CCM kuwabana Mnyika, Kafulila bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM kuwabana Mnyika, Kafulila bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Feb 6, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  CCM kuwabana Mnyika, Kafulila bungeni


  na Mwandishi wetu


  [​IMG] WAKATI mkutano wa 11 wa Bunge ukitarajiwa kuanza keshokutwa mjini Dodoma, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinahaha kuzizuia hoja binafsi za wabunge wa upinzani zisijadiliwe bungeni ili kulinda masilahi ya kisiasa ya chama hicho na serikali yake, Tanzania Daima Jumapili limeelezwa.
  Hoja hizo ni ile ya Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), inayotaka Bunge lijadili na kutoa mwongozo utakaoweka mchakato utakaowezesha kuandikwa na kuridhiwa upya kwa Katiba ya nchi.
  Nyingine ni ile ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) inayoitaka serikali itoe maelezo nchi imefikishwaje mpaka ikashindwa na Kampuni ya Dowans ambayo ilirithi mkataba ‘hewa’ kutoka kwa Kampuni ya Richmond.
  Tayari wabunge hao kwa nyakati tofauti kila mmoja ameshawasilisha kwenye ofisi ya Bunge taarifa ya kutaka kuwasilisha hoja yake binafsi katika mkutano wa Bunge unaoanza keshokutwa.
  Taarifa kutoka ndani ya CCM na ofisi ya Bunge zinasema chama hicho kwa kumtumia spika wa bunge, Anne Makinda ambaye ni mwananchama wake mtiifu, kimepanga kuizuia hoja ya Mnyika kuhusu katiba kwa kutumia njia kuu mbili; moja ni serikali kuwasilisha bungeni muswada wa sheria ya kuweka mchakato wa katiba na tume ya kuusimami na pili ni kuwatumia wabunge wake wawasilishe hoja ya Katiba kama Mnyika.
  “Spika atasema hoja ya Mnyika haiwezi kujadiliwa kwa sababu analotaka kuliwasilisha tayari anaweza kulichangia katika muswada utakaowasilishwa na serikali bungeni kuhusu tume na mchakato wa katiba.
  “Pili, watasema kuna wabunge wengine pia waliowasilisha hoja kama yake, sasa tumpe yupi, tumuache yupi….na muda hautoshi kujadili hoja zote na wala kanuni haziruhusu kujadili suala hilo hilo moja kwa hoja nyingi tofauti,” alifafanua kigogo mmoja wa CCM kwa sharti la kutotajwa jina lake.
  Kuhusu hoja ya Kafulila itakavyozuiwa, taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinasema, watatumia kisingizio cha suala la Dowans kuwa mahakamani ili kuzuia lisijadiliwe bungeni.
  “Watasema Bunge haliwezi kujadili suala linaloshughulikiwa na mhimili mwingine wa dola (Mahakama)”, alisema mtoa taarifa wetu.
  Hata hivyo, akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Kafulila, alisema msingi wa hoja yake ni kutaka kuangalia namna serikali ilivyoshindwa katika kesi hiyo wakati mkataba iliourithi Dowans una utata mkubwa wa kisheria na kwamba suala hilo haliwezi kwa namna yoyote ile kuingilia uhuru wa mahakama.
  Alisema kuwa mazingira ya kesi yenyewe yanaonyesha kuwa hujuma zimefanywa katika uendeshaji huo ndiyo maana yeye amejipanga kuwasilisha hoja hiyo ili Bunge lijadili na kujua kwa kina kilichotokea kwenye kesi hiyo.
  Alibainisha kuwa Tanzania ilishawahi kuvunja mkataba kibabe na Kampuni ya City Water ambayo ilipokwenda ICC ilishindwa pia lakini katika kesi ya Dowans inaonekana kuna mazingira yenye utata zaidi.
  Alibainisha kuwa Rais Kikwete amekiri Richmond ilikuwa haina uwezo wa kuzalisha umeme hivyo mkataba wake ukawa batili hivyo katika mazingira hayo kampuni hiyo haiwezi kuirithisha kampuni nyingine mkataba usio halali.
  “Hebu niambie Ndugu yangu kuna mwizi ameingia ndani na kuiba vitu, ukamuona na kuanza kumkimbiza, wakati ukikaribia kumkamata anaubwaga mzigo aliouiba, je, hutakwenda kumshitaki kwa sababu ya kuwa hukumshika na mzigo?” alihoji Kafulila.
  Aliongeza kuwa hivyo ndivyo inavyofanya serikali ya CCM ambayo sasa imebanwa katika sakata la Dowans na inaamua kuuacha mzigo huo ili isikamatwe.
  “CCM wamekwama kwa sababu wananchi, wanasiasa tumelipigia kelele suala wa malipo haya ya Dowans, sasa wanatafuta pa kutokea, Kikwete na watendaji wake hawawezi kukwepa kuwajibika.
  Wajiuzulu ili tutafute viongozi na watendaji wengine ambao watakuwa mstari wa mbele kujali matatizo ya wananchi na kuyapatia ufumbuzi,” alisema.
  Kuhusu hoja binafsi hiyo kupitishwa na Bunge linaloanza kesho kutwa, Kafulila alisema huu ndiyo mtihani mkubwa kwa Spika Anne Makinda na wabunge wa chama tawala kwa sababu hoja hiyo inagusa masilahi ya taifa.
  Alisema kama Makinda atatumia ufundi wa kanuni kuzuia hoja hiyo basi ajue hasira za wananchi zitakuwa kubwa kwa chama tawala na pia tatizo la umeme halitaweza kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.
  “Ninachokifanya mimi ni kuangalia namna tutakavyotoka kwenye matatizo ya nishati ya umeme ambayo tuna mikataba mibovu pamoja na kutokuwa na umeme wa uhakika, wakifanya hila wataumia.
  Alibanisha kuwa Kanuni ya 150 ya bunge, inaweka wazi kuwa Bunge linaweza kuvunja kanuni yoyote kwa ajili ya lengo la kutimiza jambo fulani lenye maslahi ya umma.
  Kama kuna kanuni itakayozuia mjadala wa Dowans itabidi ivunjwe ili kuruhusu hoja hiyo kinyume na hapo mambo yatakuwa mabaya zaidi kwa CCM.
  Alibainisha kuwa sekta nzima ya umeme ina upungufu, hivyo ni wakati mufaka kuweka mfumo utakaoliwezesha taifa kusonga mbele badala ya wajanja wachache kutumia matatizo ya wananchi kujinufaisha.
  “Dowans ni sehemu ya hoja, mambo mengi yanapasawa kufanyiwa kazi, huu ndiyo mwanzo wa kujua mambo mengi,” alisema.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Tayari wabunge hao kwa nyakati tofauti kila mmoja ameshawasilisha kwenye ofisi ya Bunge taarifa ya kutaka kuwasilisha hoja yake binafsi katika mkutano wa Bunge unaoanza keshokutwa.
    
