CCM mazoea hujenga tabia - sasa amani ipooo?

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,898
CCM imezoea miaka yote kubebwa na vyombo vyote nchini na hali kadhalika kubebana wao kwa wao. Sasa mfumo wa demokrasi wa vyama vingi unaposhika kasi ya enzi za utandawazi CCM bado hawajaamka kwani mazoea hujenga tabia. Athari za mazoea kujenga tabia ndio maana ya kuona kuwa wana haki ya kila wanachotaka iwe halali na isipokuwa halali lazima kuhalalisha haramu kwa minajili ya kudumisha kubebwa na kubebana.

Matusi kwa viongozi wa dini ambao wanasaidia kuwafinyanga watu wawe waadilifu kwa vile wanaelekeza kidole kuwafinyanga viongozi wa CCM kuwa waadilifu wanawageuka viongozi wa dini waliokuwa siku zote wanakubali kuwa wanasaidia kuleta maadili katika umma. Dharau na matusi sasa toka viongozi wa CCM yanaelekezwa kwa manabii wa Mungu. Ndio nimeshangaa hata baadhi ya matukio ya dini tulizoea kuhudhuria kama ilivyotokea Kusimikwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza hatukuhudhuria isipokuwa tunatuma sasa wawakilishi jambo ambalo si la kawaida kabisa, kwani waelewa wanajua wazi hizo ni ishara za nyakati.

Baadhi ya viongozi kutumia aya za misahafu kutoka Maandiko matakatifu kujenga hoja ningewashauri kabla ya kujenga hoja kutumia aya za maandiko matakatifu wakutane kwanza na wataalamu wa maandiko matakatifu wafafanuliwe teolojia ya hilo neno la Mungu vinginevyo wananakili na kuainisha kwa maneno yao kitu kilicho nje ya maana kamili ya maudhuri ya habari yake. Huwezi kutumia aya moja kuwa ndio mhimili wa kusimama kujenga hoja bila kusoma sura au paragrafu yote ili kupata maudhui ya neno la Mungu katika maandiko matakatifu. Ninavyojua digrii ya maandiko matakatifu ni ngumu sana katika masomo ya dini kuliko kozi nyingine zote. Ndio maana wanatakiwa kwanza wasome kigiriki, na kusomelea mila, sheria na historia ya taifa la waisraeli ili uweze kuelewa. Lakini kabla ya yote elimu ya kawaida ipande kwanza na kisha usomelee elimu ya falsafa ya kawaida ndipo unaweza jitoma kwenye digrii ya Maandiko matakatifu, vinginevyo hutaelewa nini unachofanya na pengine unaweza changanyikiwa.

Nikirudi nyuma kwenye mambo ya uongozi wa taifa letu na siasa, kuna ishara za wazi kuyumba kwa uongozi baada ya uchaguzi, na mambo kuwa kama yalivyo sasa. Kila mtu anaongea chake, kila mwanasiasa toka chama tawala anaongea anavyoona yeye, kila waziri anaongea kwa mtazamo wake na kutolea uamuzi ikiwa ni ishara wazi kwamba hakuna mshikamano katika mfumo wa uongozi. Viongozi wa juu kutotolea kauli na ufafanuzi katika masuala makubwa kitaifa yanayogusa maisha na usalama wa wananchi inatia wasiwasi sana. Maana amani ya nchi si shauri ya kuimba kama wimbo uwapo jukwaani. Dalili za kuanza kupotea kwa amani ni ishara za dhuluma ya haki katika mambo ya msingi kwa wananchi na taifa. Maana yake wachache waliopewa dhamana na wananchi wanawakosea haki wengi wa raia ambao wenye dhamana katika mambo ya msingi katika maisha yao.

Amani katu haipatikani kwa mtutu wa bunduki, ila maridhiano ya haki kwa wote ndio msingi wa amani kama tulivyozoea tokea tupate uhuru. Utumiaji wa nguvu unazidisha chuki na utengano baina ya raia, vyombo vya dola, viongozi na makundi mbalimbali. Kwa jinsi nguvu inapozidi kutumika na ndivyo amani inavyozidi kudidimia. Haki za kiraia na kisiasa zinapofanyiwa mizengwe ndivyo tunavyozidi kuweka ufa zaidi katika nchi yetu tuliyozoea kuiita kisiwa cha amani. Tulizoea kusikia na kushuhudia tawala za imla duniani na kabisa barani Afrika, na hapa kwetu tusipokuwa makini huu ukandamizaji wa raia wake wanaodai haki, hivyo haki na uhuru wao kwa kukandamizwa kwa mitutu wa bunduki ni dalili wazi za kuota mfumo wa utawala wa imla badala ya kuwa na viongozi wa taifa kama hali ilivyozoeleka.

Iwapo viongozi wataondokana na dhana ya ubinafsi na kuweka mbele maslahi ya uhuru wa vyombo vya sheria, maslahi ya wananchi na taifa, taifa letu bado lingali na amani na hali ni bado tulivu sehemu kubwa ya nchi yetu. Vinginevyo ukandamizaji wa kisiasa, haki za raia na kutokuwa wazi kwa viongozi wetu amani itabaki historia tu.
 
Back
Top Bottom