CCM Marekani yavurugana, Makamba yuko wapi?

..surnames (rugimbana, ndejembi, simba, janguo)!!! then why these cheap head low wako proCCM!! sio wenzetu hawa!!
 
Hao ni wahuni 20 waishio Houston, Marekani hakuna tawi la CCM hii moja ya njia ya kujitafutia umaarufu ambao hauna maana yoyote.
 
Hee! London kuna matawi kila kona, tena mrngine yamefunguliwa na Msekwa. Hapo London usipime, ndipo CCM ilipo. Walikuja kwenye kura za maoni wakamwagwa wote.
Sasa kama unalipiwa karo na serikali ya CCM kwanini uichukie! Shauri yao masikini huko TZ. Huu usingizi wa miaka 50 sijui utaisha lini

Serikali ni mali ya umma siyo Chama hapo ndipo CCM na viongozi wake wameshindwa kutenganisha
 
Na bado!! Mwaka huu wataparangana hadi wachoke. Tena, kuna taarifa za kiintekijensia kuwa wakifanya kikao kingine watavuruga amani.
 
Hivi chadema tuna tawi nje? Nashauri tuige mfano huu pia

Mkuu ujinga hauigwi hata siku moja, wewe cha kujiuliza au waulize hao ambao wako huko Marekani wameshawahi kuona matawi ya wakereketwa ya Republican au Democratic? itikadi inakaa ndani ya moyo mkuu, hiyo ndio itikadi ya kweli.
Elimu ya bure:
Huitaji matawi rukuki kufanya siasa za kisasa, mfano hai angalia kura walizopata chadema zile za jumla, halafu waulize viongozi wa chadema kwamba chadema ina wanachama wangapi? kitu muhimu kwenye siasa ni supportes. angalia hata simba na yanga zina wanachama wachache sana, lakini zina suppoters wengi zaidi, ambao wengine wako tayari kufa kwa ajili ya upenzi na sio uwanachama. wanachama wengi ni majungu tu kama ccm matokeo yake kuanza kugombea vyeo kama mazuzu.
 
Kama Kuna Mtanzania Anapicha Zao Tuwaone na Familia Zao Wawaone ili Wakitembelea TZ Wasuswe....

Wote wako Facebook na kwa nawavyowajua watu wa Houston hawajaweka privacy settings zozote kwenye picha...unaweza ku-download mara moja...ha ha ha!
 
Ndugu wanajumuia na wana ccm;

Rejeeni taarifa ya bwana Frank Msigwa aliyoitoa Jan. 11. 2011 ambayo kwa mara nyingine tena imezua mtafaruku mkubwa kwenye jumuia yetu yenye amani.
Ni kutokana na mtafaruku huo na ukweli kuhusu taarifa hiyo ndio iliyonifanya nije mbele yenu wanajumuia kutoa ufafanuzi baada ya kuomba radhi kwa mtafaruku huo.

Kama kiongozi wa Tawi hili la CCM napenda kuwaomba radhi wanajumuia na wana CCM kwa yote yaliyotokea na kwamba nitaendelea na jihada za kutosha kuzuia mambo kama haya yasitokee tena.
Kuhusu ukweli wa taarifa hiyo ya bwana Msigwa ni kwamba pamoja na mapungufu makubwa yaliyo katika taarifa hiyo, HAKUNA MAKUBALIANO YOYOTE yaliyofikiwa katika mgogoro huo ingawa kuna jitihada za dhati za kumaliza mgogoro huo.

Mwisho nawasihi wanachama wote wa CCM ambao mmesha jiunga na ccmgroup kutumia mtandao huo kwani kutumia mtandao wa THC kunawakwaza wenzetu ambao si wanachama wa ccm. Na kwa wale ambao hawajajiunga tafadhari fanyeni hima kujiunga ili kujua kinachoendelea na kutoa maoni yenu kwa nafasi bila woga.