  Taarifa kutoka ndani ya CCM na ofisi ya Bunge zinasema chama hicho kwa kumtumia spika wa bungeAnne Makinda ambaye ni mwananchama wake mtiifukimepanga kuizuia hoja ya Mnyika kuhusu katiba kwa kutumia njia kuu mbilimoja ni serikali kuwasilisha bungeni muswada wa sheria ya kuweka mchakato wa katiba na tume ya kuusimami na pili ni kuwatumia wabunge wake wawasilishe hoja ya Katiba kama Mnyika.
    
  “Spika atasema hoja ya Mnyika haiwezi kujadiliwa kwa sababu analotaka kuliwasilisha tayari anaweza kulichangia katika muswada utakaowasilishwa na serikali bungeni kuhusu tume na mchakato wa katiba.
    
  “Piliwatasema kuna wabunge wengine pia waliowasilisha hoja kama yakesasa tumpe yupitumuache yupi….na muda hautoshi kujadili hoja zote na wala kanuni haziruhusu kujadili suala hilo hilo moja kwa hoja nyingi tofauti,” alifafanua kigogo mmoja wa CCM kwa sharti la kutotajwa jina lake.
  Kwa mwananchi wa kawaida anachotaka ni katiba mpya atakayoiandika mwenyewe kupitia Mkutoano Mkuu wa Kikatiba ambao wajumbe wake ni yeye mwenyewe amewachagua kwa kuwapigia kura wale waliojitokeza kuziomba nafasi hizo.........................Wajumbe wa TUME itakayoongoza mchakato huo ni vyema ikapatikana kwa kutoa fursa sawa kwa raia kuomba nafasi hizo baada ya kutangazwa kwenye magazeti na Kamati husika ya Bunge ikawasaili wajumbe husika..............................
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Kuhusu hoja ya Kafulila itakavyozuiwataarifa kutoka ndani ya chama hicho zinasemawatatumia kisingizio cha suala la Dowans kuwa mahakamani ili kuzuia lisijadiliwe bungeni.
    
