CCM kuleta machafuko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM kuleta machafuko

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mtemiwao, Sep 26, 2010.

 1. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa uchu wa madaraka unaonyeshwa na ccm na kauli mbiu yao ya ushindi lazima tutegemee machafuko baada ya 31oct. Mfano ktk jimbo la busanda kata ya rwamgaza hali si shwali maana ccm kwa kutumia kikosi kiitwacho greengud kinatumika kuwawinda wafuasi wa chadema na kuwapiga baada ya kuona upepo wa kushinda udiwani kwa mgombea wa ccm tajiri mwekezaji(c.kadeo)ni finyu ukilinganisha na mgombea kijana maskini wa chadema(ntalima),ccm wamekuwa wakifanya fujo na taarifa zikilipotiwa kituo cha polisi hazishughulikiwi lakini mwanaccm akienda kushitaki hata suala la uongo ocs anaagiza gari toka geita na kuwasomba wanachadema kama waharifu mfano ni tukio la tar 23sept cku ccm walifanya mkutano wa kampeni ukakosa watu matokeo yake vijana walionywesha pombe wakaanza kuwafuata watu wanaosadikika chadema na kuwapiga na kuwaumiza,isingekuwa busara za viongozi wa chadema cku hiyo yangetokea mauaji,chonde chonde ccm tufanye uchaguzi wa amani yeyote atakaeshinda ashinde lakini mwisho tutabakia kuwa watanzania.NAWAKILISHA
   
 2. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ahsante kwa taarifa mkuu. Hayo hata mimi nayategemea sana kutokea maana hawa wenzetu ccm naona hawataki kukalia benchi hata kama kiwango kiko chini. Jamani CCM walioko humu jamvini jaribuni kutumia akili yetu kuepusha haya yote. Wee need democracy, siyo fujo. Najua inauma kukaa benchi lakini viwango vyenu vi vidogo, pesa mbele lakini viwango hakuna. Tunataka timu mpyaa tuonyeshe kazi East Africa nakwingineko.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  inabidi tuombe Mungu, na chadema wanatakiwa wapate ushindi wa tsunami ili jamaa washinde hata kuiba kura zenyewe.
   
 4. Ngaramu

  Ngaramu JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2010
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  CCM Wanayataka machafuko haswa!!!!

  Manake ktk Jimbo la Nyamagana Mwanza (anakogombea Masha), polisi walitembeza mabomu ya machozi kwenye mkutano wa chadema uliofanyika kata ya Buhongwa juzi (nadhani kwa maelekezo ya waziri fulani),

  The next day (jana) mkutano wa chadema (Wenje) ktk eneo la Bulale watu walikua waoga kuhudhulia mpaka elimu ya kutosha kwa vipaza sauti ilipotolewa (kwamba polisi ni wenzetu/wanetu wanaopigika/maskini kama sisi - tusiwaogope) - MKUTANO ULIFANA.

  Hatudanganyiki na vitisho vya mafisadi.

  GO CHADEMA GO!!!!! mpaka kieleweke.
   
 5. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Tunawapeni pole ndugu zetu wa Nyamagana kwa kupigwa mabomu ya machozi na askari wenu. Kuna watu wenye uchu wa kuhodhi madaraka kiasi kwamba watawatoeni hata baadhi yenu roho ili waendelee kutawala. Tafadhali wekeni kumbukumbu sahihi za nani kavunja amani ili mkishajikomboa (Octoba 31) muweze kuwafikisha kwenye mkono wa sheria. Muandike aliyeamuru mpigwe ni nani, na waliopiga ni nani. Wote muwaajibishe baadaye.

  Wananchi wa Nyamagana mlishiriki kumuondoa mkoloni mwaka 1961, na hamkupigwa mabomu. Ila hili la kuondoa ukiritimba wa madaraka wa CCM ni gumu zaidi. Tunawaombea kwa Mungu ili msife moyo na kujikuta mnabaki kwenye makucha ya CCM.
   
 6. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Endapo CHADEMA itashinda wasijaribu kuiba au kudanganya haki ya Umma, itakuwa zaidi ya yale yaliyotokea Kenya. CCM wategee matokeo yoyote na wasijidanganye kwamba USHINDI NI LAZIMA. Mungu ibariki nchi hii tupite salama hadi kuapishwa kwa Rais Mpya.
   
 7. d

  dmalale Member

  #7
  Sep 27, 2010
  Joined: Jun 7, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Hawa jamaa walizoea vya kunyonga! sasa vitawatokea puani! katika akili zao wanafikri kwamba wao wamezaliwa kutawala wengine wote ni watawaliwa hawana akili hata kidogo, wamefikia hatua ya kuandaa kizazi cha kurithiana kiasi kwamba famili ya kikwete yot ni marais, huyo mke wake anajiona naye ni jembe ulaya na huyo mtoto naye anatembea kifua mbele utafikiri serikali yote iko mikononi mwake! wakae wakijua kabisa za mwizi ni arobaini na sasa hivi zishafika 39 bado moja tu wakione cha moto wasifiri watanzania ni wajinga sana wa kudanganywa kama watoto wadogo, na huo ushindi wa kishindo tunasubiri tuone utatokea wapi, na hizo safari za ulaya na marekani zimeishia wapi? kama ungekuwa hivyo siku zote mbona nchi ingekuwa mbali! kutembelea kona zote wao ni mpaka wakati wa uchaguzi tu! mmekwisha!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 8. R

  Ramos JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Vurugu nyingine za CCM zimetokea huku Morogoro pale mgombea ubunge Kwa ticket ya CCMjimbo la Morogoro - Kusini Ndg. Innocent Kalogiris kuleta fujo kaitka mkutani wa kampeni wa CHADEMA na kumpiga kichwa na kumuumiza mgombea udiwani kwa tikeit ya CHADEMA.
   
 9. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Wanajipa jeuri ya bure tu. Mwisho wa siku serikali itakuwa ya Chadema na hao wailofanya fujo watakiona cha moto.
   
 10. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Ukiona hivi jua maji ya shingo yamewafika!!

  Kazi ni moja, kuongeza kasi tu!!
   
Loading...