CCM:Maalim Seif afukuzwe serikalini

CCM:Maalim Seif afukuzwe serikalini

Greenwhich

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
1,337
Reaction score
968
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mjini Magharibi, Borafya Silima ambaye amechaguliwa hivi karibuni amesema kwamba nafasi aliyopata ni muhimu katika siasa za Zanzibar na kwamba ataitumia vizuri na kuwataka wapinzani wake wajipange vizuri ili kukabiliana nao kwani wameingizwa madarakani kwa maridhiano.

Kauli hiyo imetolewa jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mabata huko Magomeni Mjini Unguja na kuhudhuriwa na wanachama wa CCM na wafuasi wa CUF ambapo mgeni rasmi wa mkutano huo alikuwa ni Mwenyekiti wa Mkoa wa Mjini Magharibi Borafya Silima.​

Borafya alisema Maalim Seif amekuwa amepewa wizara zisizo na uzito wowote serikali na hivyo amekuwa akimuonea choyo makamo wa pili wa rais, Balozi Seif Ali Idd kwa kuwa yeye ndio mshughulikiaji wa wizara zote za serikali.
Mazungumzaji katika mkutano huo ambao kwa kiasi kikubwa wote waliohutubia walimlenga na kumshutumu moja kwa moja Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad na kumtaka aachie ngazi kwa kuwa ameshindwa kutekeleza yale ambao aliapa kuyasimamia wakati akiingia madarakani.
Mbali na matusi ya nguoni na kumshutumu kwamba anahusika na kundi la Uamsho walisema Maalim Seif hafai kuwa kiongozi kutokana na kuwa mbinafsi kwa kuwa ameisema serikali yake mbele ya viongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) kwa kuwaeleza kwamba jeshi la polisi na vikosi vya SMZ vinahitaji mafunzo ya kukabiliana na vurugu ili waweze kupata mafunzo ya kukabiliana na vurugu hizo bila ya kuvunja haki za binaadamu.
“Huyu Maalim Seif anawaambia UNDP kwamba jeshi letu la polisi linahitaji mafunzo ya kuwakamata wahalifu sisi tunamwambia polisi wetu na vikosi vyetu havihitaji mafunzo wewe ndio unahitaji mafunzo kwa sababu kwani wewe unalindwa na nani? Si hawa hawa polisi” alisema Khalifa.
Katika hatua nyengine viongozi hao wa CCM walimtaka Maalim Seif kuachia ngazi kwa kwa kumsema rais wake Dk Shein hadharani kitendo ambacho walisema ni kwenda kinyume na kiapo chake cha kuheshimu, kulinda na kutotoa siri za serikali.
Hivi karibuni katika mkutano wake Maalim Seif alimtaka Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein kutekeleza ahadi yake ya kuwalinda wananchi wote bila ya ubaguzi na kuhakikisha vyombo vya ulinzi vinasitisha ukiukwaji wa haki za binaadamu kwa kuwa wananchi wamechoshwa na ukandamizaji wanaofanyiwa katika nchi yao.

Source:H@ki Ngowi
​
 
Migogoro ndani ya ndoa kawaida sasa naona niyo imeanza migogoro!!!
 
kwa sasa na mimi nakubaliana na huyu jamaa kwamba Maalim Seif hafai kuwa kiongozi wa juu kwa kuwa ni kigeugeu na mwenye kiherehere.na zaidi si mtu makini kupima matamshi yake kwa jamii anayoiongoza!
 
Du..!Mambo yamenza sasa.Nyerere alisema ukianza ubaguzi hutabaki salama.Waliungana wakaanza kubagua wabara sasa naona dhambi inawaridia wenyewe.
 
