CCM kwa ujanja nimewakubali

CCM kwa ujanja nimewakubali

makundubhyali

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2013
Posts
2,389
Reaction score
886
Leo hii nimepata nafasi ya kuzungumza mkubwa tu CCM na pia ni nusanusa wao.Huyu bwani alikiri kuwa CCM inawakati mgumu lakini akanithibitishia kuwa watawashangaza UKAWA kwa kuibuka na ushindi 2015. Amesema baada ya kuona uchaguzi huo utakuwa mgumu walishauri mwenyekiti aweke pembeni makubaliano yake na UKAWA wa kupiga kura baada ya uchaguzi mkuu .Aliongeza kuwa hiyo ingelipa Bunge nafasi ya kubadilisha katiba ya hasa kile kipengele cha kuhoji matokeo ya Rais mahakamani ambacho kingekuwa ni mwiba mchungu kwa CCM. Hivyo kwa sasa wana uhakika kama katiba inayopendekezwa ikipigiwa kura mwezi wa nne na ikashindwa kupita itakuwa ni kicheko kwao na watakuwa wamemaliza mchezo kwani hakutakuwa na nafasi kwa Bunge kurekebisha katiba ya sasa hasa kipengele cha kupinga matokeo ya Rais mahakamani na mgombea binafsi ambacho anahofu kitapasua chama kwa kuwa na wagombea binafsi kibaao kitoka CCM hivyo kugawa kura za CCM kwani wagombea wengi wamehatumia hera nyingi kujiandaa hivyo watatumia nafasi ya mgombea binafsi kufikia malengo yao.
Pia aliongezea kuwa hata katiba itapita itajengwa hoja kwamba sheria haziandaliwa hivyo katiba ya sasa itaendelea kutumika. UKAWA KAENI CHONJO SAA MBAYA.
Chanzo mimi mwenyewe ukikataa unaacha.
 
CCM kwa njama hata wa kisimamisha "mbwa" atapitishwa na kuapishwa.Hiyo ndio sad reality ya nchi hii.
 
Hata mimi hii imeniingia kwa kweli. Kwa nini mwenyekiti wa CCM hasimamii maamuzi yake?
 
Mkuu uongo wako mwepesi sana hata dr slaa japo anauelewa mdogo kuhusu mambo ya kisiasa huwezi kumuongopea kitu kama hiki jaribu kutunga uongo wenye mantiki huu watu wengi sana watakustukia sana.
 
Na ninyi Watanzania mnakubali muendelee na maisha haya kwa sababu ccm ni wajanja sana?
Sijaona ubaya wa ccm pengine ni chuki tu ambazo hazina mashiko ccm wanamapungufu yao lakini wamejitahidi kuwa na utawala bora na kuleta maendeleo ya dhati kwa watu wote.
 
Mkuu uongo wako mwepesi sana hata dr slaa japo anauelewa mdogo kuhusu mambo ya kisiasa huwezi kumuongopea kitu kama hiki jaribu kutunga uongo wenye mantiki huu watu wengi sana watakustukia sana.

Hawa ndo masipini dokta wa CCM. Kulinga na malamiko ya kila mwaka wa uchaguzi hasa Zanzibar siwezi kubeza kabisa taarifa hii.
 
Leo hii nimepata nafasi ya kuzungumza mkubwa tu CCM na pia ni nusanusa wao.Huyu bwani alikiri kuwa CCM inawakati mgumu lakini akanithibitishia kuwa watawashangaza UKAWA kwa kuibuka na ushindi 2015. Amesema baada ya kuona uchaguzi huo utakuwa mgumu walishauri mwenyekiti aweke pembeni makubaliano yake na UKAWA wa kupiga kura baada ya uchaguzi mkuu .Aliongeza kuwa hiyo ingelipa Bunge nafasi ya kubadilisha katiba ya hasa kile kipengele cha kuhoji matokeo ya Rais mahakamani ambacho kingekuwa ni mwiba mchungu kwa CCM. Hivyo kwa sasa wana uhakika kama katiba inayopendekezwa ikipigiwa kura mwezi wa nne na ikashindwa kupita itakuwa ni kicheko kwao na watakuwa wamemaliza mchezo kwani hakutakuwa na nafasi kwa Bunge kurekebisha katiba ya sasa hasa kipengele cha kupinga matokeo ya Rais mahakamani na mgombea binafsi ambacho anahofu kitapasua chama kwa kuwa na wagombea binafsi kibaao kitoka CCM hivyo kugawa kura za CCM kwani wagombea wengi wamehatumia hera nyingi kujiandaa hivyo watatumia nafasi ya mgombea binafsi kufikia malengo yao.
Pia aliongezea kuwa hata katiba itapita itajengwa hoja kwamba sheria haziandaliwa hivyo katiba ya sasa itaendelea kutumika. UKAWA KAENI CHONJO SAA MBAYA.
Chanzo mimi mwenyewe ukikataa unaacha.