  "Watasema Bunge haliwezi kujadili suala linaloshughulikiwa na mhimili mwingine wa dola (Mahakama)"alisema mtoa taarifa wetu.
    
  Hata hivyoakizungumza na Tanzania Daima JumapiliKafulilaalisema msingi wa hoja yake ni kutaka kuangalia namna serikali ilivyoshindwa katika kesi hiyo wakati mkataba iliourithi Dowans una utata mkubwa wa kisheria na kwamba suala hilo haliwezi kwa namna yoyote ile kuingilia uhuru wa mahakama.
    
  Alisema kuwa mazingira ya kesi yenyewe yanaonyesha kuwa hujuma zimefanywa katika uendeshaji huo ndiyo maana yeye amejipanga kuwasilisha hoja hiyo ili Bunge lijadili na kujua kwa kina kilichotokea kwenye kesi hiyo.
  Hakuna uhusiano kati ya hoja ya Kafulila na ile iliyopo Mahakamani..................................Mahakamani hoja ni kulipa au la............................wakati ya kafulila ni akina nani hao ambao wamelifikisha taifa kwenye njia panda na wachukuliwe hatua zipi jambo ambalo Mahakama haitajadili................two diametrically opposite issues involving different parties in a different setup....................
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Hoja za Katiba mpya, Dowans zisiminywe

  [​IMG]

  [​IMG] BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaanza vikao vyake kesho kutwa mjini Dodoma, ambapo wabunge watafanya shughuli mbalimbali ikiwamo kujadili hotuba ya rais aliyoitoa Novemba mwaka jana wakati akilizindua Bunge baada ya uchaguzi wa Oktoba 30.
  Wakati wabunge wakikusanyika kesho kutwa katika viwanja hivyo, wabunge wawili kutoka vyama vya upinzani wameonyesha nia ya kupeleka hoja binafsi ya kutaka Bunge litoe mwongozo juu ya mchakato utakaowezesha kupatikana kwa Katiba mpya.
  Hoja nyingine ni ile ya kulitaka Bunge lijadili kushindwa kwa serikali katika mahakama ya kimataifa inayojishughulisha na utatuzi wa migogoro ya kibiashara dhidi ya Kampuni ya Dowans ambayo inapaswa kulipwa sh bilioni 94 na TANESCO.
  Kimsingi hoja hizi mbili zina masilahi makubwa kwa taifa, kwa kuwa kwa muda mrefu Tanzania imekuwa ikikabiliwa na matatizo mbalimbali yanayotokana na upungufu uliomo ndani ya Katiba ambayo pamoja na nchi kuingia katika mfumo wa vyama vingi bado kuna vipengele ni kandamizi.
  Sekta ya umeme nayo kwa muda mrefu imekuwa ikienda kwa mwendo wa kusuasua kwa sababu ya kutokuwapo kwa mikakati madhubuti ya kutatua matatizo yanayojitokeza, hivyo kuifanya nchi kutokuwa na umeme wa uhakika.
  Tunaamini kuwa wabunge watatumia fursa hii ya kukutana kwao kuweka mbele masilahi ya taifa kwa kuruhusu na ikiwezekana kujadili kwa ufasaha hoja hizi badala ya kufuata itikadi za chama.
  Tunasema hivyo kwa kuwa tayari kumeanza kusisika minong'ono kuwa baadhi ya wabunge hasa wa chama tawala ambao wapo wengi wamekuwa wakifanya mizengwe ili hoja hizo zisipate nafasi kwa hofu ya kukiweka mahali pabaya chama chao.
  Hatuamini kama wabunge makini wanaweza kufanya hujuma ya aina hiyo kwa hoja zenye masilahi kwa taifa, hasa katika kutatua matatizo ya muda mrefu yanayolikumba taifa hili.
  Tunawaomba wabunge waweke mbele masilahi ya wananchi ambao kadiri siku zinavyokwenda ndivyo wanavyozidi kuwa maskini kutokana na mgawanyo mbovu wa rasilimali za taifa.
  Sote tunajua umuhimu wa sekta ya umeme kwa taifa kiuchumi, hivyo hakuna sababu kwa wabunge kufanya masihara katika mambo muhimu yanayogusa moja kwa masilahi ya wananchi.
  Kadiri tunavyofanya mzaha katika sakata hili ndivyo tunavyozidisha ugumu wa maisha kwa wananchi.
  Tunaamini kuwa wabunge watatumia fursa hii kujadili hoja zenye lengo la kuitoa nchi yetu hapa tulipo na wala si kujadili zaidi siasa na porojo zenye kumuumiza mwananchi.
   
