William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,466
Unataka kusema sijawahi kutoa mawazo ya kuwa solution za kuleta maendeleo Tanzania au kuboresha mfumo wa siasa?
Naomba nikukumbushe kwanza kwa kukuomba usome Marshal Plan ya Mchungaji na hasa kipengele cha Uongozi
'Marshall Plan' - Restoration and Recovery Plan for Tanzania
Kisha soma Dynamic Productivity Dynamic Productivity; Tija na Maarifa
Endelea na Why Vita vya Ufisadi will not win election Why "Vita vya Ufisadi" failed and will never win election..
KUna Money Matters Money Matters: Maendeleo, Ubunifu, Maadili na Kujitegemea
Pia kuna nyingine tatu za Focus 2010, Chadema must reform na Azimio Jipya, sizioni tena naona mods wamechanganya hoja hivyo sijapata linki zake.
NInachojaribu kuonyesha hapa ni kuwa nimekuwa nikimpigia kelele Kikwete na kumtupia lawama kwa ukali, lakini hata kama ni Amiri Jeshi MKuu, yeye si pekee katika uongozi na CCM ilipaswa kuwa makini kumuongoza hata Mkapa, Mwinyi na Nyerere. Katika hizo thread nilizokuonyesha hapo juu, solution zake si kwa ajili ya CCM, bali ni kwa ajili ya Taifa zima. Solution kwa CCM kujisafisha ni kwa watu kuacha kuoneana haya na woga na wafanye kweli ama wafukuze au wajiondoe.
Exactly ndio ninachosema nilitegemea uweke solutions maana ninaamini kwamba unao huo uwezo, sasa shukrani kwa link zako lakini ungeziwakilisha kwenye hii mada ya Mwanakijiji, ningeelewa.
- Hapa ndio yale yale, hakuna solution ila lawama tupu kwa wengine wa CCM, mkuu huko kwenye tumefikaje hapa tulipo Mwanakijiji ameshapitia kabla ya kutoa hii mada, tumetokea kwa Mwalimu, sasa anatafuta solution, kama uliwahi kuzitoa huko nyuma ilikuwa kwenye mijadala mingine lakini sio huu, lawama sio solution kwa sababu matatizo yako sio ya mwingine.
- CCM wajisafishe wasijisafishe, sio tatizo letu wananchi hapa kwenye hii mada tatizo letu ni solution kutoka kwenye shimo tulilomo tayari, kuwalaumu viongozi watano au sita wa CCM hakutatui tatizo, kwa sababu CCM they are not doing it, so what tusubiri mpaka watakapoamua kufanya kama unavyosema itakua ni lini hiyo?
I mean kama ni ukali kila mtu hapa anaweza kuutoa, lakini where is a solution kwa sisi wananchi na taifa lililoko shimoni??
FMES,
Bila kuonyesha ubovu wa CCM, kamwe Watanzania walio wengi hawataweza kuoanisha na kuelewa kiini cha matatizo yao. Unakumbuka mapokezi waliopewa kina Chenge na Lowassa? ambayo yaliandaliwa na Chama? Je mapambio mengine mengiya kukisifu chama huku kinashindwa kufanya kazi zake kwa umakini kwa nini basi tusiwapashe habari Watanzania wajue udhaifu wa Chama walichokiamini ili waweze kuamka kama unavyotaka waamke na kuwajibika? Wananchi wengi wameridhika na CCM, wameridhika kutokana na mazoea na hisia kuwa kila kitu ni heri ndani ya CCM.
Lakini ukweli ni kuwa Serikali ya CCM imeshindwa kazi. Leo Chiligati anasema CCM isihusishwe na wizi wa pesa za EPA. Hilo ni sawa, kwa kuwa tunaweza tusipate ushahidi kamili wa kunufaika kwa CCM kutokana na wizi huo wa EPA, Meremeta, Kagoda, IPTL, Richmond, Rada na tuhuma nyingine nyingi za Uhujumu na Ufisadi. Lakini swali linabakia, ni nani alikuwa na majukumu na mamlaka ya kuongoza nchi na kudhibiti rasilimali na uchumi? Jibu ni Serikali ya CCM..
