CCM mmeishiwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM mmeishiwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyambala, May 24, 2011.

 1. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  CCM Mmeishiwa?


  Kuna kila dalili kwamba kile chama chetu kikongwe kinapitia wakati mgumu kuliko muda wowote katika uhai wake. CCM na wanaCCM wamejikuta wanashangaa jinsi walivyopoteza mvuto kwa wananchi, hawafahamu aidha makusudi au bahati mbaya ni kwa nini wamepoteza umaarufu.


  Wote tunakumbuka CCM walichaguliwa tena kuingoza Tanzania katika uchaguzi uliopita -2010 (Suala la uhalali au uhalisi wa matokeo ni nje ya mada hii). CCM walikuwa na ilani waliyoinadi nchi nzima kuhusu ni namna gani watakavyotawala na kufufua matumaini ya mtanzania. Zaidi ya hayo waliahidi miahadi kem kem. Cha kushangaza CCM imeisahau ilani yake na ahadi zake, miezi karibu nane toka kuapishwa na hatimaye kuundwa kwa serikali mpya tunashuhudia malumbano tu. Ni kana kwamba CCM ilichaguliwa kwa ajili ya kuja kulumbana na upinzani. Inasikitisha na kushangaza pale baadhi ya viongozi wa CCM wanataka tuamini mgao huu wa umeme umeletwa na Chadema, ufisadi umeletwa na Chadema, umasikini umeletwa na Chadema, ukosefu maadili umeletwa na Chadema etc.
  Inashangaza kuona chama kikongwe na chenye wakongwe wa siasa kuamini wapinzani wake ni chadema pekee.


  Naomba nikiri kwamba mimi sio political scientist, lakini nimesukumwa na mapenzi ya hatima ya nchi yetu hivyo ntajaribu kuelezea kwa namna nnavyoelewa.


  Wapinzani wa CCM ni nani?


  1. Competitive Opposition (Wapinzani shindani) – Hawa ni vyama pinzani kama CHADEMA, na wanaoamini kwamba wana sera bora na zinazohitajika ili kuweza kushinda uchaguzi ujao. Mojawapo ya Jukumu kubwa la hawa ni ku-expose weaknesses za chama tawala ili wao wachaguliwe uchaguzi ujao. Kundi hili lina wafuasi ambao si lazima wawe wanachama wa vyama hivyo . Humu kuna Anti-establishment na anti-status quo (Wasiopenda utaratibu wa utawala uliojilimbikiza na uliopo) – Hili ni kundi kubwa mno linahusisha wananchi wa kawaida,wanaoitwa au kujiita wasomi, technocrats, wanamegeuzi, wapenda mabadiliko, middle class na hata wana-CCM. Kifupi hili ni kundi linaloamini we are better than we are, we deserve better roads and general infrastructure, better schools, better housing, better hospitals and everything just as better. na kwamba hatuwezi kuishi ndoto hii chini ya utawala na uongozi wa CCM.

  2. Cooperative Opposition (Wapinzani shirikishi) - Hawa mara nyingi hawalengi uchaguzi ujao, wao hasa ni kutaka sera mbadala wanazoamini zitekelezwe na utawala ulio madarakani na ikiwezekana ziwe intergrated ndani ya sheria na utaratibu wa serikali iliyo madarakani, Bahati mbaya hawa huwa hawawezi kuiping serikali hadharani, au kuonyesha hadharani udhaifu wake. Kundi hili ni kama vile unions (allied to the ruling party), NGO's za mlengo huo, wanachi na hata baadhi ya vyama vya upinzani, bahati mbaya humu ndiyo pia mara nyingi chimbo la mafisadi. Ushiriki wa unions na NGO's kwa upinzani huu mara nyingi ni temporary na hutegemea competence ya serikali iliyo madarakani.

