CCM: Kumpinga Mwenyekiti ni uhaini

CCM: Kumpinga Mwenyekiti ni uhaini

Mkusa

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2010
Posts
548
Reaction score
209
Wana Bodi,
Kila Mara nimekuwa nikijuliza hivi CCM suala la Demokrasia wanamhubiria nani ilhal wao wenyewe hata Maana ya hilo Neno hawaijui na wala hawajui kuishi katika hilo.
Kwenye maandalizi ya Uchaguzi wao wa Mwenyekiti kwanza sijasikia ni lini fomu za kuwania nafasi hiyo zilitangazwa kuanza kugawiwa, sijasikia hata sehemu inayomnukuu Mkwe.re kwenda kuchukua form hizo wala kujinadi na kuomba kupewa Nafasi hiyo
Mbaya zaid kuna vijana eti wameapa kumlinda JK kwa Gharama yeyote ili awe mwenyekiti.
Ni nini kutumia Nguvu Nyingi kumlinda mtu ambaye wanadhani anakubalika kwa madai yao??????

From Mwananchi

Kwa upande wao wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kupitia kundi la vijana, walisema kuwa watamlinda kwa gharama yoyote Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete pamoja na kuhakikisha kuwa anapata kura zote za ‘ndiyo.' Mbali na hilo, vijana hao walisema kuwa watafanya kila njia kumsaka mtu aliyetengeneza vipeperushi hivyo vinavyosambazwa dhidi ya mwenyekiti wao, Rais Jakaya Kikwete.
Wajumbe hao saba kati ya kumi waliitisha mkutano na waandishi wa habari katika Ofisi za CCM Mkoa wa Dodoma na kutoa tamko hilo, huku wakieleza kuwa hawatalala hadi watakapoona mwenyekiti wao akiibuka na ushindi wa kishindo.

"Sisi ndiyo jeshi la chama. Itakuwa ni aibu kama mwenyekiti wetu atakuwa akidhalilishwa kwa kupata kura chache, ilhali nasi tupo. Lazima kuwaaibisha watu wa aina hiyo na kuwasaka popote walipo. Tunaomba vijana wenzetu watuamini kuwa tuko Dodoma kufanya kazi hiyo," alisema Jery Silaa kwa niaba ya wenzake.

Important
Kwenye Uchaguzi wa CDM, Tukisikia Mwana CCM yeyote ana benua mdomo Kike Kike na kutia Neno Lolote, Naapa tuta Zaa NAE
 
Kwa vile mkt wa ccm ndiye rais wa tz kumpinga ni uhaini, wala huhitaji kuomba busara kutoka kwa Mungu kulijua hilo.
 
Democratic na Republican vya Marekani lakini kwa waafrika wagaganga njaaa baaaaaaaaaaaaado sana
Huu ndiyo ukweli ndugu yangu kwetu sisi waafrika ambao siasa ni njia ya kufanikiwa kimaisha hiyo hali ya kuchagua Mwenyekiti wa chama cha siasa kidemokrasia bado sana, ingawa kila mmoja wetu huona ni "demokrasia" pale yule anayemuunga Mkono "anapochaguliwa" kuwa Mwenyekiti.
 
Naam wewe wasema! mkt ambaye ndiye rais wa serikali ya jmt. Hivi unanielewa lakini?
Naruida tena kusema, WANAMPINGA MWENYEKITI WAO MAGAMBA NA SIO RAIS, Haijalishi kama huyo MWENYEKIT NI RAIS PIA, Acha Ubweg.e
 
Back
Top Bottom