CCM kutumia chupa za chai na hotpot kuiba kura Arumeru Mashariki tarehe 1/4

Mwakiluma

Senior Member
Jan 23, 2012
120
47
Ndugu wa Jf....
Sasa ni dhahiri kuwa dk. Slaa ametibua mbinu zote za kuiba kura zilizokuwa zikipangwa na CCM kule arumeru mashariki.Uzoefu unaonyesha kuwa kuna njia nyingi ambazo ccm wamekuwa wakizitumia katika kufanya wizi wa kura. Moja ya njia hizo ni kutumia chupa za chai na hotpot za vyakula.

Katika njia hizi hotpot na chupa za chai hupelekwa katika vyumba vya kuhesabia kura katika nyakati tofauti na watu huamini kuwa vile ni vyakula na chai wanavyopelewa wahesabuji wa kura.

Katika mbinu mawakala wengi hawaamini kuwa mle ndani ya hizo chupa na hotpot mnaweza kuwekwa karatasi zinazokuwa tayari zilishapigwa kwa chama cha CCM.

Hii mbinu ilitumika maeneo mengi katika uchaguzi wa 2010 kama vile jimbo la babati.


Mytake. CDM KUWENI MAKINI SANA NA MBINU HII.
 
Dr slaa kichwa hapo inabidi wasiingie navyo kwenye chumba cha kuhesabia kura,mtu akitaka kula anaenda kwenye chumba maalumu kwa ajili ya kula na sio kwenye chumba cha kura!
 
mahotpot na machupayao ya chai yakaguliwe, hata ikibidi nguo za ndani zipigwe pekshi.
 
mafisadi wameishiwa mbinu.

na hakika hawa labda wakimbie na mabox haki ya mungu!
 
Kama hawa magamba wangekuwa wabunifu namna hii katika kupambana na umaskini tungekuwa kama Japan. Inahitaji ubunifu wa hali ya juu sana kufikiria kuiba kura kwa kutumia HOTPOT, sisiem ni noma
 
Magwanda yanapoanza kubana huwa kero. Mbinu zote za kuiba mnazijua na mmedhibiti, kwa hiyo atapotawazwa Sioi, msilalame.
 
Ndugu wa Jf....
Sasa ni dhahiri kuwa dk. Slaa ametibua mbinu zote za kuiba kura zilizokuwa zikipangwa na CCM kule arumeru mashariki.Uzoefu unaonyesha kuwa kuna njia nyingi ambazo ccm wamekuwa wakizitumia katika kufanya wizi wa kura. Moja ya njia hizo ni kutumia chupa za chai na hotpot za vyakula. Katika njia hizi hotpot na chupa za chai hupelekwa katika vyumba vya kuhesabia kura katika nyakati tofauti na watu huamini kuwa vile ni vyakula na chai wanavyopelewa wahesabuji wa kura...katika mbinu mawakala wengi hawaamini kuwa mle ndani ya hizo chupa na hotpot mnaweza kuwekwa karatasi zinazokuwa tayari zilishapigwa kwa chama cha CCM... Hii mbinu ilitumika maeneo mengi katika uchaguzi wa 2010 kama vile jimbo la babati.


Mytake. CDM KUWENI MAKINI SANA NA MBINU HII.

Duh!haya yote ya nini jamani kama watawaliwa wamekukata kwa sanduku la kura huu uchakachuaji utakufikisha wapi?unaiba ili umuongeze nani?kwa kifupi utakuwa mbunge wa hotpot au chupa ya chai na siyo wananchi
 
Magwanda yanapoanza kubana huwa kero. Mbinu zote za kuiba mnazijua na mmedhibiti, kwa hiyo atapotawazwa Sioi, msilalame.

Kulalamika ni haki ya msingi pale ambapo haki haijatendeka.wezi kila siku wanakuja na mbinu mpya.
 
Yaani kweli Magamba ni professional kwa wizi!!!! Halafu kibaya zaidi ni wao wenyewe wanaenda kunueleza habari zote Dr. Slaa.

WanaJF msifikiri Dr. Slaa anaota ni hao hao CCM ndiyo wanenda kusema ukweli kwa kuwa wamechoshwa na uovu uliotamalaki chamani.
 
1 Kupiga kura zidi ya mara moja: Bandika wino usiotoka (Ukitoka je)
2 Gawa shahada kwa wasio husika: Mawakala kuwagundua kwa sura
3 Kugawa karatasi zaidi ya moja kwa mpiga kura: Wakala kuwa makini
4 Kutumbukiza kura katika box kabla ya kufunga
Kufunga kituo: Wakala akihongwa anakubali. (Sijui hapa watafanya nini)
5 Mpiga kura anaweza kuingia na karatasi nyingi za kura alizopigia nyumbani. Hii hutumika sana kama masanduku ya kura yakiwekwa kwenye vizimba. (Tunazibiti vipi)
5 Tuwe makini na hizi Ambulance zinazokpita pita kila mara haswa wakati huu wa Uchaguzi (Tafanyeje sasa)

6 Kutumia nguvu kuwatisha mawakala, kuchakachua (Nini kifanyike), hii inaweza ikawa katika vituo vya kupigia kura, wakati wa kusafirisha masanduku na wakati wa majumuisho. (Hapa naona ipo kazi, labda mawakala wa nguvu wasioogopa MG)
7 Kuwahi sana kupiga kura na kuwaacha mawakala peke yao katika vituo (hapa inakuwaje?)
8 Segerea style, kukimbia na masanduku ya kura. Hapa panahitajika escot ya nguvu sana, bila hivyo sijui. Bodaboda wanaweza hii kazi.
9 Je Magari ya Jeshi yanaweza kutumika, Basi tume ipate ma MP ili kushirikiana na wananchi wenye wasiwasi.
10
kuanzisha vurugu kituo cha kupigia kura hasa mida ya jioni. (Kuabakia katia vituo m 103 hadi kura zinapoondoka)
11 Karatasi ya kupigia kura huchanwa kwenye kitabu: Kwa maana hiyo idadi ya kura zinazopigwa ni lazima iwiane kwa idadi na serial namba za karatasi, itakayokosekana kwenye kishina cha kitabu si kura halali. mawakala wahesabu idadi ya karatasi zilizotumika, wawianishe kwenye vishina wakati wa kuhesabu.
12 kutumia chupa za chai na hotpot za vyakula.
(Zinapoletwa kwa mawakala zisachiwe)
 
Kununua shahada za wapiga kura,kuficha mabox ya kura kwenye ceiling board za vituo vya kupigia kura,kura kutoka vituo hewa,na mwisho kbs ni mbinu ya 'tangaza mshindi ni CCM asiyeridhika aende mahakamani'.
 
Kununua shahada za wapiga kura,kuficha mabox ya kura kwenye ceiling board za vituo vya kupigia kura,kura kutoka vituo hewa,na mwisho kbs ni mbinu ya 'tangaza mshindi ni CCM asiyeridhika aende mahakamani'.


110% CCM wamepanga kutumia hotpot na chupa za chai katika kuiba kura. Vifaa hivyo vinategemewa kuingia Arumeru leo usiku na watu watakao fanya kazi hiyo ni watu ambao si wenyeji wa Arumeru.
 
Back
Top Bottom