CCM kwanini hamtaki Katiba Mpya?

jiwe angavu

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
19,092
35,900
Wasalaam,

Nimekua nikijiuliza maswali mengi sana kuhusiana na mustakabali wa nchi hii na maendeleo yajayo ya watoto na wajukuu zetu.

CCM imekua madarakani kwa miaka zaidi ya 60 sasa tangu tupate uhuru..chakusikitisha zaidi nchi hii imeendelea kupamba na maadui wale wale tangu kupata kwake uhuru.

Hali ya uchumi..kisiasi na kijamii kwakweli bado hairidhishi haki, uhuru wa kidemokrasia, uhuru wa mihimili ya nchi nako ni danganya toto nchi kupitia chama inaamini sana propaganda uchwara bila hata aibu.

Takribani miaka mingi Chama cha Mapinduzi kimekua kikifanyia marekebisho katiba yake ya chama kuendana na uhitaji wa kiuongozi na muda na siku ya April mosi wataenda pia kufanya maboresho ya katiba ya chama.

Swali langu je kama mnaona umuhimu na mlishafanya mabadiliko ya katiba ya chama,shida iko wapi sasa kuruhusu kuwana na katiba mpya ya Jaji Warioba iliyopendekezwa.

Je, mnamuogopa nani au mnaogopa nini?

Lipi hasa tishio kwenu kama nchi ikipata katiba mpya?

Je, mmeshaona kuwa hamna ushawishi tena mbele ya wananchi?

Je, hamtaki nchi ipige hatua katika nyanja za kijamii..kiuchumi..uhuru wa kidemokrasia haki na uhuru wa kiraia.

Je, hofu yenu kubwa sana ni nini?leo tuambieni wazi wazi.

Nchi hii ni yetu sote hakuna mwenye hatmiliki nayo.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom