Kukuwazabanga
Member
- Jan 12, 2017
- 19
- 178
Kuwapuuza wapinzani wetu bila kuwakabili kwa mbinu sahihi na za kisasa hakuwaondoi wanazidi kujijenga.
Kusema tuachane na gwajima anayetumika na chadema kukibomoa CCM ni kujidanganya na mwanzo wa kushindwa.
Kudhani kuwa gwajima hana impact hivyo tukae kimya ni kujidanganya.
Kudhani kuwa TLS iliyo chini ya CHADEMA leo haina impact kisheria na mahakamani ni kujidanganya.
Lazima tufahamu kuwa TLS members ni wasomi na wameweza kutekwa na CHADEMA.
CHADEMA wametumia mbinu wakaikuza TLS na Lisu.
Lazima CCM tufanye mikakati na mbinu tujue tulipokosea tupange mashambulizi kwa kasi. Tusijidanganye kuwa nothing has happened.
Mahaba na ushabiki bila mbinu tutaendelea kuzidiwa kete kila mara hasa mahakamani na ktk siasa za propaganda.
Kama wapo hawajui siasa za propaganda na madhara yake niwakumbushe tu kuwa Adolf Hitler wa Ujerumani aliwatia mzuka wanajeshi wake kwa propaganda tu wakiwa wamekata tamaa na vita vikaanza upya.
USSR ilianza kuangushwa kwa propaganda hata kabla ya vita.
KANU kiliangushwa kwa propaganda tu za wapinzani hata kabla ya KANU kusambaratika.
ANC leo kinaelekea kuanguka kwa propaganda tu za Malema.
Wana CCM tusome tutumie mbinu. Mahaba tu na ushabiki havitoshi.
Leo propaganda na mbinu imeukuza TLS na Lisu. Hatujui kesho ni mbinu ya kukuza na kubomoa kipi.
Mwalimu Nyerere aliwahi kutuasa kuwa hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kudhani kuwa hayapo. Tukubali kuna tatizo na tuunde mbinu ya kupambana nalo. Mzaha mzaha mguu hutumbua usaha.
Itakuwa ni makosa kuipuuza CHADEMA kwa mahaba tu ya CCM. Tunafaa kuipuuza CHADEMA kwa kuharibu mbinu zao kwa mikakati yenye tija vinginevyo. Hatari ipo mbele.
Haya tusiyangoje tu kutoka kwa mwenyekiti wa CCM Taifa Ndugu Magufuli. Sasa atafanya mangapi. Lazima tuwe wabunifu kumsaidia na kukisaidia chama chetu cha Mapinduzi.