CCM kumtenga Makonda inajiharibia

Sabaya alivuka mstari. Huyu Makonda uhuni wake wote ni kwaajili ya chama. Kunyanyasa watu. Kumsingizia Lowassa mtoto nk nk. Watu wataacha kukifanyia chama mambo kama hayo.
 
Makonda atumie kipindi hiki cha Kwaresma kwenda kuomba msamaha kwa familia za Mzee Warioba, Kikwete, na ya Philip Mpango. Kisha atoke hadharani awaombe msamaha Watanzania aliyowahi kuwaumiza kwa namna moja ama nyingine kwa maamuzi aliyowahi kuyafanya ili apate kumfurahisha aliyekuwa bosi wake.

Watu maarufu wanaotajwa kwa uchache ni Tundu Lissu,MO mfadhili mkuu wa mikia, Yusuph Manji, Mbowe, Ridhiwani kama yeye binafsi, familia za marehemu Kabwe, Ben Saanane, Gamba na ya Ruge, na wengine wengi ambao waliamua kunyuti kuhusu dhuluma walizofanyiwa.
 
Samahani lakini lazima niseme maoni haya

Makonda si chochote wala lolote nchi hii.

Akipotea kesho hakuna mtu atajua alikuwepo.
 
Wacha Makonda afunzwe adabu, mwache.
 
Unaongelea CCM kama iko moja wakati imegawanyika makundi.
 
Uhuni huo ndiyo umefanya wabunge wengi wa CCM wawepo bungeni. Ndiyo uliowapa madiwani na kushika local goverment nchi nzima. Kifupi inaishi kwa mtindo hui. Wakianza kunyosheana vidole wataanguka.
 
Uhuni huo ndiyo umefanya wabunge wengi wa CCM wawepo bungeni. Ndiyo uliowapa madiwani na kushika local goverment nchi nzima. Kifupi inaishi kwa mtindo hui. Wakianza kunyosheana vidole wataanguka.
Kabisa ujinga walioufanya kuanzia serikali za mitaa 2019 ni aibu tu.

Mimi naamimi washamba walishika madaraka so kila kitu kikaenda kishamba tu.
 
Acheni kukumbatia wapuuzi kama huyu.
 
Walimtenga Sabaya na maisha yanaendelea.
 
Yamekuwa hayo! Lakini mbona mlifurahi na kumzawadia ukuu wa wilaya baada ya kumpiga kofi Jaji Warioba? Ccm ni kokoro kweli!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…