Maalim namchukia kwa vitendo vyake vya kusupport uamsho na redio iman.
Naamini ccm wanaijutia sn ndoa yao na cuf hasa kutokana na huyu mtu.
 
ndoa jamani ina mgogoro....hehehehehehe:majani7:
 
Maalim namchukia kwa vitendo vyake vya kusupport uamsho na redio iman.
Naamini ccm wanaijutia sn ndoa yao na cuf hasa kutokana na huyu mtu.
Tulisha sema humu jamvini kuwa Uamsho ni mradi wa Maalim Seif.
Na sasa wamemtibua kwa kuwa yule Sheikh aliyetumwa kuongoza Uamsho hadharani kwa vile yuko ndani na hana jinsi ya kumtoa huko.
 
maalim seif ni kunguru,hafugiki,ukimfuga we mchawi
 
Marriage without consent is nothing!
 
Na aliomba hata mwezi mungu amsemahe! .... yakuwa maneno mazito sana yale

Du..!Mambo yamenza sasa.Nyerere alisema ukianza ubaguzi hutabaki salama.Waliungana wakaanza kubagua wabara sasa naona dhambi inawaridia wenyewe.
 
Tulishasema kuwa Seif alipowekwa kinyumba akageuzwa nyumba ndogo ya CCM alipaswa kutimuliwa CUF. Sasa angalia anaanza kudharauliwa na kila mtu kutokana na uroho wake wa madaraka na kuwachuuza wenzake.
 
Their marriage has broken down irrepairably.
 
Sawa sawa? Maalim anawazuga tu wapemba wenzake kishaufyata mkia siku hizi hana tena mvuto,na ukitaka kujua msaliti no 1 wa znz ni maalim kawaingiza mkenge wenzake na ndoa na ccm sasa kakiuwa chama chote cuf hawana tena,na kwa sbb makubaliano yao na ccm kwa sbb wanashabihiana kura,subiri 2015 cuf hawatafikia zile kura miaka ya nyuma,na hapoa hawatakuwa na sifa tena ya kuunda serikali ya umoja kwa hiyo ccm watakuwa wao tu,hiyo ndio mbinu ilikuwa kuimaliza cuf
 
Msije kusema Chadema inahusika na huo mgogoro wenu. Wakati mnakubaliana mlikua peke yenu na kuyamaliza myamalize peke yenu...nadhani mmegundua adui yenu sio mtanganyika bali adui wa mpemba ni muunguja na adui wa muunguja ni mpemba..!
 
Hivi nani alikuwa shahidi wa hii ndoa yao?

Msije kusema Chadema inahusika na huo mgogoro wenu. Wakati mnakubaliana mlikua peke yenu na kuyamaliza myamalize peke yenu...nadhani mmegundua adui yenu sio mtanganyika bali adui wa mpemba ni muunguja na adui wa muunguja ni mpemba..!
 
Tulishasema kuwa Seif alipowekwa kinyumba akageuzwa nyumba ndogo ya CCM alipaswa kutimuliwa CUF. Sasa angalia anaanza kudharauliwa na kila mtu kutokana na uroho wake wa madaraka na kuwachuuza wenzake.

Mkuu usisaha haya ni matatizo ya viongozi wengi mno wakiafrica wao ni uchu wa madaraka na mali tu,usimsahau John garang aliwaingiza sudan kusini vitani miaka 22 lakini alipoambiwa atakuwa makamu wa rais wa al-bashir mara 1 alikubali na kurudi kuwahadaa watu wake,unajua mungu huwa hamfichi mnafiki wiki 2 tu zilitosha kutoa uhai wake kwa ajali ya helkopta,sasa hapo unajiuliza maiak 22 umepiga vita bora ungefia huku unatetea haki za wenzako wangekukumbuka kama shujaa,lakini wiki mbili tu zimetosha kuthibitisha unafiki wake alikuwa nao kwa sudan kusini,
 
Mkuu asante sana hata mkiwabagua Waislamu ndani ya chadema haitaishia hapo itaendelea kula tu.
Du..!Mambo yamenza sasa.Nyerere alisema ukianza ubaguzi hutabaki salama.Waliungana wakaanza kubagua wabara sasa naona dhambi inawaridia wenyewe.
 
Back
Top Bottom