CCM Marekani yavurugana, Makamba yuko wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Marekani yavurugana, Makamba yuko wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kinepi_nepi, Jan 14, 2011.

 1. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  TAARIFA YA KIKAO MAALUM CHA USURUHISHI WA MGOGORO
  WA CCM TAWI LA MAREKANI KILICHOFANYIKA
  KATIKA UKUMBI WA SAFARI-HOUSTON TEXAS, TAREHE 02/Januari/2011
  WAJUMBE WALIOHUDHURIA
  1. Frank Matthew Mwenyekiti-Kamati ya usuruhishi/Mwenyekiti wa kikao
  2. Mkude Augustine Katibu-Kamati ya usuruhishi/ Katibu wa kikao
  3. Anthony Rugimbana Mjumbe-Kamati ya usuruhishi
  4. Michael Ndejembi Mjumbe
  5. Misso Temu Mjumbe
  6. Salum Rajabu Mjumbe
  7. Simon Makangula Mjumbe
  8. Isaac Kitogo Mjumbe
  9. Abdallah Nyangasa Mjumbe
  10. Innocent Batamula Mjumbe
  11. Novastus Simba Mjumbe
  12. Miraji Malewa. Mjumbe

  WAJUMBE WALIOSHINDWA KUHUDHURIA
  1. Alvin Lema Kazini
  2. Shaibu Saidi Kazini
  3. Magreth Pambamaji Kazini
  4. James Shemdoe Kazini
  5. Abdulkarim Faraji Safari kikazi
  6. Zainab Janguo Safarini Tanzania
  7. Andrew Sanga Safarini Tanzania

  1.0 Ufunguzi
  Mwenyekiti alielezea kuwa kamati ya usuruhishi imeundwa na Halmashauri Kuu ya CCM Tawi la Marekani ili kumaliza mgogoro uliopo kati ya pande mbili. Kamati ilichukua hatua ya kuonana na Ndg Kitogo, na kumuomba kufanya mkutano wa pamoja. Nao wakaridhia na ndio sababu ya kikao hiki kizito.
  Mwenyekiti alitaarifu lengo kuwa ni kuondoa tofauti zilizopo kati ya CCM-Kitogo na CCM-Ndejembi na kuwa na CCM moja yenye nguvu na mwelekeo wa kichama na kutokuwa na chuki ama makundi.
  Alitaka kikao hiki cha pamoja kitoe maamuzi na mwelekeo bora kwa chama.
  Alifungua kikao saa 1:32 jioni.

  1.1 Kupokea maelezo
  Mr Kitogo:
  Alielezea matatizo ya Mwenyekiti aliyekuwapo madarakani Mr Ndejembi kuwa ni pamoja na
  -Kuendesha chama kama taasisi binafsi.
  -kutopokea maoni/mapendekezo ya viongozi wenzake
  -Kutotoa nyara na nyaraka muhimu za chama ikiwamo kuficha orodha ya wanachama.
  -Kutumia lugha za matusi kwa wajumbe na kuwafokea viongozi wenzake.
  -Kufanya mikutano binafsi bila wajumbe wengine na kutangaza maazimio bila wengine kuhudhuria.
  Kutokana na matatizo mengi walimuandikia barua ya kujieleza ambayo hakuijibu na hivyo kumfukuza uenyekiti na nafasi hiyo akateuliwa yeye-Kitogo kushika kwa muda.  Mr. Ndejembi
  Alielezea kukosa ushirikiano wa viongozi wenzake ambapo kulijitokeza kundi la kumpinga kwa makusudi kutokana ama na umri au uenyeji na hivyo alikuwa na wakati mgumu kufanya kazi na viongozi wenzake
  -Kulikuwa na dharau ya kutosha kutoka kwa wajumbe.
  -Vingozi wenzake walishindwa kutimiza yote wanayoagizana vikaoni.
  -Uzembe, majungu na visa visivyo msingi vimechangia kuleta migogoro na hivyo kuzaa makundi.
  Alitaarifu kuwa viongozi wenzake hawakuwa tayari kufanya uchaguzi na hivyo yeye aliitisha uchaguzi wa wazi, haki na amani na yeye kuchaguliwa kuwa mwenyekiti ambapo viongozi wenzake walikaidi kuhudhuria.

  *Wajumbe walibaini kuwepo kwa ukiukwaji wa katiba kwa pande zote mbili kwa kutokuunda Halmashauri Kuu ya Tawi, kutoitisha Mkutano Mkuu,taratibu za kumfukuza Mwenyekiti zilikuwa batili na uchaguzi uliofanyika ni batili pia.

