.M. Mang'enya November 20, 1973 November 5, 1975 Adam Sapi Mkwawa November 6, 1975 April 25, 1994 Pius Msekwa April 28, 1994 November 20, 2005 Samuel Sitta December 26, 2005 2010 Anne Makinda 12 November 2010 . katika mabunge niliyoshuhudia uhai wangu wakati wa chama kimoja CCM wabunge walikuwa machachari na walikuwa wanatoa shilimgi kwenye bajeti. Kama mnakumbuka G 55 UKISIKIA NJELU KASAKA AU TUMTEMEKE SANGA unajua ni moto.

  Baada ya siasa ya vyama vingi mvuto na maana ya bunge ulipungua sana sababu maslahi ya chama kwanza halafu baadaye maslahi ya taifa.

  Siasa za upinzani kuwa na uwakilishi bungeni Zilianzia na mbunge wa kwanza wa Ujiji Dr Walid Amani Kaborou. chama cha upinzani chenye nguvu Kilikuwa NNCR mageuzi cha mheshimiwa Agustino Lytonga Mrema. NCCR mageuzi ilikuwa na wabunge wengi wa upinzani matatizo na mizozo ndani ya chama ikakisabaratisha Vyama vya upinzani vimekuwa na mataizo ya kuto kuaminiana hasa pale ambapo hujui nani katumwa na nani kuvuruga chama. Bahati nzuri historia haijifichi kila mtu atajulikana nia yake na chama au vyama vitajifunza jinsi ya kuwatambua watu wake. CCM imekuwa madarakani muda mrefu na fahamu zake za kufikia ukingoni ziko mbali mno.

  CCM ilifikiri itaendelea kuwanyonya wananchi, ilifikiri inaweza kuwadhibiti wasema kweli na wasio woga kwa rungu lake la utawala bahati mbaya muda umewatupa mkono. Wabunge wa CCM wana chaguliwa na wananchi kama watakitumikia chama kwa kulinda mafisadi wanajinyima nafasi zao za kuchaguliwa.japokuwa bado wanafikiri wananchi wanasubiri hongo wakati wa kupiga kura wajionee wenyewe mambo yanavyokwenda kombo Wananchi wanataka wabunge safi wenye kuwatetea wakati wote na wakweli wa haki.

  Spika ni mtu muhimu sana katika bunge pia anahusika kwenye vikao vya chama spika Ana makinda atakumbukwa kuwa spika ambaye amekumbana na bunge Gumu katika historia ya tanzania, Ingawa mgeuzi haya yalianzia kwa Samwel sita ambaye Najua ana hasira za kunyimwa uspika , hasa labda kutokana na kujitoa muhanga kupinga mafisadi wazi wazi.

  Pamoja na nia Njema ya Samwel Sita sijui kama ndio ulikuwa wakati wake muafaka wa kupambana na mafisadi mimi naona alichelewa mno kuonyesha makali yake. Kuokoa uhai ni muhimu au aliamua kupigana siku nyigine na imekuwa sasa.

  Je kama CCm inachukia wapinzani sababu itakuwa nini? labda wanafichua madudu ya CCM je CCM inachaguliwa ili kuficha madudu yake?Tunataka madudu ya CCM yafichuliwe na wana CCM . CCM jiandae kuwa chama cha upinzani jisafishe ingawa uchafu umezidi kiwango labda mjifute kabisa.
   
Loading...