CCM matokeo ya urais yapingwe mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM matokeo ya urais yapingwe mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, May 18, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=2]CCM matokeo ya urais yapingwe mahakamani[/h]


  Na Muhibu Said  18th May 2012
  [​IMG] Pia yashauri madaraka ya rais yajadiliwe
  [​IMG] Yagusa uteuzi wa waziri mkuu, mawaziri  [​IMG]
  Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete.


  Baadhi ya mambo ambayo yamekuwa yakihojiwa na makundi mbalimbali ya jamii na kutaka yawekwe katika Katiba mpya, likiwamo la kuhoji mahakamani matokeo ya uchaguzi wa Rais, yamekubaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujadiliwa kwa mapana katika mchakato wa kupata Katiba hiyo.

  Mambo hayo yalijadiliwa na kukubaliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM katika semina kuhusu ‘Mwongozo wa CCM katika kushiriki mjadala wa Katiba mpya’ iliyofanyika mkoani Dodoma, Mei 13, mwaka huu na kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo ya makao makuu ya CCM Mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema mambo hayo yanahusu uendeshaji wa serikali na kutaka wananchi wapewe fursa ya kuchangia maoni yao kwa kadiri kila mmoja anavyoona inafaa kwa kuzingatia maslahi ya taifa.

  Aliyataja mambo hayo ambayo alisema yapo wazi kwa mjadala mpana kuwa ni pamoja na mambo yanayosababisha kuwapo kwa kero za Muungano zilizopo, hususan orodha ya mambo ya Muungano.

  Mengine ni utaratibu wa uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, madaraka ya Rais, taratibu za uteuzi wa mawaziri na waziri mkuu, utaratibu wa uteuzi wa tume huru ya uchaguzi na suala la mgombea binafsi katika uchaguzi wa dola.

  Mengine ni kuhusu muundo wa Bunge na Baraza la Wawakilishi na aina ya wabunge na wawakilishi, kuhoji mahakamani matokeo ya uchaguzi wa Rais, uwapo wa baraza la pili la kutunga sheria, ukomo wa idadi ya wabunge, mfumo wa mahakama na nafasi ya Rais wa Zanzibar katika uongozi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano.

  Suala la kuwepo kwa mgombea binafsi limekuwa likipendekezwa kwa muda mrefu, lakini serikali imekuwa ikilipinga licha ya Mahakama kutoa hukumu kadhaa za kuruhusu wawepo.

  Mahakama Kuu ilitoa hukumu mbili za kuwaruhusu katika kesi zilizofunguliwa na Mchungaji Christopher Mtikila.

  Hata hivyo, serikali ilikata rufani katika Mahakama ya Rufani na mwaka 2010, jopo la majaji saba wa mahakama hiyo likiongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu, Agustino Ramadhani, lilibatilisha uamuzi wa Mahakama Kuu kwa kusema kuwa mahakama haina mamlaka ya kuliamua kwa kuwa ni la kikatiba kwa maana ya kutungwa kwa sheria na linapaswa kurejeshwa bungeni.

  Tangu mabadiliko ya 11 ya Katiba yalipomwondoa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais na kubakia kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wazanzibari wamekuwa wakihoji na kulalamika kuwa ameshushiwa hadhi.

  Kuhusu Tume ya Uchaguzi, makundi mbalimbali yakekuwa yakishinikiza kuwepo kwa tume huru kwa madai kuwa tume ya sasa inaundwa na makada wa CCM wanaokipendelea chama hicho.

  Kuhusu uteuzi wa mawaziri na Waziri Mkuu, kumekuwepo na maoni kutoka makundi mbalimbali kwamba mfumo wa Westminster wa kuteua mawaziri kutoka bungeni uachwe badala yake utumike mfumo wa mawaziri kuteuliwa nje ya Bunge ili kuwezesha uwajibikaji.

  Kwa mujibu wa Katiba ya sasa Ibara ya 51 (2) Rais anaruhusiwa kumteua mbunge wa kuchaguliwa kutoka jimbo la uchaguzi anayetokana na chama cha siasa chenye wabunge wengi bungeni au kama hakuna chama cha siasa chenye wabunge wengi zaidi anayeelekea kuungwa mkono na wabunge walio wengi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.

  Waziri Mkuu hatashika madaraka hadi uteuzi wake kwanza uthibitishwe na Bunge.