Kwanza hata kama story yako ingekuwa kweli conclusion yako ya kusema ''ccm kwa ujanja nimewakubali'' inaonyesha ulivyo mtupu. Huo sio ujanja bali ujinga wa hali ya juu (hapo nime-assume story kuwa ni kweli japo sio kweli)! Pili hilo la kupigiwa kura katiba wala usiwe na mawazo kuwa kura za HAPANA ZITASHINDA! Kwa hali yoyote lazima ccm watachakachua kura ili katiba ipite. (walichakachua za wajumbe wa kilichoitwa bunge la katiba ambao hawakufika hata elfu tatu watashindwaje kuchakachua za watu milioni 10++. Na mwisho hilo la kusema eti sijui vipengele vya kuhoji blah blah blah mahakamani wala haviwatii hofu kwani mahakama ni zao na majaji na wao na ikishindikana kabisa watasema ''katiba mpya itaanza kutumika baada ya uchaguzi''.
 
Hawa watakuwa na nia ya kuleta machafuko na wasije wakajaribu kuleta upu.mbavu,mjenga nchi ndiye mvunja nchi. Badala ya sanduku la kura,tutadai rasmali zetu na uchaguzi huru kwa njia ya panga,jembe,fyekeo,jiwe,rungu,koleo,mkuki,nyundo,nondo,fimbo,shoka nk.Tumechoka kutawaliwa na CCM,tumechoka,nasema tumechoka,narudia tena tumechoka.
 
huoni ubaya kwa sababu ya ushabiki uluokupofusha! EPA RICHMOND BOT kuchomwa IPTL Balali gavana kufariki na kuzikwa kwa mwaliko,madini kule buhemba NBC kutolewa km zawadi na madudu yote bado unaona hakuna ubaya!si bure wewe kweli kada! na uchaguzi hujui ccm huwa inashindwa?
 
Kwanza hata kama story yako ingekuwa kweli conclusion yako ya kusema ''ccm kwa ujanja nimewakubali'' inaonyesha ulivyo mtupu. Huo sio ujanja bali ujinga wa hali ya juu (hapo nime-assume story kuwa ni kweli japo sio kweli)! Pili hilo la kupigiwa kura katiba wala usiwe na mawazo kuwa kura za HAPANA ZITASHINDA! Kwa hali yoyote lazima ccm watachakachua kura ili katiba ipite. (walichakachua za wajumbe wa kilichoitwa bunge la katiba ambao hawakufika hata elfu tatu watashindwaje kuchakachua za watu milioni 10++. Na mwisho hilo la kusema eti sijui vipengele vya kuhoji blah blah blah mahakamani wala haviwatii hofu kwani mahakama ni zao na majaji na wao na ikishindikana kabisa watasema ''katiba mpya itaanza kutumika baada ya uchaguzi''.

Naona mawazo yako yako sawa, lakini mbinu ulizotaja ambazo CCM WANAWEZA KUTUMIA ni sehemu ya mbinu za nyongeza kwa alizotaja mleta uzi. Mdharu mwimba huota tende.
 
CCM kwa njama hata wa kisimamisha "mbwa" atapitishwa na kuapishwa.Hiyo ndio sad reality ya nchi hii.
Watanzania ni wagumu wa kuamini lakini ninachowaeleza ni kweli tupu. Huyo bwana pia alinidokeeza kuwa vyama vya upinzani nguvu yao kubwa huwa wanaipeleka kwenye Ubunge na udiwani na kutojari kura za Urais hivyo kutoa mwanya mzuri kwa mambo kufanyika.
 
Back
Top Bottom