CCM kama CCM bila rushwa na nguvu ya dola (teuzi, polisi, matumizi ya mabavu, Bungeni huko, n.k.) wana mbinu gani za ushawishi hebu niambieni. In short CCM ya leo kwa nguvu ya hoja ni sifuri; wanachojua wao ni kulazimisha hoja zao zipite kwa nguvu badala ya ushawishi. Tumeshuhudia haya BMK, Bunge la Jamhuri, na kwenye platforms nyingine nyingi.
Ni mwana-CCM yupi leo atasimama hadharani ashawishi wananchi kwa hoja maridhawa pasi na matusi, vitisho, personal attack, vitimbi, dharau, kejeli, na mambo kama hayo? Kwamba nchi haitolewi kwa vikaratasi ndio hoja zenyewe hizo? CCM ya leo sio ile ya Nyerere wala msidanganye watu.