  Ibara ya 55 (1) hadi (4) inasema kuwa, mawaziri wote ambao ni wajumbe wa baraza la mawaziri watateuliwa na Rais baada ya kushauriana na Waziri Mkuu.

  Mawaziri na naibu mawaziri watateuliwa kutoka miongoni mwa wabunge.

  Vile vile, madaraka ya Rais yamekuwa yakilalamikiwa kwamba ni makubwa mno; kwamba amepewa madaraka ya kuteua wateule wengi kuanzia mawaziri naibu mawaziri, wakuu wa mikoa, makatibu wakuu wa wizara, wakuu wa wilaya, wakuu wa vyombo vya dola, majaji, wakurugenzi na makamishna wa taasisi mbalimbali, wenyeviti wa bodi na wateule wengine.

  Wote hao hawathibitishwi na mamlaka nyingine yoyote nchini.

  Jambo jingine ambalo limekuwa likilalamikiwa ni matokeo ya uchaguzi wa urais kutohojiwa na chombo chochote, ikiwemo Mahakama.

  Ibara ya 41 (7) inasema kuwa iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais, hakuna mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka kuchunguza kuchaguliwa kwake.

  MAMBO 15 YA KUBAKI KATIKA KATIBA

  Hata hivyo, Nape, alisema NEC imetaka mambo 15, ukiwamo muundo wa serikali ya Jamhuri ya Muungano kuwa wa serikali mbili yabaki au yaingie ndani ya Katiba mpya kwa kuwa ndiyo misingi mikuu ya taifa.

  “Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ilijadili na kukubaliana kuwa wanachama na wananchi kwa jumla wahakikishe kuwa misingi mikuu ya taifa letu inabaki katika Katiba mpya itakayoandikwa,” alisema Nape.

  Aliyataja mambo hayo kuwa ni pamoja na kuwapo kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na muundo wa serikali ya Jamhuri ya Muungano kuwa serikali mbili; ambayo ni Serikali Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

  Alisema muundo wa serikali mbili ndio msingi na sera ya CCM, ambayo haina upungufu.

  Misingi mingine mikuu ya taifa aliitaja kuwa ni kuendelea kuwapo kwa mihimili mitatu ya dola (Serikali, Bunge na Mahakama) na kuendelea kuwapo kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kuendelea kuwapo kwa umoja wa kitaifa, amani, utulivu, usawa na haki.

  Alisema CCM haijaona kama ni wakati muafaka wa kuwa na mhimili wanne wa dola ambao ni wa vyombo vya habari, kama ambavyo umekuwa ukitajwa kama mhimili wa dola usio rasmi.

  Misingi mingine ni kufanyika kwa uchaguzi wa mara kwa mara katika vipindi maalum na kuzingatia haki ya kupiga kura kwa kila mtu mwenye sifa zinazohitajika kwa mujibu wa sheria, kuendeleza uhifadhi na ukuzaji wa haki za binadamu na kuheshimu usawa mbele ya sheria, kuendeleza sera ya dola kutokuwa na dini rasmi, bali inaruhusu kila mtu awe na uhuru wa kufuata dini anayoitaka mwenyewe.

  Mingine ni kuendeleza sera ya serikali kuwa ndiye mmiliki wa rasilimali kuu za nchi, hususan ardhi, kuendeleza sera ya kuwapo kwa usimamizi madhubuti wa maadili ya viongozi kwa kuupa nguvu za kikatiba na kuimarisha madaraka ya umma.

  Mingine ni kuhamasisha sera ya msingi ya kujitegemea, kusimamia usawa wa jinsia na haki za wanawake, watoto na makundi mengine maalum katika jamii, kusimamia hifadhi ya mazingira na kuendelea kuwapo kwa Rais Mtendaji.

  Nape alisema baada ya NEC kukubaliana mambo hayo, chama kitaandaa na kupeleka maoni yake kwa Tume ya Rais ya Kukusanya Maoni ya Wananchi kwa ajili ya Mabadiliko ya Katiba ya nchi.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  CCM wanaweweseka tu -- sasa wanataka matokeo ya urais yapingwe mahakamani ni kwa sababu wanajua kuna uwezekani mkubwa sana, tena sana watashindwa kura ya urais 2015 hivyo katiba mpya impe mwanya mgombea wao mshindwa kwenda mahakamani.

  Walikuwa hawataki ushindi wa urais kwenda mahakani kwani walikuwa wao ndiyo wanashinda tu kwa njia mbali mbali zikiwemo zile za haramu, ambazo zingebainika mahakamani.