  Azimio/Maamuzi
  -Tusahau yaliyopita na kuanza upya kwa kufikia maamuzi sahihi ya kukijenga chama kwa pamoja
  -Ilikubalika kuwa wajumbe (wa kila upande) waliopo ni zaidi ya nusu ya idadi ya wajumbe wote maamuzi yatakayotolewa kikaoni ni halali na wasiohudhuria watajulishwa.
  -Maamuzi yatakayofikiwa kikaoni ndio mwelekeo mpya wa CCM Tawi la Marekani

  2.0 Muafaka.
  Baada ya majadiliano ya kina yenye kutumia busara na amani wajumbe kwa pamoja walikubaliana
  -Kuungana kwa pande zote mbili na kuwa kitu kimoja.
  -Iundwe kamati ya uongozi ya kuratibu upya shuguli za chama
  -Uandaliwe uchaguzi mpya, huru na wenye amani ili kupata uongozi wa pamoja.
  -Nyara na nyaraka za chama vikabidhiwe kwa uongozi wa kamati hiyo.
  -Uwepo mshikamano, upendo, utii na nidhamu kati yetu wanachama na kwa viongozi wote.
  Azimio/Maamuzi
  Kamati iliundwa ikiwa na wajumbe watatu (3) kutoka kila upande. Ikiwa ni viongozi wa kutoka kila upande isipokuwa Ndg Ndejembi na Mr Kitogo walioshauriwa kukaa pembeni ili kuondoa sura ya zamani ya mgogoro. Wajumbe wa kamati ni:
  Mwenyekiti Novastus Simba, Katibu Abdallah Nyangasa, Wajumbe Innocent Batamula, Abdulkarim Faraji, Misso Temu
  Na Salum Rajabu .
  Kamati ilikabidhiwa majukumu yote ya msingi ikiwa ni pamoja na
  Kutengeneza dira ya uendeshaji wa chama kikatiba
  Kuandaa uchaguzi wa uongozi mpya
  Kukusanya nyara na nyaraka za CCM Tawi la Marekani

  Kusimamia mtandao wa mawasiliano uliopo na kutengeneza mwingine.

  Kufunga
  Sambamba na wajumbe wengine Ndg Ndejembi alitangaza kukubaliana na maamuzi halali ya kikao. Mjumbe Mkude alitumia nafasi hiyo kumsifu Ndg Ndejembi kwa uasisi wake wa tawi, heshima ambayo haitakufa milele
  Na kumpongeza kwa kukubaliana na maamuzi halali ya kikao.
  Mwenyekiti aliwashukuru wajumbe na alifunga kikao ilipotimia saa 3:17 usiku

  Imeandalia na kusainiwa na

  …………………………. ………………………… ……………….
  Anthon Rugimbana (Mjumbe) Augustine Mkude (Katibu) Frank Mathew (Mwenyekiti)
   
 2. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Sishangai kama tawi liko HOUSTON maana hata zile kesi kubwa kubwa za utapeli wa Watanzania zilikua Houston. Kweli kila mtu na fani yake.
   
 3. n

  niweze JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndio Maana Wapo Marekani? Kilicho Wapeleka Marekani ni Shida za CCM-Tanzania na Wamekwenda Marekani Kueneza Hayo Hayo. Huu zi Unafiki? Wanataka Kurudi Wakisha Maliza Masomo au Kazi? Huu ni Upungufu wa Akili? Hivi Watanzania Kuna Matatizo Gani? Wenzao Bongo Wanataka Kuwaondoa kwa Mapinduzi na Huko Marekani Wanakaa Kuunga Mkono CCM-Tanzania. "Something Wrong Here" Either Brain Dead au Wanataka Kujiunga Kuchukua Checks za Dowans. Kitu Gani CCM Inawafanya Vijana Kuwa Attracted to? Kuna Kigogo Anawadanganya na Amewahahidi Kazi Bongo. Thats It
   
 4. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Hivi na nyie na kukaa kote nje bado hamuoni jinsi hicho chama kinavyotesa Watanzania??nilifikiri kwa uelewa wenu mgekuwa chachu ya kusemea maovu ya hiki chama kumbe na nyie ni wale wale tu,,Mnafikiri mtaonewa huruma mje mpewe mamlaka?
  Nilitegemea mgekuwa mstari wa Mbele kukemea rushwa, udini, uonevu, uzembe unaopandikizwa na CCM kumbe na Nyie ni migogoro?

