CCM mmeishiwa?

In short CDM can not be gauged the same way as CCM, CDM haijaunda serikali, haikusanyi kodi na wala haina dola. Whilst CDM would gain more credit for more sensible talk that is not the case with CCM which need to doing more. CCM need no more to be a party of promises but a party of action. That is what ruling parties are supposed to be doing.

Haiingii akilini pale mwenyekiti na baadhi ya viongozi wa CCM wanapo-pretend kuwa outsiders, walalamikaji na watazamaji wa matukio.
 
CCM lazima muelewe hizi ni harakati na nyie ndiyo “makaburu wetu”, “ndiyo wakoloni wetu” ndiyo mabepari wetu na makabaila wetu” Mnahitaji kutuonyesha kwa vitendo kwamba hamko hivyo na si porojo na malumbano. Hii support wanayoipata chadema nyie mmekuwa nayo kwa zaidi ya miaka 40, ni support inayokuja kwa imani wala haina bei (TANU never bought it). You guyz have squandered that, and you now really have to prove urselves up. Msione wivu kwa uungwaji mkono huu wa Chadema ambao ni bure na whole-heartedly ( JF is a good example). Ndivyo ilivyo siku zote kwa chama cha ukombozi kama ilivyokuwa kwa TANU, ANC, MDC, ODM etc.

Ukaribu wa wananchini na chama ndio unaohalalisha ushabiki na mapenzi ya wananchi kwa chama. Ukiona kiongozi anaanza kugawa kadi apigiwe kura, anagawa kanga au pesa apate kura au mahudhurio katika mkutano ni vizuri kuretreat maana chama huwa kimepoteza dira (Kolimba). Sasa CCM iko katika hali gani, bila kofia, fulana, kanga, hela nakuwabeba watu katika mikutano, mambo hayaendi. CCM bye:A S 103:
 
Sidhani kama hapa nimekuwekea mipaka ila nimeuliza tuu mchango wako wewe ni upi

Anywayz naona mkuu umenikomalia pamoja na kwamba sikutaka tuingie huo upande kwa sasa. Lakini so far ukiacha kodi nimeshatoa vitabu 600 kwa shule tatu tofauti, Sasa hivi tunashirikiana na mbunge wetu kujenga madarasa ya shule ya kata, na pia nipo kwenye mikakati ya kufunga windmill kwa ajili ya kupump maji kijiji fulani huko Mbeya.
 
CCM lazima muelewe hizi ni harakati na nyie ndiyo "makaburu wetu", "ndiyo wakoloni wetu" ndiyo mabepari wetu na makabaila wetu" Mnahitaji kutuonyesha kwa vitendo kwamba hamko hivyo na si porojo na malumbano. Hii support wanayoipata chadema nyie mmekuwa nayo kwa zaidi ya miaka 40, ni support inayokuja kwa imani wala haina bei (TANU never bought it). You guyz have squandered that, and you now really have to prove urselves up. Msione wivu kwa uungwaji mkono huu wa Chadema ambao ni bure na whole-heartedly ( JF is a good example). Ndivyo ilivyo siku zote kwa chama cha ukombozi kama ilivyokuwa kwa TANU, ANC, MDC, ODM etc.

Ukaribu wa wananchini na chama ndio unaohalalisha ushabiki na mapenzi ya wananchi kwa chama. Ukiona kiongozi anaanza kugawa kadi apigiwe kura, anagawa kanga au pesa apate kura au mahudhurio katika mkutano ni vizuri kuretreat maana chama huwa kimepoteza dira (Kolimba). Sasa CCM iko katika hali gani, bila kofia, fulana, kanga, hela nakuwabeba watu katika mikutano, mambo hayaendi. CCM bye:A S 103:

Sawasawa mkuu na ukiangalia kiundani CCM hawakereki na Mgao wa umeme, wala barabara mbovu, wala umaskini na hali ngumu za watanzania. Ila wanakereka sana Mwenyekiti wao akisemwa vibaya au CCM ikitajwa kupoteza dira. Hapo utamsikia kila mwanaCCM and apologists wakitaka kuchangia hoja.
 