NB: TAARIFA ZAIDI ZITATOLEWA KWENYE ccm groups mapema iwezekanavyo,

Michael Ndejembi
Mwenyekiti
CCM - Marekani.
 
hawana kazi za kufanya hao jumlisha na kujipendekeza!kama wanaipenda sana hiyo sisiem warudi bongo ili waitumikie kwa karibu zaidi!
ccm ccm ooh chama cha mapinduzi,ccm nambari one...............
Kazi tunazo mama ni mapenzi ya dhati kwa ccm ndio yanayonisumbua,dr.jakaya wa kikwete yupo juu indeed,,
 
Ndugu wanajumuia na wana ccm;

Rejeeni taarifa ya bwana Frank Msigwa aliyoitoa Jan. 11. 2011 ambayo kwa mara nyingine tena imezua mtafaruku mkubwa kwenye jumuia yetu yenye amani.
Ni kutokana na mtafaruku huo na ukweli kuhusu taarifa hiyo ndio iliyonifanya nije mbele yenu wanajumuia kutoa ufafanuzi baada ya kuomba radhi kwa mtafaruku huo.

Kama kiongozi wa Tawi hili la CCM napenda kuwaomba radhi wanajumuia na wana CCM kwa yote yaliyotokea na kwamba nitaendelea na jihada za kutosha kuzuia mambo kama haya yasitokee tena.
Kuhusu ukweli wa taarifa hiyo ya bwana Msigwa ni kwamba pamoja na mapungufu makubwa yaliyo katika taarifa hiyo, HAKUNA MAKUBALIANO YOYOTE yaliyofikiwa katika mgogoro huo ingawa kuna jitihada za dhati za kumaliza mgogoro huo.

Mwisho nawasihi wanachama wote wa CCM ambao mmesha jiunga na ccmgroup kutumia mtandao huo kwani kutumia mtandao wa THC kunawakwaza wenzetu ambao si wanachama wa ccm. Na kwa wale ambao hawajajiunga tafadhari fanyeni hima kujiunga ili kujua kinachoendelea na kutoa maoni yenu kwa nafasi bila woga.

NB: TAARIFA ZAIDI ZITATOLEWA KWENYE ccm groups mapema iwezekanavyo,

Michael Ndejembi
Mwenyekiti
CCM - Marekani
.

Hapo kwenye RED unamaanisha wewe ndio mwenyekiti wa chama cha majambazi(ccm) Marekani nzima? kweli nimeamini akili na njaa haviwezi kwenda pamoja hata siku moja. maisha yamewashinda hapa Tanzania mmekwenda kuwa wakimbizi huko marekani, badala ya kutafuta mkwanja mnajipendekeza kwenye siasa za majitaka.

ONYO: Kwa yeyote huko mlipo mwenye ndoto za kuja kuwaghiribu watanzania ili agombee ubunge naomba afute ndoto hizo, kabla ya yote mngekwenda kuomba ushauri kwa Laurence Masha.
 
Nyie wanga wa Houston acheni uzushi njaa itawaua, CCM Marekani ? wanga watupu
 
Wengi wa watz wanaokwenda kutafuta maisha majuu wanakimbia hali ngumu ya maisha hapa Tanzania ambayo imechangiwa na utawala wa kiimla na ukiritimba wa ccm. Kinachoni shangaza wakiwa huko wanaiita tena ccm iwafuate huko.

Huu ni ujinga wa kiwango gani?
 
Na bado!! Mwaka huu wataparangana hadi wachoke. Tena, kuna taarifa za kiintekijensia kuwa wakifanya kikao kingine watavuruga amani.
Nimesoma hapo kwenye nyekundu nimebaki nacheka mwenyewe,naona sasa imekuwa msamiati mpya!!
 
gademu... sasa na London na Moscow nako vikianza si itakuwa ni tatizo kubwa.

if we dont care back home, who cares in moscow, London etc....ushenzi kabisa kujifanya unaanzisha ccm ukiwa mkimbizi wa maisha magumu bongo yaliasisiwa na ccm, na ukifika huko unajifanya kuipenda ccm.
 
Inavyoonekana sasa, CCM si chama tu bali ni roho ndiyo maana inasambaa kote kote. Mungu aturehemu na kutuponya ni hii roho!!
 
Vita ya panzi....thank you 4 hizo taarifa za kiinteligensia maana they make us want to pray harder for this country that lacks patriotism from the thithiem!
 
Kujiunga na hiyo CCM inakuwaje? Au ni ule mtindo wa 'Don't ask Don't tell?' hata homo humo humo!
 
CCM ughaibuni mpoo? Hatujawasikia mkitoa tamko lolote juu ya Dowans. Kulikoni?:coffee:
 
Back
Top Bottom