CCM lazima ife tu!

CCM lazima ife tu!

Kashaijabutege

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2010
Posts
2,696
Reaction score
740
CCM kama chama kikongwe hakitarudisha imani ya wananchi ati kwa kuendesha propaganda zisizo na mashiko dhidi ya CHADEMA. Dawa ni kuacha yale wanayoyachukia wananchi (ufisadi, mfumuko wa bei, rushwa, n.k) na si kufikiri kuwa maradhi yao yamesbabishwa na CHADEMA.

Ikumbukwe kuwa, hata CHADEMA ikidhoofu, bado watanzania wataendelea kutoipenda serikali ya CCM kwa kuwa tatizo lao si vyama, bali ni vyama hivyo kutotimiza ahadi zake kwa wananchi.

Ninanavyoona, CCM itakufa kifo kibaya kwa kufikiria kuwa kikifa CHADEMA basi wao watasitawi. Labda watwambie kuwa walistawi kwa kuwa hakukuwa na CHADEMA; na kama si hivyo, kifo cha CCM kina karibia.

CCM inanikumbusha riwaya ya "LAZIMA UFE JORAMU" nami nasema "LAZIMA UFE CCM".
 
Utakufa wewe utaicha ccm imala na itatawala milele ccm ni chama kubwa!!!
 
ccm kama taasisi lazima itakufa kwa hakuna kilichozaliwa na hakikufa na umri wa tasisi unategemea na jinsi itakavyosimamia malengo yake na kukaa kwenye mstari.

ccm imeondoka kwenye mstari na imepotea njia.ccm sasa hivi ni kampuni na kazi yake ni kupora rasilimali za taifa na kumilikisha walio madarakani wake zao waume zao,watoto wao,vimada wao na wapambe wao.


mimi nasema sisiem ni LAZIMA IUWAWE KAMA ITACHELEWA KUFA YENYEWE YENYEWE.
 
Mtasubiri sana mtasali sana mtakesha sana lakini ccm inasonga chadema chama cha wachaga kitakufa kitakiacha ccm chama cha kitaifa kina dunda kidumu chama cha mapinduzi.
 
Utakufa wewe utaicha ccm imala na itatawala milele ccm ni chama kubwa!!!

Kama nyie wenye akili hii ndio mnaotegemewa na CCM, basi kumbe CCM inasubiri mazishi tu. Hivi unafahamu haujawahi kuokea utawala uliokuwa na nguvu kama utawala wa RUMI? leo uko wapi? Ndugu yangu CCM ilishakufa kilichobaki inapumulia kwenye mashine tu kwa msaada wa vyombo vya dola na mifumo kandamizi iliyokuwepo toka enzi za chama kimoja
 
naita muujiza kwakweli............
kwani ulifikiri CCM itadumu milele?? mbona utawala wa farao nao ulikoma tu??
nafikiri ishu sio kufa bali itakufa lini??
na haitakufa 2015 ama 10 yrs to come, no na ukiangalia kwa upana zaidi kabla ccm haijafa cdm itakuwa imeshakufa kitamboooooooo yani itakuwa imesatowek akwenye ramani ya tanzania.
 
Ndg yangu pole usifananishe ccm na rumi, ccm ina mtaji wa wapiga kura wengi sana vijijini tofauti unavyo tegemea wewe kama huamini tembelea vijini kipindi cha sherehe za ccm utakuta wananchi wakicheza ngoma na kula nyama wakifurahia kuzariwa kwa ccm. Hivyo basi kama wewe unategemea ccm itakufa kesho utasubiri sana mkubwa.
 
Ndiyo kabisa; ccm lazima ife kwa sababu isipokufa Tanzania yetu itaangamia
 
Huu mkono wa huyu binadamu mbona haudondoki?? Akasema fisi.
 
Mbona ccm ishakufa inasubiriwa kuzikwa tu hapo 2015.

unatumia kigezo gani mkuu? Ccm ndio chama kilichounda serikali,kina wabunge zaidi ya 250,kina mtandao wa uongozi kuanzia shina,tawi,kata,wilaya nchi nzima hadi taifa na zaid kinachanja mbuga kwa kutekeleza ilani yake ya uchaguzi.acha kujidanganya mkuu.
 