Anywayz naona mkuu umenikomalia pamoja na kwamba sikutaka tuingie huo upande kwa sasa. Lakini so far ukiacha kodi nimeshatoa vitabu 600 kwa shule tatu tofauti, Sasa hivi tunashirikiana na mbunge wetu kujenga madarasa ya shule ya kata, na pia nipo kwenye mikakati ya kufunga windmill kwa ajili ya kupump maji kijiji fulani huko Mbeya.

Hapa nakupongeza sana kwa mchango wako na naamini utaendelea kutoa kwa kadri utakavyoweza
Ila naomba nikuombe kitu kimoja elimu ya uraia ni kitu muhimu sana wananchi wajielewe waelewe haki zao waelewe ni nini wanatakiw awafanyiwe na waifanyie serikali yao waulize matumizi ya kodi zao waulize viongozi wao waliowachagua ziko wapi ahadi zao walizoahidi waikatae rushwa na kiongozi anayetoa rushwa wamuone ni msaliti wajue wana wajibu wa kuitetea nchi yao na kuwapenda viongozi ambao wanatimiza majukumu yao na sio wale wanaojaza matumbo yao. Waelewe huduma zao za kimsingi ambazo wanatakiwa wazipate kutoka serikalini ni zipi na mchango wao kama wananchi ni upi
 
Sawasawa mkuu na ukiangalia kiundani CCM hawakereki na Mgao wa umeme, wala barabara mbovu, wala umaskini na hali ngumu za watanzania. Ila wanakereka sana Mwenyekiti wao akisemwa vibaya au CCM ikitajwa kupoteza dira. Hapo utamsikia kila mwanaCCM and apologists wakitaka kuchangia hoja.

Mkuu Nyambala inaonekana kama haya matatizo sijui hawayapati maana sioni hata kama wanayasemea au kuyatolea matamko utasikia tuu tamko la kulaani maamndamano au sijui nini ila sijasikia mtu katoa tamko la kupinga mgao wa umeme au barabara mbovu wilayani kwake as if barabara zote za tanzania ni lami tupu mpaka kule vijijini
 
Mkuu Nyambala inaonekana kama haya matatizo sijui hawayapati maana sioni hata kama wanayasemea au kuyatolea matamko utasikia tuu tamko la kulaani maamndamano au sijui nini ila sijasikia mtu katoa tamko la kupinga mgao wa umeme au barabara mbovu wilayani kwake as if barabara zote za tanzania ni lami tupu mpaka kule vijijini

This is what alwayz amazes me, yaani hao jmaa huwa siwaelewi kabisa...
 
This is what alwayz amazes me, yaani hao jmaa huwa siwaelewi kabisa...

Yaani wanakaa wanapoteza muda na kulipana posho ya vikao wanatoa tamko la kulaani maaandamano kwa nini wasitoe tamko la kuitaka serikali ijenge zahanati kule katika kila kijiji na yenye huduma zote kwa ajili ya kinamama wanaojifungulia vichakani na majumbani
 
CCM Mmeishiwa?


Kuna kila dalili kwamba kile chama chetu kikongwe kinapitia wakati mgumu kuliko muda wowote katika uhai wake. CCM na wanaCCM wamejikuta wanashangaa jinsi walivyopoteza mvuto kwa wananchi, hawafahamu aidha makusudi au bahati mbaya ni kwa nini wamepoteza umaarufu.


Wote tunakumbuka CCM walichaguliwa tena kuingoza Tanzania katika uchaguzi uliopita -2010 (Suala la uhalali au uhalisi wa matokeo ni nje ya mada hii). CCM walikuwa na ilani waliyoinadi nchi nzima kuhusu ni namna gani watakavyotawala na kufufua matumaini ya mtanzania. Zaidi ya hayo waliahidi miahadi kem kem. Cha kushangaza CCM imeisahau ilani yake na ahadi zake, miezi karibu nane toka kuapishwa na hatimaye kuundwa kwa serikali mpya tunashuhudia malumbano tu. Ni kana kwamba CCM ilichaguliwa kwa ajili ya kuja kulumbana na upinzani. Inasikitisha na kushangaza pale baadhi ya viongozi wa CCM wanataka tuamini mgao huu wa umeme umeletwa na Chadema, ufisadi umeletwa na Chadema, umasikini umeletwa na Chadema, ukosefu maadili umeletwa na Chadema etc.
Inashangaza kuona chama kikongwe na chenye wakongwe wa siasa kuamini wapinzani wake ni chadema pekee.