  Poleni saana natumaini MSEKWA atawatumia babu yenu makamba aje kuwasaluhisha,
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,845
  Trophy Points: 280
  yaani nyie mngejua jinsi bongo unavyotupiga huku msingeendelea na ccm, sema baba zenu wapo juu serikalini
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Jan 14, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hawana kazi za kufanya hao jumlisha na kujipendekeza!Kama wanaipenda sana hiyo sisiem warudi bongo ili waitumikie kwa karibu zaidi!
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Jan 14, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  gademu... sasa na London na Moscow nako vikianza si itakuwa ni tatizo kubwa.
   
 8. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,845
  Trophy Points: 280
  wengi wao ni watoto wa wakubwa ndio wanain'gan'gania ccm huko ughaibuni
   
 10. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #10
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  mafisadi watoto
   
 11. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #11
  Jan 14, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Wafu wanazika wafu wao.
   
 12. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #12
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mimi huwa najiuliza kila siku kwanini popote kwenye tawi la CCM kuna ugomvi, wanagombania nini?
  Faida ya haya matawi ni nini? Kukataa tamaa ya maisha/ufisadi/undugu au nini?
  Tangia yameanza kufunguliwa ni faida gani wameipata ?
   
 13. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #13
  Jan 14, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Duuu, ama kweli sikio la kufa halisikii dawa!! Yaani mparanganyiko ndani ya ccm upo mpaka kwenye matawi yake ya nje ya nchi!! Dhambi ya kuwachezea watanzania itawatafuna mpaka uvunguni. Watakiona cha moto.
   
 14. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #14
  Jan 14, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Aaah kumbe wabongo wenyewe ni wa Houston!
  :clock:
   
 15. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #15
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ukiangalia "Surnames" unaweza kupata ujumbe fulani!

  Hivi hawa wameenda all the way to America kufanya U-CCM! Hawana cha maana zaidi cha kufanya kuliko CCM? w.*.*?
   
 16. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #16
  Jan 14, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  lol..yani watu wa Nyamagana wanawazidi IQs.
   
 17. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #17
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280
  Njaa na akili haviwezi kwenda pamoja hata siku moja, kama kuwenda Marekani ndio kingekuwa kigenzo cha kuwa na IQS kubwa basi Marekani kusingekuwa na clinic za vichaa, kichekesho pale mtanzania akifariki huko marekani, tangazo la msiba na kuomba mchango wa kuusafirisha mwili wa marehemu kurudisha Tanzania linabandikwa michuzi blog kwa wiki mbili, kisa pesa ya nauli isiyozidi dolla 3000. sasa mbwa kama hawa msipoteze muda kuwajadili hapa, wangekuwa na akili wangekuwa na umoja wa kusaidiana na kuzikana, tusingekuwa tunaona tangazo kwenye michuzi blog wakiomba mchango wa kugharamia kusafirisha mwili wa marehemu. na kama wanaota kuja kugombea ubunge eti kisa walikuwa marekani nawasihi kwanza waombe ushauri kwa Laurence Masha.
   
 18. n

  niweze JF-Expert Member

  #18
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama Kuna Mtanzania Anapicha Zao Tuwaone na Familia Zao Wawaone ili Wakitembelea TZ Wasuswe....
   
 19. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #19
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280

  Seek to understand first & then to be understood, wewe hao wakirudi utawaonea wapi? umeshawahi kunywa brekfast yako sea cliff? hao sio wale ndugu zetu ambao tunawachangiaga vipesa mpaka vya visa fee, hapana, hawa wengi wao ni wale ambao baba zao baada kusaini mikataba ya kuifisadi nchi, moja ya asante zao wanazopewaga ni hizo watoto zao kutafutiwa vyuo USA na UK, na tuition fee zao zinagharamiwa na hao majambazi wenzao, wale watoto wanaotokea manzese, magomeni, tandika gongolamboto, wakifika huko ughaibuni wanapiga box kwa hasira ili waje kusaidia familia zao maskini walizoziacha huku nyumbani, hao wanaojifanya ccm wengine hata pocket money ya kutumia ya kila mwezi wanatumiwa na wazazi wao kila mwezi.
  kwa kifupi kabisa hawa ni kula kulala, hakuna wanachokijuwa kwenye maisha yao, hawa hata ukiwaaambia watanzania wanaandama kwa kukosa mkate si hajabu, wakasema kama mikate hakuna si watu wapewe keki!
   
 20. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #20
  Jan 14, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Hee! London kuna matawi kila kona, tena mrngine yamefunguliwa na Msekwa. Hapo London usipime, ndipo CCM ilipo. Walikuja kwenye kura za maoni wakamwagwa wote.
  Sasa kama unalipiwa karo na serikali ya CCM kwanini uichukie! Shauri yao masikini huko TZ. Huu usingizi wa miaka 50 sijui utaisha lini
   
Loading...