 5. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2011
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nguvu ya umma itawafuata hukuhuku dodoma kwa kweli hali sio nzuri kabisa kwa wananchi
   
 6. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  pia wajadili ongezeko la gharama za umeme na fuel! twafa!
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  JK: Tutazingatia ushauri wa wabunge kuhusu Dowans

  Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 5th February 2011 @ 23:57


  HATIMAYE Rais Jakaya Kikwete amelitolea ufafanuzi suala la Kampuni ya kufua umeme ya Dowans akisema Serikali itazingatia ushauri wa Kamati ya Wabunge wa CCM iliyokaa hivi karibuni.

  Akihutubia wanachama wa CCM wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 34 ya chama hicho zilizofanyika kitaifa Dodoma jana, Rais Kikwete alisema Serikali yake iko makini kutafuta ufumbuzi wa tatizo la Dowans ambao hautaleta madhara makubwa kwa wananchi.

  Akitoa historia juu ya kilichosababisha nchi kutafuta ufumbuzi wa haraka, Rais Kikwete alisema alipoingia madarakani, miongoni mwa changamoto zilizojitokeza, ni ukame uliosababisha kukauka kwa vyanzo vya maji na hatimaye nchi kuingia gizani.

  Alisema mavuno ya chakula yalikuwa mabaya na kukawa na njaa kali ambapo watu 3,776,000 walilazimika kuhudumiwa na Serikali. Aidha, mito mikubwa na midogo ikapungukiwa sana maji na mingine kukauka kabisa.

  Alisema jitihada zilifanyika na moja ya hatua ilikuwa ni kutafuta kampuni ambayo ingeweza kupata suluhisho la haraka na ndipo mchakato ulipofanyika wa kumpata mzabuni ambaye angefanya kazi hiyo.

  "Mimi nilitilia shaka nilipoambiwa kwamba Kampuni ya Richmond iko tayari, lakini wanataka tuwalipe kwanza dola milioni 10.

  Niliwambia walete hiyo mitambo, kisha sisi tuwalipe. Shaka yangu ilikuwa ni ya kweli, kwani badala ya kuleta mitambo, wakauza mkataba huo kwa Dowans," alisema Rais Kikwete na kuongeza:

  "Hawa Dowans ni kweli walileta mitambo na umeme ukapatikana, lakini suala likaja, je hawa walioingia mikataba nao si ilikuwa kampuni ya mfukoni?

  Ndipo Bunge likalazimika kuunda tume na ikagundulika kwamba Richmond kweli ni kampuni ya mfukoni".

  Hata hivyo, Rais Kikwete alisema badala ya watu kutafuta jinsi ya kutatua tatizo lililopo mbele yao, wakawa wanamhusisha kuhusika na Kampuni hiyo ya Dowans.

  "Yapo maneno mengi eti mbona Rais yuko kimya sana, hatujamsikia kusema chochote? Niseme nini zaidi na hao wote wameshasema kwa niaba yangu? Wapo wanaosema niko kimya kwa sababu nahusika na Downs, na eti ndiye mwenyewe hasa.

  Wapo wanaosema niko kimya au nashindwa kuchukua hatua, kwa sababu marafiki zangu wamehusika, nawalinda, " alisema Rais Kikwete na kuongeza:

  "Jambo ninalotaka kulizungumzia sasa sikutaka kulizungumza, kwa sababu Waziri Mkuu alishalifafanua baada ya semina ya wabunge wa CCM na hata John Chiligati, Katibu wa Siasa na Uenezi Taifa alishalizungumzia.

  Sikuona umuhimu wa kufanya hivyo kwa sababu viongozi wenzangu hao wameelezea kwa ufasaha uamuzi wa Kamati Kuu na ule wa kikao cha pamoja cha wabunge wa CCM".

  Akiweka msimamo juu ya kutohusika kwake na Dowans, Rais Kikwete alisema: "Napenda kuwahakikishia wana-CCM na wananchi wenzangu, kuwa sina uhusiano wowote wa kimaslahi kwa namna yoyote ile na Kampuni ya Dowans.

  Sina hisa zozote wala manufaa yoyote yale. Pia sina ajizi wala kigugumizi cha kuchukua hatua kwa sababu ya rafiki yangu au hata kama angekuwa ndugu yangu kahusika".

  Alisema uamuzi uliofanywa na Kamati Kuu na Kamati ya Chama ya Wabunge wa CCM ulifanywa chini ya uongozi wake na hivyo; " ni uthibitisho tosha wa ukweli huo.

