Ccm mmechoka! Magamba mapya kwa nyoka mwenye kansa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm mmechoka! Magamba mapya kwa nyoka mwenye kansa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Analyst, Apr 15, 2011.

 1. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Wanachojaribu kukifanya CCM kujiokoa na kupoteza umaarufu kwao naona hakiwasaidii lalote zaidi ya kusema watapoteza fedha bure endapo watatumia mabadiliko ya juzi ktk CC na Secretariet kujinadi kwa wananchi kwamba tayari wao ni chama safi na kinachowafaa wananchi kuliko Chadema.
  Ninachoamini mimi kazi ya CDM ni kuwakumbusha tu wananchi (walioanza kuelewa) ‘wizi mtupu' uliojaa ndani ya chama tawala kwa kudhania kwamba watanzania wa leo ni sawa na wa karne iliyopita na kwamba watapelekwa hovyo hovyo. Kila mtu mwenye akili timamu anajua Mramba, Yona na Mgonja ni watuhumiwa wa ufisadi lakini sababu ya wao kuwa mahakamani wakati mafisadi wazito zaidi yao kama wale wa Kagoda, Richmond na Dowans wako huru ni kwa kuwa wale hawakuwa wana-mtandao. Hatuhitaji miujiza kuuza tabia chafu za CCM kwa wananchi kwa mara nyingine tena. Kama chama kimejivua gamba basi ndani kina kansa kubwa ya ufisadi, fitna na makundi ambayo hayawezi kwisha kwa kumtoa Makamba na kumweka mwanaye katika CC. Labda kama JK anataka kuleta tofauti ya kweli kwa wananchi ajitoe muhanga kuwashtaki Rostam, Karamagi, Lowasa na wenzao wengi na kufuta mikataba ya kihuni kama ule wa TICSS bandarini, Dowans na ahakikishe reli zetu zinafanya kazi upya kwa malengo ya kulinufaisha taifa na si rafiki zake vinginevyo, CCM kiama kinakuja maana kama si 2015 ni 2020 na mkishindwa mjue na chama kinakufa kabisa.
  Naomba muelewe kama Mungu anatuweka hai mkishindwa tu wote mnakwiba sasa hivi mahakamai mtaingia na ushahidi utatosha. Unadhani wachina wanatoa wapi ushahidi wanapopeleka kesi zao za ufisadi mahakamani.
  Ndiyo maana nasema tena CCM mmechoka! gamba jipya halimsaidii nyoka mgonjwa wa kansa, lazima afe tu. Udhaifu wenu ktk ufisadi na kukosa vision ni kansa kubwa na ya hatari kama ya ubongo.
   
Loading...