CCM Makambako wapumua

Mlyafinono

Senior Member
Apr 6, 2012
177
47
Wafuasi wa Chama cha magamba wameanza kuvaa maguo yao ya kijani baada ya nape kuhutubia mkutano wa hadhara makambako jana, kabla ya hapo walikuwa wanaogopa kuvaa kutokana na kuogopa kuzomewa na kuitwa mafisadi
 
Makambako haitabiriki ni hao hao waliomzomea Jackson Makwetta (kabla ya Deo Sanga(Jah People)) mbele ya Kikwete kuwa hawamtaki lakini mwisho wa siku walimchagua tena. Otherwise Thomas Nyimbo na Alatanga Nyagawa (Lutondwi) wanatakiwa waongeze kasi ya mabadiliko hasa ukizingatia kuwa Makambako pana young vibrant population kubwa tu.
 
Suala la kuangalia hapa ni je idadi ya waliohudhuria mkutano wa CHADEMA na CCM ni sawa? au je ni upi ulikuwa na watu wengi? Hicho kinaweza kuwa kipimo cha awali
 
HIYO MAKAMBAKO YA WAPI UNAIONGELEA WEWE? maana aibu waliyoipata jana ni kubwa mno,kwanza walilazimika kukodi bajaji zaidi ya 20 ambazo hazikuwa na abiria hata mmoja na kuwalipa sh.elf 5 kila bajaji nkwa ajili ya kuongeza msafara toka majengo hadi uwanja wa polisi makambako (0.5km) na bajaji zilipofika uwanjani zote zilitawanyika na kutupa bendera walizopewa ,walipofika uwanjani hakukuwa na watu wa kutosha ikalazimu nape asubirie watu waongezeke ndo ahutubie,alipokuwa anahutubia alipoanza kuiponda cdm wananchi walianza kumzomea ikabidi aanze kutukana hali iliyozidisha hasira kwa wananchi na kuanza kumzomea zaidi,ilipofika saa 10;39 alimua kumaliza mkutano ,alipokuwa anaondoka alikutana na umati wa mikono ya wana cdm ndo akatukana kwa kwa vidole,WATU WENYEWE WALIKUWA WACHACHE SANA,HAO HAO WACHACHE WALIMZOMEA,WATU WALIOIHUDHURIA MKUTANO WAKE HAWAFIKII HATA NUSU YA MKUTANO WA SUGU NA SILINDE WALIPOKUWA WANAFUNGUA MATAWI YA CDM MAY 6.HII NDO HALI HALISI YA KILICHOTOKEA JANA
 
Tweve ukisha andika umbea hivi unajisikiaje?

UMBEA AMA UKWELI? MI NASIMULIA NILICHOKUTANA NACHO JANA MAANA NILIKUWEPO KUANZIA MWANZO WA MATUKIO HADI MWISHO WA MKUTANO,AU UNATAKA NIKUAMBIE NA MATANGAZO YA UJIO WAKE YALIKUWAJE NA YALITANGAZWA SIKU NGAPI?WE NAONA umesimuliwa!
 
Back
Top Bottom