  KWELI MKUKI NI KWA NGURUWE, wahenga walinena!
   
 3. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  nishahisi 2015 kutakua hakuna Rais, leo ccm ndio inaijua mahakama sio...
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mlitaka katiba mpya ibaki kama ya zamani? au mnataka iandikwe chadema ni lazima waongoze nchi?
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  wanaandaa mazingira eeeh?
   
 6. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,789
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  hii mada ilipaswa isomeke 'CCM YAUNGA MKONO HOJA YA CDM KUHUSU MATOKEO YA URAIS KUHOJIWA MAHAKAMANI" AU "CCM YARUDIA MATAPISHI YAKE"
   
 7. Alfred Daud Pigangoma

  Alfred Daud Pigangoma Verified User

  #7
  May 18, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,778
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Mtiti unaanza mapemaaaaaa na kama kuchukua nchi kwa CHADEMA wamekwisha chukua kilichobaki ni 2015 kufika na kuapishwa tu....
   
 8. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0  Katiba inataka na itajadili maoni ya wananchi na sio maoni ya chama. CCM wajadili hayo kama wananchi wengine na sio kama kikundi kinachotetea maslahi yake.
  Hali ya uchumi wetu hauturuhusu kuwa na mzigo zaidi ambapo mwisho wa yote wanaolipa na kuteseka ni walipa kodi. Jambo ambalo lingependekezwa ni kuwa ikiwa hakuna chama kilichopata zaidi ya asilimia 50 ya kura, kuwepo na duru ya pili ya uchaguzi baina ya vyama viwili vilivyopata kura nyingi zaidi. Kwa mfumo wa sasa na utitiri wa vyama uliopo, kuna hatari siku moja Tanzania kuongozwa na chama chenye asilimia 20 ya kura, halmuradi tu kinaongoza.  Tume ya sasa imeundwa na CCM hii hii inayosema kuwa "sera zake hazina mapungufu".  Hivyo vipengele viwili vinapingana ...mara wateuliwe, mara wasiteuliwe nje ya bunge ...Nyambaf!!!


  Tunakubali kuwa hiyo ni sera ya CCM, lakini kusema haina mapungufu na kama kweli wanaamini hivyo, kwa nini basi wakata pawepo na mabadiliko ya katiba na tusiendelee na sera yao isiyokuwa na mapungufu?

  CCM wafahamu kuwa katiba ni ya wananchi wote na sio ya CCM peke yao. Wananchi wastaarabu wataheshimu maoni yao japo mengine ni pumba, lakini CCM isijipige kifua kuwa sera zao hazina mapungufu, wawaache wananchi waamue kwa uhuru bila ya kuwekewa vipengele ambavyo hawataki vitoke hata kabla katiba haijapitishwa. Wananchi wote waachwe wachangie maoni yao na juu ya Tume ya Katiba kuamua lipi liwemo, lipi lisiwemo, kwa mujibu wa maoni ya wananchi walio wengi na sio kwa mujibu sera zisizo na mapungufu na CCM


  Haya yote yaliyotajwa hapa hivi sasa yamo kwenye katiba na CCM imekuwa ikivunja katiba mfululizo kwa kujimilikisha ardhi na raslimali nchi. Sasa imefikia pahali serikali imekuwa na maana ya viongozi na jamaa zao badala ya kuwa serikali ya wananchi.


  Mambo kama yalivyo sasa, tuna raisi mtendaji ambaye si mtendaji


   
 9. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Alahhhh Kumbe!!!

  Wewe ulijuaje kama CDM itaongoza nchi mwaka 2015.

  CCM imeshakufa bado kuzikwa tu, wana-CCM jiandaeni kuchukua uanachama vyama vingine na nyie mafisadi jiandaeni kuhama nchi. Lazima mali zote mlizoiba mtarudisha, haiwezekani sisi tulalie mikeka nyie mtengeneze mazingira kwenu na watoto wenu kulala katika MAGODORO YA DODOMA!!!

  Haiwezekani sisi twende Hospitali kama hii:-

  WAGONJWA_ZAHANATI_KISAKI[1]_.JPG

  Na nyie na watoto wenu mnaenda India.

  Nyambafuuuuuu!!!!!!!  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
 10. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  CCM wameishiwa hawana jipya.


  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Wanajiandaa kipsychologia kuwa chama cha Upinzani 2015
   
Loading...