Naomba nikiri kwamba mimi sio political scientist, lakini nimesukumwa na mapenzi ya hatima ya nchi yetu hivyo ntajaribu kuelezea kwa namna nnavyoelewa.


Wapinzani wa CCM ni nani?


1. Competitive Opposition (Wapinzani shindani) – Hawa ni vyama pinzani kama CHADEMA, na wanaoamini kwamba wana sera bora na zinazohitajika ili kuweza kushinda uchaguzi ujao. Mojawapo ya Jukumu kubwa la hawa ni ku-expose weaknesses za chama tawala ili wao wachaguliwe uchaguzi ujao. Kundi hili lina wafuasi ambao si lazima wawe wanachama wa vyama hivyo . Humu kuna Anti-establishment na anti-status quo (Wasiopenda utaratibu wa utawala uliojilimbikiza na uliopo) – Hili ni kundi kubwa mno linahusisha wananchi wa kawaida,wanaoitwa au kujiita wasomi, technocrats, wanamegeuzi, wapenda mabadiliko, middle class na hata wana-CCM. Kifupi hili ni kundi linaloamini we are better than we are, we deserve better roads and general infrastructure, better schools, better housing, better hospitals and everything just as better. na kwamba hatuwezi kuishi ndoto hii chini ya utawala na uongozi wa CCM.

2. Cooperative Opposition (Wapinzani shirikishi) - Hawa mara nyingi hawalengi uchaguzi ujao, wao hasa ni kutaka sera mbadala wanazoamini zitekelezwe na utawala ulio madarakani na ikiwezekana ziwe intergrated ndani ya sheria na utaratibu wa serikali iliyo madarakani, Bahati mbaya hawa huwa hawawezi kuiping serikali hadharani, au kuonyesha hadharani udhaifu wake. Kundi hili ni kama vile unions (allied to the ruling party), NGO’s za mlengo huo, wanachi na hata baadhi ya vyama vya upinzani, bahati mbaya humu ndiyo pia mara nyingi chimbo la mafisadi. Ushiriki wa unions na NGO’s kwa upinzani huu mara nyingi ni temporary na hutegemea competence ya serikali iliyo madarakani.

Cha ajabu aidha kwa bahati mbaya au makusudi CCM, Viongozi wake, wanachama wake na hata waanzilishi wake wanapenda upinzani wa kundi la pili tu. Wanaliona hilo ni kundi friendly, easy to manipulate na easy to live with. Ukichunguza vizuri unakuta hata hoja zinazotolewa dhidi ya Chadema ni some sort ya kushangaa kwamba inakuwaje hawa wa kundi la pili wanataka kuwa la kwanza.

CCM inashindwa kabisa kulewa Chadema inatoa wapi support na kwa nini watu wana-sympathize nayo.CCM inashangaa na inaona wivu ni kwa nini Chadema inapendwa na vijana, Chadema inaaminiwa na watanzania kadri siku zinavyokwenda.

C’moon Chadema ni chama cha ukombozi na tumaini la wafuasi wa kundi la kwanza la upinzani. Chadema haaiihitaji kuwa kwanza “perfect” ili ndiyo iaminiwe kupewa madaraka, CCM haijawahi kuwa hivyo, TANU haikuwahi kusubiri kuwa perfect ili itawale, vivyo hivyo ANC na hata ODM. Inashangaza CCM inapojipa madaraka ya kutaka kutuamulia aina ya upinzani. CCM eti wanaiona Chadema sio “perfect” kutuongoza.

CCM lazima muelewe hizi ni harakati na nyie ndiyo “makaburu wetu”, “ndiyo wakoloni wetu” ndiyo mabepari wetu na makabaila wetu” Mnahitaji kutuonyesha kwa vitendo kwamba hamko hivyo na si porojo na malumbano. Hii support wanayoipata chadema nyie mmekuwa nayo kwa zaidi ya miaka 40, ni support inayokuja kwa imani wala haina bei (TANU never bought it). You guyz have squandered that, and you now really have to prove urselves up. Msione wivu kwa uungwaji mkono huu wa Chadema ambao ni bure na whole-heartedly ( JF is a good example). Ndivyo ilivyo siku zote kwa chama cha ukombozi kama ilivyokuwa kwa TANU, ANC, MDC, ODM etc.