  Waliokuwepo kwenye vikao hivyo wanajua ukweli wa haya ninayosema. Ningekuwa na maslahi au hofu tusingefanya uamuzi ule."

  Alisema anachobaini katika sakata hili ni yeye kukubaliana na ombi la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa wakati huo ambalo liliiomba Serikali igharamie ukodishaji wa mitambo kutoka nje, jambo ambalo alisema lilikubaliwa kulingana na hali halisi.

  Aliongeza: "Ili kukabiliana na tatizo hilo, ushauri ulitolewa na Tanesco nasi tukaukubali kuwa wakodishe mitambo ya kuzalisha umeme kutoka nje.

  Serikali tukaombwa kugharamia ukodishaji huo. Taratibu za kisheria zikafanywa, tenda zikatangazwa na washindi wakapatikana Aggreco, Richmond na Alstom.

  Kampuni za Aggreco na Alstom zilileta mitambo yao kwa wakati, lakini Richmond ikawa
  inasuasua.

  "Wakati huo huo maneno mengi yakawa yanazagaa kuhusu Richmond kutostahili kupewa tenda kwa sababu ya kutokuwa na uwezo na kutokuwa hai.

  "Ikadaiwa kuwa wamepewa tenda kwa sababu ya kubebwa na baadhi ya viongozi serikalini. Maneno hayo yalifanya Wizara ya Fedha isite kutoa fedha za kuanzia kwa kampuni hiyo.

  "Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati ule alipokuja kuniomba niingilie kati ili kampuni hiyo ilipwe malipo ya awali nikakataa na kumwambia Waziri aachane nao kwani kampuni hiyo ni ya shaka".

  Rais Kikwete alisema hata hivyo Richmond haikulipwa malipo hayo kwa kushindwa kutimiza mkataba, ingawa alisema maneno yalizidi kadri makali ya kukosa umeme yalivyoendelea kuuma.

  Aliongeza kwamba baada ya hapo Kampuni ya Richmond ikauza mkataba wake kwa Dowans ambayo ilileta mitambo na uzalishaji umeme ukafanyika na kupunguza kabisa makali ya mgawo.

   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Feb 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  PHP:
  "Mimi nilitilia shaka nilipoambiwa kwamba Kampuni ya Richmond iko tayari, lakini wanataka tuwalipe kwanza dola milioni 10. 

  Niliwambia walete hiyo mitambo, kisha sisi tuwalipe. Shaka yangu ilikuwa ni ya kweli, kwani badala ya kuleta mitambo, wakauza mkataba huo kwa Dowans," 
  alisema Rais Kikwete na kuongeza

  "Hawa Dowans ni kweli walileta mitambo na umeme ukapatikana, lakini suala likaja, je hawa walioingia mikataba nao si ilikuwa kampuni ya mfukoni? 

  Ndipo Bunge likalazimika kuunda tume na ikagundulika kwamba Richmond kweli ni kampuni ya mfukoni"


  Hata hivyoRais Kikwete alisema badala ya watu kutafuta jinsi ya kutatua tatizo lililopo mbele yaowakawa wanamhusisha kuhusika na Kampuni hiyo ya Dowans

  "Yapo maneno mengi eti mbona Rais yuko kimya sana, hatujamsikia kusema chochote? Niseme nini zaidi na hao wote wameshasema kwa niaba yangu? Wapo wanaosema niko kimya kwa sababu nahusika na Downs, na eti ndiye mwenyewe hasa. 

  Wapo wanaosema niko kimya au nashindwa kuchukua hatua, kwa sababu marafiki zangu wamehusika, nawalinda, " 
  alisema Rais Kikwete na kuongeza
  Swali ambalo JK kamwe hawezi kulijibu ni...............................why now?

  mbona likaa kimya wakati Richmond inakabidhi shughuli zake kwa DOWANS.......................anapaswa kutueleza mchakato mzima wa ajira ya Dr. Idrissa Rashidi pale Tanesco na yeye binafsi alishiriki vipi?
   
 9. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nadhani spika wetu anahitaji kuazima busara za spika wa kenya, keneth marende aliyeruhusu hoja ilikuwa mahakamani kujadiliwa na wabunge on the ground that "the House will not give up jurisdiction easily because some litigation has commenced on the matter to. To hold otherwise would be to invite every person apprehensive on the action the government might make on any matter to head to court and derail the house"
   
 10. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #10
  Feb 6, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Za mwizi arobaini
   
Loading...