  Cha ajabu aidha kwa bahati mbaya au makusudi CCM, Viongozi wake, wanachama wake na hata waanzilishi wake wanapenda upinzani wa kundi la pili tu. Wanaliona hilo ni kundi friendly, easy to manipulate na easy to live with. Ukichunguza vizuri unakuta hata hoja zinazotolewa dhidi ya Chadema ni some sort ya kushangaa kwamba inakuwaje hawa wanaotakiwa kuwa wa kundi la pili wanataka kuwa la kwanza.

  CCM inashindwa kabisa kulewa Chadema inatoa wapi support na kwa nini watu wana-sympathize nayo.CCM inashangaa na inaona wivu ni kwa nini Chadema inapendwa na vijana, Chadema inaaminiwa na watanzania kadri siku zinavyokwenda.

  C'moon Chadema ni chama cha ukombozi na tumaini la wafuasi wa kundi la kwanza la upinzani. Chadema haaiihitaji kuwa kwanza "perfect" ili ndiyo iaminiwe kupewa madaraka, CCM haijawahi kuwa hivyo, TANU haikuwahi kusubiri kuwa perfect ili itawale, vivyo hivyo ANC na hata ODM. Inashangaza CCM inapojipa madaraka ya kutaka kutuamulia aina ya upinzani. CCM eti wanaiona Chadema sio "perfect" kutuongoza.

  CCM lazima muelewe hizi ni harakati na nyie ndiyo "makaburu wetu", "ndiyo wakoloni wetu" ndiyo mabepari wetu na makabaila wetu" Mnahitaji kutuonyesha kwa vitendo kwamba hamko hivyo na si porojo na malumbano. Hii support wanayoipata chadema nyie mmekuwa nayo kwa zaidi ya miaka 40, ni support inayokuja kwa imani wala haina bei (TANU never bought it). You guyz have squandered that, and you now really have to prove urselves up. Msione wivu kwa uungwaji mkono huu wa Chadema ambao ni bure na whole-heartedly ( JF is a good example). Ndivyo ilivyo siku zote kwa chama cha ukombozi kama ilivyokuwa kwa TANU, ANC, MDC, ODM etc.

  CCM sio tu mkae nje ya fence bali mnatakiwa mkae ng'ambo ile. Mtuambie mafanikio yenu, ilani yenu, uthubutu wenu katika kuindoa nchi ndani ya lindi la umasikini. Mnapofika mahali na kuonekana kazi yenu ni kujibizana na chadema ndiyo kabisaaaa mnazidi kujiharibia na kuonekana you just need to go. Kwanza nashangaa ni kwa nini mna hata hicho cheo cha uenezi, uenezi wa nini na wapi?

  Mnapolalamika eti kuna watu na wanasiasa wapinzani wameamua kumchafua mwenyekiti wenu na familia yake ili kuwalinda the so called mapacha watatu ni hoja ya kitoto, kwani hao mafisadi mnao huko huko. Na haihitaji Chadema ili kuwachukulia hatua.

  Hata siku moja udhaifu wa Chadema will never be CCM's strength. Chadema itaendelea kupendwa hivyo hivyo na udhaifu wake maana so far is the only reliable alternative. CCM you have no authority whatsoever hata ya kutufikikirisha what our alternative should be.

  CCM lazima muelewe Chadema will cease every opportunity ili kuwa competitive opposition. A mere promise from Slaa is more powerful kuliko an ill-accomplishment ya JK. Hivyo ndivyo siasa ilivyo. Stop playing in Chadema's book otherwise ndiyo mnatuongezea hasira sisi tunaoamini mme-overstay, you are irrelevant na hamna jipya


  Nawakilisha!
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Ujumbe mzuri ila sidhani kama utawafikia walengwa wako busy kwa sasa
   
 3. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Tutajitahidi uwafikie!!!!! Angalau wausome tu hata wakiamua kupuuza.
   
 4. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa! Umtendeavyo mwenzako ndivyo nawe utatendewa! CCM Mwaka jana walimwambie Mr. Seleli hana mvuto wa kisiasa wakamwengua kwenye post yake ya kugombea ubunge wakampa jamaa aliyeshika nafasi ya 3 kwenye kura za maoni. Sasa kama wanajua mtu anaweza kupoteza mvuto wa kisiasa basi na sasa watambue kwamba na wao CCM wamepoteza mvuto wa kiasia kama walivyomchomekea bwana Seleli.
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ndiyo hijvyo mkuu inashangaza pale wanapokuwa wanaoukimbia kimbia ukweli!
   