Kama nyie wenye akili hii ndio mnaotegemewa na CCM, basi kumbe CCM inasubiri mazishi tu. Hivi unafahamu haujawahi kuokea utawala uliokuwa na nguvu kama utawala wa RUMI? leo uko wapi? Ndugu yangu CCM ilishakufa kilichobaki inapumulia kwenye mashine tu kwa msaada wa vyombo vya dola na mifumo kandamizi iliyokuwepo toka enzi za chama kimoja

tunashauriwa kutumia kichwa kufikiri sio tu kufugia nywele peke ake.kupembua na kuchanganua mambo mbalimbali na kuyafanyia maamuzi sio kufuata tu upepo
 
unatumia kigezo gani mkuu? Ccm ndio chama kilichounda serikali,kina wabunge zaidi ya 250,kina mtandao wa uongozi kuanzia shina,tawi,kata,wilaya nchi nzima hadi taifa na zaid kinachanja mbuga kwa kutekeleza ilani yake ya uchaguzi.acha kujidanganya mkuu.

Hao wabunge wamechaguliwa na wananchi au rushwa? Wabunge wachache sana wamepita ki-haki wa ccm wengi magumashi tu!!!!
 
CCM ikiwa hai itakua njema zaidi nafikiri kutakua na chalenge kwa chama kitakacho madarakani mda huo. Kwani CCM itakapo shindwa itajifunza mengi, na sifikirii kama itahitaji ushindani itaendelea kuyakumbati mambo yanayo wa gharimu ivi sasa., itabadilika
 
CCM kama chama kikongwe hakitarudisha imani ya wananchi ati kwa kuendesha propaganda zisizo na mashiko dhidi ya CHADEMA. Dawa ni kuacha yale wanayoyachukia wananchi (ufisadi, mfumuko wa bei, rushwa, n.k) na si kufikiri kuwa maradhi yao yamesbabishwa na CHADEMA.

Ikumbukwe kuwa, hata CHADEMA ikidhoofu, bado watanzania wataendelea kutoipenda serikali ya CCM kwa kuwa tatizo lao si vyama, bali ni vyama hivyo kutotimiza ahadi zake kwa wananchi.

Ninanavyoona, CCM itakufa kifo kibaya kwa kufikiria kuwa kikifa CHADEMA basi wao watasitawi. Labda watwambie kuwa walistawi kwa kuwa hakukuwa na CHADEMA; na kama si hivyo, kifo cha CCM kina karibia.

CCM inanikumbusha riwaya ya "LAZIMA UFE JORAMU" nami nasema "LAZIMA UFE CCM".

acha ndoto za mchana wewe, serikali ya ccm imejenga mtandao wa barabara za lami nchi nzima,imejenga shule za sekondari kila kata nchi nzima,imejenga vyuo vikuu kadhaa na hivyo kuongeza graduate kutoka ef 3 hadi ef 30 kwa mwaka na sasa inaboresha miundombinu ya reli nchi nzima.usitumie kichwa kufugia nywele peke ake
 
Hao wabunge wamechaguliwa na wananchi au rushwa? Wabunge wachache sana wamepita ki-haki wa ccm wengi magumashi tu!!!!

unajifariji tu wewe,hiyo ndio sababu itakayowafanya muendelee kugongwa na kitu chenye ncha kali kichwani.tafuteni sababu ya msingi ya kushindwa kwenu msisingizie jua eti ndio inayowafanya mkauke
 
CCM kama chama kikongwe hakitarudisha imani ya wananchi ati kwa kuendesha propaganda zisizo na mashiko dhidi ya CHADEMA. Dawa ni kuacha yale wanayoyachukia wananchi (ufisadi, mfumuko wa bei, rushwa, nk.

ni vyama hivyo kutotimiza ahadi zake kwa wananchi.

.

suala la mfumuko wa bei ni la kidunia mkuu, marekani,ulaya na dunia nzima inayumba kiuchumi kwa sababu ya mfumuko wa bei..wewe uko dunia gani?? Pili ni kero zipi za wananchi ambazo serikali ya ccm haijazitatua? Mawaziri kadhaa leo hii wana kesi mahakamani,barabara zimejengwa nchi nzima na bado ccm inaendelea kujenga miundombinu mingine ya uchumi ikiwemo kuhakikisha nchi ina umeme wa uhakika, sasa hebu be specific ili ueleweke acha malalamiko ya jumla jumla kama mtoto mdogo
 
swala la CCM kufa wala halina mjadala ni muda tu unasubiliwa na si mbali 2015. Tumeona chaguzi uchaguzi 2010 na kugundua CCM imeendelea kuwepo kwa sababu ni mifumo support ya kiserikali kama vile Majeshi yeote, tasisi zote za serikali na Udini kama ngiriba kwa watanzania. Sasa basi kama Vyombo vya dola vitajidaganya kuwa CCM ndio nchi tusubirie mazito 2015 kwani watanzania wanataka mabadiliko ambayo hakuna wa kuyazuia.
CCM ipo madarakani kwa sababu ya Dola na iwapo itaendelea kuitegemea dola kama Polisi mwisho wao si mbali CCM itazikwa rasmi....
 
Back
Top Bottom