CCM sio tu mkae nje ya fence bali mnatakiwa mkae ng’ambo ile. Mtuambie mafanikio yenu, ilani yenu, uthubutu wenu katika kuindoa nchi ndanni ya lindi la umasikini. Mnapofika mahali na kuonekana kazi yenu ni kujibizana na chadema ndiyo kabisaaaa mnazidi kujiharibia na kuonekana you just need to go. Kwanza nashangaa ni kwa nini mna hata hicho cheo cha uenezi, uenezi wa nini na wapi?

Mnapolalamika eti kuna watu na wanasiasa wapinzani wameamua kumchafua mwenyekiti wenu na familia yake ili kuwalinda the so called mapacha watatu ni hoja ya kitoto, kwani hao mafisadi mnao huko huko. Na haihitaji Chadema ili kuwachukulia hatua.

Hata siku moja udhaifu wa Chadema will never be CCM’s strength. Chadema itaendelea kupendwa hivyo hivyo na udhaifu wake maana so far is the only reliable alternative. CCM you have no authority whatsoever hata ya kutufikikirisha what our alternative should be.

CCM lazima muelewe Chadema will cease every opportunity ili kuwa competitive opposition. A mere promise from Slaa is more powerful kuliko an ill-accomplishment ya JK. Hivyo ndivyo siasa ilivyo. Stop playing in Chadema’s book otherwise ndiyo mnatuongezea hasira sisi tunaoamini mme-overstay, you are irrelevant na hamna jipya


Nawakilisha!

Ujumbe huu sio kwa CCM, Ujumbe huu ni kwa watanzania wote wanaotaka mabadiliko,
unatusukuma kutaka mabadiliko zaidi, unatusukuma tuichukie ccm zaidi, unatusukuma
tuipende CHADEMA zaidi, unatupa matumaini kwamba firka, matakwa, hoja, mahitaji
na malengo yetu yako sawa sawa kabisa na inatukumbusha kwamba bado kidooogo
tupate ukombozi wa pili
 
Miaka iliyobaki ni ya kukimbizwa mchakamchaka kila kona,sasa hivi sio mwananchi kukimbizwa mchaka mchaka ni zamu ya wakubwa kwani tumechoka
 
Hebu ona kwanza, CCM wana kitu kama hiki?
Falsafa ya Chama
1. Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika “Nguvu na Mamlaka ya Umma” (The People’s Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao.
2. Aidha falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni.
3. Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.
4. Historia inaonyesha kuwa “UMMA” wa Watanzania haujawahi kuwa na sauti, mamlaka na madaraka juu ya maamuzi ya hatima ya maisha ya watu. Uhuru, nguvu, mamlaka na madaraka wakati wote, tokea enzi za ukoloni mpaka leo, vimekuwa vikihodhiwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wana mamlaka ya kuongoza SERIKALI na kuwakandamiza wananchi.
5. CHADEMA tunaamini kuwa mifumo na miundo ya utawala wa nchi yetu havijawapo kwa ajili ya kuutumikia umma, bali umma ndiyo huzitumikia serikali hizo ambazo ni mali ya watu wachache wanaopoka “Nguvu ya Umma”. Sambamba na hilo, umma wa Watanzania umekuwa hauna mamlaka ya mwisho ya kuhoji maamuzi ya serikali yanayowaathiri watu, na hivyo kujikuta hauna mamlaka juu ya rasilimali, sheria, utawala, na uendeshaji wa nchi. Aidha, Katiba ya Nchi imekuwa miliki ya Serikali kwa kutumia Bunge ambalo linatawaliwa na mawazo kongwe ya ukiritimba wa enzi za mfumo wa Chama kimoja cha siasa nchini.
6. CHADEMA tunaamini na kutambua kuwa “kuchaguliwa” kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi wachaguliwa kujitwalia mamalaka ya UMMA na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza “waliowachagua” kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.
7. Hivyo basi, falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki.
8. Falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” inalenga kuwaamsha, kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwaandaa Watanzania wachukue hatua ya kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao tofauti na kipindi cha miaka mingi chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na miaka kumi na nne ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi.
 
Nyambala ujumbe umetufika,kwa kweli tunahitaji kuona matunda yatokanayo na ilani
 
Back
Top Bottom