Movement 4 Change na Magufuli 4 Change ulivyotibua Ilani ya CCM, mnufaika mwanachi

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Wana JF,

Mabadiliko ya M4C ya pande zote ndiyo yaliibua mvumo wa vyama vyote kila chama kikipambana kuwavuta wapiga kura.

Kama mnakumbuka upande wa CCM ulitaka kuzidiwa nguvu mbali na kutumia viongozi wote waliowahi kushika nafasi za juu, Rais mstaafu JK alikuwa akipigana chini juu chama kisimfie mikononi.

Watu waliichukia sana CCM kutuingiza kwenye umaskini uliotukuka ndipo Rais aliyepo ikabidi abadilishe mbinu, hii ilikuwa ni kuchota sehemu kubwa ya ahadi zilizokiwa zinahubiliwa wapinzani. Kama vile elimu bure jambo ambalo CCM iliipinga sana kuwa haiwezekani.

Hapo CCM ilikuputisha wazee wote ikajipanga upya na kutengeneza M4C Magufuri 4Change ili kuwacjanganya watu waliokuwa wametekwa na Chadema. Kwa hili walifanikiwa kwani waliweza kuuteka mji wa mwanza na Shinyanga na kujizolea kura nyingi zilizomwezesha Magufuli kushinda. Jambo ambalo CCM ilidandia na linaiumiza ni ahadi ya elimu bure, matibabu bure. CCM haikujiandaa kabisa na sera hizi.

Baada ya kufanikiwa kuanza kutekeleza, Magufuri ilibidi awe mkali sana kubana matumizi na kuziba njia zote za wizi, hii ilifanya CCM ianze kumeguka, akawepo kundi la mafisadi na kundi la wazalendo.

Kundi la mafisadi lilijifanya ndilo lenye chama, kundi la wazalendo hili nalo likaanza kujizatiti kuwa upande wa wanyonge ambao walimwamini Magufuli pekee wala sio chama CCM. Nguvu ya Magufuli ilikuwa ni kuakikisha katika teuzi zake aweke watu anaowamudu wasio na chembe ya uchama hata mafisadi.

Yeye anaamini katika kazi, Yale mafisadi yanaamini katika upigaji na dili. Nguvu hizi za M4C hazikuishia hapa, hata CC na NEC ya CCM ilitikiswa kwa kupata ingizo jipya.

Maendeleo haya yameleta wasiwasi mkubwa kwamba safari hii huenda wabunge waliozoea dili hawawezi kurudi kwani kipindi hiki ubunge hauna dili. Wale waliozoea kutoa mlungula hawana uwezo tena kwani hata wakikopa hawawezi rudisha.
 
Nilipoona neno "wapiga kula" badala ya "wapiga kura" nimeahirisha kusoma hili gazeti lako.
Kila lakheri
 
Hivi M4C si Slogani inayomilikiwa na Chadema?

Magu alivyosema M4C ni Magufuli 4 Change hatua gani zilichukuliwa khs Mambo ya Trademark/Copyright?

NI YEYEEEEEE
 
Back
Top Bottom