Wananchama wengi wa CCM wametia nia ya kugombea nafasi za Udiwani na Ubunge. Moja ya sharti lililowekwa na CCM ni kuwa watia nia wote kwa nafasi za Udiwani na Ubunge kwanza watachujwa na Kamati za Wilaya na Mikoa na hatimaye majina yote kupelekwa Makao Makuu ya CCM - Dodoma kila mmoja akipewa alama na Kamati za Wilaya na Mikoa.
Utaratibu huu ni mzuri lakini kwangu siyo nzuri kwa sababu zifuatazo:-
(1) Utaratibu huu unachochea upendeleo kwa wachache ambao watapata upendeleo kutoka kwenye Kamati za Wilaya na Mikoa na hata Taifa.
(2) Utaratibu huu unachochea RUSHWA . Kwa wale wanaotaka kupitishwa majina yao wanapitisha rushwa kwa Kamati za Wilaya na Mikoa na hata Taifa.
(3) Utaratibu huu unaleta uonevu. Kwa yule mgombea ambaye hana ndugu kwenye Kamati zilizotajwa ataonewa pasipo sababu.
USHAURI WANGU. Ninashauri kuwa wale wote waliotia nia ya kugombea Udiwani na Ubunge majina yao yarudishwe yote kwa wajumbe ili wapigiwe kura ili mshindi/washindi wapatikane kwa njia ya haki bila upendeleo. Kurudisha majina matatu ili waje wapigiwe kura na wajumbe kutaleta manung'uniko makubwa na upendeleo kitu ambacho kinaweza kuchafua Chama chetu.
Nawasilisha.