CCM Mbeya: RPC anatukandamiza sana CCM!

GreenCity

JF-Expert Member
May 28, 2012
5,620
4,265
Nikiwa ndani ya daladala, kupitia Radio IbonyFm Habari nimemsikia katibu wa CCM mkoa wa Mbeya akilalamika kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya RPC DIWANI ATHUMAN amekuwa akifanya kazi kwa upendeleo hasa tangu CCM KUANZISHA KAMBI ya mafunzo kwa vijana wake maeneo ya Ivumwe jijini Mbeya!

Aidha, katibu huyo bila kusita, amemtaja RPC kuikandamiza CCM na kuipendelea CHADEMA hasa kwa kuwakamata vijana kadhaa wa CCM kufuatia kutekwa na kuteswa kwa kiongozi mmoja wa CHADEMA aliyekuwa anakatiza eneo ilipo kambi hiyo ya mafunzo ya CCM. namnukuu "haiwezekani mtu apite KAMBINI kwetu huku amevalia mzura wa CHADEMA na banghi mfukani halafu sisi tumuangalie tu, tena anaanza kuleta ubishi"!

Kwa upande wake RPC amesikika akisema yeye anafanya kazi kwa utafiti lakini anashangaa vyama vyote vikilalamika juu ya jeshi la polisi! pia akijibu kuhusu katibu wa CCM kumlaumu, RPC amejibu "huu ni uzushi...tena kama unaweza kuandika hii andika lakini nasema huu ni uzushi, kama wao wameshindwa majukwaani shauri zao lakini wasije kupotosha watu huku mitaani" alimalizia RPC!

chanzo: Ibony Fm Habari saa 13:00.

wana jamii! huu mtindo wa kuanzisha makambi ya mafunzo ya kujilinda mimi napata wasiwasi nayo!
 
Tukimwambia "nchi imemshinda" anabisha, mara anaanza kulia "amani" wanaanzisha makambi ya fujo, wanategemea Amani itakuwepo?

Ni kwanini anaanzisha makambi ya kijeshi ndani ya Chama? baada tutasikia amani inapotea ama ndio tambiko la ANGUKO
 
Ukina na maccM yanalalamikia policcm ujue ukombozi wa taifa uko mlangoni
 
Tukimwambia "nchi imemshinda" anabisha, mara anaanza kulia "amani" wanaanzisha makambi ya fujo, wanategemea Amani itakuwepo?

Ni kwanini anaanzisha makambi ya kijeshi ndani ya Chama? baada tutasikia amani inapotea ama ndio tambiko la ANGUKO

Hahahahahahaha. Vijana wanaandaliwa KITAMBIKO... JK kwishney
 
-pole yao wanaccm kwa kukandamizwa.Ombi langu tu makambi yao yasifundishe vijana wao kuwa watekaji na wauaji kwa wale wasiokuwa upande wao
 
Hizi kambi tusipozipigia kelele leo,kesho zitatumaliza sisi wenyewe,"Ukicheka na kima utavuna mabua"
 
CCM NI WAGOMVI KWELI SIKU HIZI, tangu lini chama cha siasa kinajishughulisha na mafunzo ya kijeshi ? badala ya kueneza siasa, amani ya nchi hii ikitoweka ccm hamtakwepa lawama hii
 
Wanajifunza kutoa kucha na kung'oa meno bila ganzi,hawa magamba ni mashetani
 
"pia akijibu kuhusu katibu wa CCM kumlaumu, RPC amejibu "huu ni uzushi...tena kama unaweza kuandika hii andika lakini nasema huu ni uzushi, kama wao wameshindwa majukwaani shauri zao lakini wasije kupotosha watu huku mitaani" alimalizia RPC!"

Kama kweli haya yametoka Kinywani mwa RPC, basi u DCP, CP n.k atausikia kwenye Bomba.
Very Soon atarudishwa Makao Makuu Kupewa kazi ya Kupitia Madodoso
 
Ni katiba ipi ya Tanzania inaruhusu chama kuwa na jeshi lake?
 
Ni kweli kuna kambi ya Maninja wa CCM Ivumwe sekondari wakijiandaa na vurugu wakati wa uchaguzi wa Udiwani jumapili kata ya Iyela.

Wanavaa mizula inayofunika nyuso zao.
Kwa asiwe amini aende Ivumwe na Itende Sekondari atayaona haya ninayosema.
 
Kama kweli haya yametoka Kinywani mwa RPC, basi u DCP, CP n.k atausikia kwenye Bomba.
Very Soon atarudishwa Makao Makuu Kupewa kazi ya Kupitia Madodoso

Ndio tatizo la wetendaji wetu wabovu liliko.
Sioni maantiki ya chama kuanzisha kujenga wafuasi wake katika mipasho ya kikakamavu na kupigana, hicho ni chanzo cha vurugu "Tukubali au Tukatae". Na kama taifa limekosa walinzi mpaka baadhi ya vyama vianze kuandaa majeshi yake basi ni wazi kuwa Sasa kila chama kitaanzisha kambi hizo na mwisho wa siku ni Vita tu.
CCM ni vyema kuwa na uzalendo wa kujali maisha ya wananchi wa Tanzania kaliko kujali maslahi ya wachache wanaotaka kukaa madarakani milele.
 
Tatizo CCM wamezoea kubebwabebwa hata wanapofanya makosa anapotokea mtu anaesimamia sheria kikamilifu ana kuwa adui yao.
 
Back
Top Bottom