Hivyo kukwepa kuwajibika kwa kuwa eti hatujawakamata CCM kama Paulo Usijekuchza na sisi, si tija wala halina nguvu. Madhali uhujumu huu ulifanyika kwa zaidi ya miaka 6, ni wazi basi kuwa CCM na Serikali yake havina uwezo wa kuongoza na kulinda rasilimali za nchi, mbaya zaidi, haina uwezo wa kudhibiti, kukagua na kuhakiki shughuli za uzalishaji mali na biashara.
Sasa kwa hili, kwa nini tusiinyoshee CCM vidole na kuilamu ili wale ambao wameishi wakiridhika na kufikiri CCM ni safi waone udhaifu wa CCM na hivyo kujirekebisha na kuanza kudai uwajibikaji?
Solution yangu kwa hili swali ni hivi: Wale wanaojiita ni CCM Mageuzi wajitoe ndani ya hiki chama, maana kimeoza na ni kazi kusafishika. KIbaya zaidi ni hizi njama ambazo tumekuwa tukizisikia kwa zaidi ya miezi 10 ya kuwashikisha adabu wale CCM mageuzi kwa kuhakikisha hawapati nafasi za uongozi wala uwakilishi 2010. Kwa mtaji huo, viapo vya hawa CCM mageuzi bado ni matatani maana kama wao wanajivutavuta kuwaondoa wale wachache, basi wao ndio watakaoondolewa.
Solution ni moja, get rid of CCM!
__________________
FMES,
Naona tunacheza Sega Dance kama si Segere Matata!
Kama Mkapa na kakundi kake ka mafisadi ndio wanaokichafulia jina Chama, kwa nini inakuwa ni vigumu kuwatoa?
Je Mkapa na kundi lake ndio wanaoshikilia bajeti na mipango ya maendeleo ya Taifa?[/QUOTE]
- Najua kuwa ndio waliochukua hela za EPA, na ndio wenye nguvu ndani ya serikali yetu leo, si nimeona mahali humu kwamba Lowassa was the best, au si wote wamoja hao, au?
- Wanatolewa na nani? Mkapa ambaye Mwalimu baba wa taifa mwenye nguvu za kulaani na kubariki, alisema ni malaika na ndiye aliyekwua mwenye CCM, sasa Mkapa anatolewa na nani huko CCM?
- Najua kuwa ndio waliochukua hela za EPA, na ndio wenye nguvu ndani ya serikali yetu leo, si nimeona mahali humu kwamba Lowassa was the best, au si wote wamoja hao, au?
Then tunarudi kwenye ile hoja yangu kuwa CCM haiwezi kujisafisha na hata CCM mageuzi hawawezi kukigeuza chama ila nji amoja, wajitoe CCM.
Kama Mkapa na wafuasi wake wanaogopewa eti mteule wa Nyerere au visingizio vingine huku inajulikana wazi kuwa alishindwa kazi na anaongoa genge la wahujumu, basi wale wote wanaobakia kudai CCM ni mama yao au wao ni CCM mpaka kufa wana walakini na hivyo kamwe tusitegemee CCM ituletee mabadiliko au kuruhusu kufanyika mabadiliko yeyote kwa kuwa ndani ya chama kuna udhaifu mkubwa!
Mkuu wangu ni rahisi kusema lakini imani ya mtu ktk dini haitokani na mchungaji hata kidogo.. Mchungaji anaweza kukukuta wewe tayari umekwisha kuwa na imani ya dini hiyo kutokana na mafundisho ya Kitabu - Yaani Biblia ama Msahafu, kwani Mungu ni neno na neno hilo ndilo lililoandikwa ktk kitabu sio Mchungaji wala Sheikh..ndio maana siku zote hata kwenye ubishi wa dini huwa sipendi mtu aanapotumia mapungufu ya kiongozi fulani wa dini kuwachamba waumini wote...On this mkuu nipo na FMES..Bob Mkandara,
Mtu anapojirudi na kujisahihisha na kuanza kufuata njia iliyo bora na njema, ni rahisi sana kukubalika. Hata Mchungaji, Padiri au mhubiri kama amefanya makosa na waumini tukayaona, naye akaja ungama kwetu na kwa nadhiri ya kweli akajisahihisha na kutenda yale yaliyomema, atapokelewa na kupewa nafasi ya mara ya pili.