 6. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Kukubali ukweli kwa binadam yoyote inakuwa ngumu sana na wengi wetu kukubali kuw asometime kuna sehemu tumeanguka inabidi tunyanyuke na tuendelee na safari inakuwa ni ngumu. So ujumbe kama huu kukubalika inakuwa ngumu sana maana japo kuna kuanguka bado anajiona amesimama na hakuna tatizo lolote na kama ni nguvu bado anazo na bado ana mapenzi yale yale aliyokuwa nayo mwanzoni wakati mambo yamebadilika. Kukubali kuwa kuna down and ups na then zile downfal kuzifanyia kazi inakuwa ni safi sana ila nani yuko tayari kufanya hayo
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hapana mkuu hii ni tabia iliyoendekezwa hapo Tanzania tu na baadhi ya watu!
   
 8. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Sasa ni namna gani ya kuiondoa hii tabia maana imeshakuw amazoea unaweza kumuona mtu amechafuka na ukamwambia aise una uchafu kwenye nguo akakukatalia kabis akuwa ule sio uchafu ni rangi yake
  Njia mbadala ya kufikisha ujumbe mkuu inakwua tatizo na tatizo sio kulilea ni kulitatua liondoke na watu wasonge mbele.
   
 9. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Anywayz lakini sidhani kama hiyo inakuzuia kumwambia kuendela kumwambia na ikiwezekana kumwonyesha exactly mahali palipochafuka!
   
 10. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Utawafikia tu mkuu,nafikiri wanatembele mitaa hii.
   
 11. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wengine nawaona hata sasa!
   
 12. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Ok kuna wakati mtu anaweka pamba masikioni hasikii wala haelewi ni nini kinachoendelea na anaweza akawa na macho ila haoni yeye akiona red allert anaona kama ni kijani inamtruhusu kwenda hapo k una kazi sana kuhakikisha kuw aujumbe unawafikia walengwa
   
 13. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Wanatembelea ila wanawaona kama nyie ni wachochezi hakuna lolote ni nyie tuu mnazusha kila kitu kiko salama
   
 14. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Na hii ndiyo haswaa kwa nini nimeamua kuandika ujumbe huu!
   
 15. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Huwa wanasema udongo uwahi ungali maji ili kuweza kukutengeneza chungu katika mtindo unaoupenda maana hata kama ni zege likipoa linaganda halifai tena kwa kazi. Sasa hapa ni kuondoa unafiki na wanasema call a spade a spade na sio big spoon. Kusema kweli kuwa kuna sehem tumefulia kuna sehem tumekosea na wajirekebishe na waonekane wamejirekebisha waacha siasa za chuki za kupakana matope na wajivue unafiki walio nao waseme kweli tulipotoka na tumejua tumepotoka tumejirudi na sasa tufanye kazi mliyotutuma

  Je Nyambala yuko wa aina hii
   
 16. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #16
  May 24, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kwa siasa inayoendeshwa miaka hii na watanzania wasivyo mabwege tena watalazimika tu kuwepo wa aina hiyo!
   
 17. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Ukiwa kama kijana upi mchango wako wewe
  pambana mahali ulipo kuhakikisha kuwa kika kitu kinaenda linavyotakiwa
   
 18. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu ningeomba uanzishe Mpango Maalumu Wa Eilimu Ya Siasa Kwa Walioikosa(MMESIKWA).
  Unaweza ukawasaidia jamaa zangu wa CCM.
   
 19. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #19
  May 24, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Sijui wameziba masikio na maxcho maana hawasikii wala hawaoni maana unawez ahata kuwaanzishia shule na bado wakachemsha
   
 20. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #20
  May 24, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  This is just a matter of common sense mkuu!
   
Loading...