Kwa hadhi ya mzee Mkapa na hapa namwita mzee sio ati kwa vijisenti vyake bali hakika kiumri ni mzee, unapomsikia akitukana tena wakati anajua wazi kuwa dunia nzima inamwangalia na kumsikia, naona ccm tumekwisha. CCM wameona kuwa hawana tumaini hivyo wakaamua angalao, tushibe matusi tu.
Ndo maana hata yule mjukuu wa mkapa alipopewa nafasi ya kuwatukana babu zake, Magufuli alimpigia makofi. Sera ya matusi sijui inaleta maendeleo gani au inawasaidiaje vijana wetu waliokata tamaa na kuamua kubwia unga na kuwa makontena. This is a shame to this nation.
Naomba msamaha kwa niliyemwudhi
Ni kweli, CCM sasa maji yako shingoni. Si mkapa pekee anayehubiri matusi karibu kila anayesimama jukwaani, kwenye mitandao na hata redio na vijigazeti uchwara vinafanya kazi moja tu ya kutukana!
Ndiyo, CCM inaelekea kaburini kwani tuliyozowea kuyaona kwa baadhi ya wapinzani miaka ya nyuma sasa tunayashuhudia CCM! Baadhi ya wapinzani walikuwa wakikusanya watu kwa magari kuwapeleka sehemu walizofanya mikutano na kuondoka nao; na sasa ndiyo haswa kinachofanyika na CCM, hawawezi kufanya mkutano utakaovutia watu kwa hiyari hadi kulazimika kusomba watu toka hadi mamia ya kilometa, kuwalipia chakula na kuwapa nguo, kofia na hata fulana na kukodi wasanii mahiri nchini kwa gharama za mamilioni ili kuwavutia watu kwenye mikutano yao! Ilifanyika Mwanza, Dsm, Geita, Arusha, Moshi na karibu sehemu zote alizotembelea Maghufuli!
Baadhi ya wapinzani hapo nyuma walilaumiwa kwa umahalia na itikadi; CCM ya sasa inahubiri kwenye majukwaa wakisikilizwa na dunia nzima ati "Hatuwezi kuwapa urais wa Kaskazini" labda wakimaanisha CHADEMA na UKAWA!
CCM hii si ile aliyoiacha Nyerere, imetekwa na majangiri, majambazi, vibaka, vibakauchumi na hata wauza unga. Wapo waliotuhumiwa kujihusisha na biashara ya mihadarati ambao hadi leo ndiyo makada!
Si kazi ngumu kutabiri matokeo ya Jumapili ijayo ya 25/10/2015; yatakuwa sawa na yale waliyokuwa wakipata baadhi ya wapinzani waliokuwa wakisomba watu kuuhadaa ulumwengu juu ya kukubalika kwao. inashangaza kuona jinsi wapinzani walivyobadilika safari hii bila kutoa hata chembe ya tusi kwa CCM bali wanaendelea kumwaga sera zao.
CCM sasa wamepagawa; wanaahidi chochote hata mbingu! Maghufuli anaahidi kuigeuza Tanzania kuwa ya Viwanda, uongo ambao hata mtoto ataujua. Nyerere alitumia miaka zaidi ya ishirini kuweka misingi ya viwanda ambao manyang'au hawa waliibomoa kwa mwango mmoja tu na sasa wanaahidi kujenga upya kwa miezi isiyozidi sitini!
Wasubiri kuhukumiwa na umma walioubeza, kuudharau na kuupuuza hadi kuwaita malofa na wapumbavu.
Jumapili ijayo itaamua adhabu yao.