Inapokuwa Mchungaji huyu, anafumbia macho maovu ya watu wake au yake mwenyewe na kukataa katu katu kuwa mnyenyekevu na kujisahihisha hata kuomba toba si kwa Mungu pekee bali hata kwa waumini na wafuasi wake, basi ni ama Mchungaji huyu aondolewe madarakani kwa kufukuzwa, au kupigiwa kura ya kutokuwa imani au hatari kubwa zaidi kama Mchungaji huyu ana mizizi ambayo haikatiki, ni waumini kumuachia hilo kanisa lake mwenyewe.
Sasa CCM kama ni Kanisa au Msikiti, lina viongozi, wawe Wachungaji, Mashekhe, Wainjilisti, Wahubiri, Mapadiri,Imamu au Masharifu. Wanaposhindwa kuliongoza Kanisa au Msikiti, inawapasa waachie ngazi ili wengine wenye uwezo na wenye kuaminiwana waumini, waongoze chombo hiki.
Lakini kama CCM, tuna makanisa na misikiti ambayo viongozi wake wamekwaza roho za waumini kwa madhambi ya ajabu ajabu, iwe ni wizi, uzembe, uzinzi, uasherati, ulawiti, dhuluma, unafiki, fitina au kukosa mwamko wa kiroho kuongoza makanisa na misikiti hii na hivyo kurutubisha imani za waumini wa masikiti na misikiti hii.
Jamani naomba tuwe realistic kidogo na tuache blah blah ambazo haziwezi kutufikisha popote. Ukweli ni kuwa hivi sasa tunayo serikali ya kiimla inayoendeshwa kwa mtindo wa udikteta wa chama.
Mkuu nakubaliana na wewe 100% na ndio sababu tupo hapa JF.. Hata FMES amekuwa mstari wa mbele kuelezea mabaya ya viongozi walioshika na watakaoshika madaraka..Tatizo kubwa la Tanzania ni Viongozi wabovu...Jamani naomba tuwe realistic kidogo na tuache blah blah ambazo haziwezi kutufikisha popote. Ukweli ni kuwa hivi sasa tunayo serikali ya kiimla inayoendeshwa kwa mtindo wa udikteta wa chama. Chini ya mfumo kama huu ukweli ni kuwa mabadiliko hayawezekani bila "blessing" ya hicho chama labda yatokee mapinduzi. Mapinduzi yanawezekana tu wananchi kwa wingi wao wanapoikataa serikali na kuichukia - na wataichukia tu watakapoweza kung'amua uozo ulio ndani yake.
FMES, Mkandara, Mag3, Mwanakijiji na wachangiaji wengine,
Nawaeleweni vizuri sana, ila kinachonitatiza ni kule kujivutavuta, kusubiri mtondogoo tuanze kufanya kazi. Waswahili walisema cheleachelea utakuta mtoto si wako, sisi nasi tumeridhika na kasi hii ya konokono kama si kinyonga, ya kuburuza miguu badala ya kuchangamka na kuwa wepesi wa maamuzi.
Leo hii, tunaanza kuwaonea huruma na kudai tuwape nafasi au eti ndivyo tulivyo. Kama ni hivyo na ndivyo tunavyofikiri na kufanya mambo, tutegemee lini kupata mabadiliko?
Quote: GT
yaani hiki ni kchekesho sana yaani unabadili jina kisha unajipongeza mwenyewe!
ama kweli ukistaajabu ya Musa utashangaa ya Fir'aun
Quote: ???????
FMES nitajie jina la pili ninalotumia hapa JF ni lipi? uje kule uliposhadadia, usikimbie.
Haya mfungie na GT sasa tuone ubabe wako, bwa! ha! ha! ha! ha! halafu nifungie na mimi pia!
mkuu GT hebu shika simu niko hewani, this is lovely!