Chama cha Mapinduzi (CCM) kifutwe kitatuletea machafuko hapa nchini Tanzania

Chama cha Mapinduzi (CCM) kifutwe kitatuletea machafuko hapa nchini Tanzania

Narumu yetu

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
2,448
Reaction score
5,146
Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi anatakiwa kukifutia usajili wa kudumu mara moja chama cha mapinduzi (ccm), ni baada ya kuonyesha dalili za kuvuruga amani ya nchi.

Kuna kila dalili ccm imeanza kutuletea machafuko hapa nchini, kutokana na wingi wa matukio yanayotokea na yaliyotokea huko nyuma bila kuchukuliwa hatua zozote.

Matukio ya kutekwa, kuteswa, na kuuliwa baadhi ya watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa, waandishi wa habari na viongozi wa dini na wengine kubambikiwa kesi zisizo na dhamana, ni matukio ya kinyama yasiyovumiliwa kwa uvunjifu wa sheria na haki za binadamu.

Miongoni mwa waliobambikiziwa kesi ya uhaini ni Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Mh. Tundu Antiphas Lissu, baada ya kukamatwa na jeshi la Polisi na baadhi ya viongozi wa chama hicho, wananchi, wapenzi na wanachama wa chama hicho wakati wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia mwenendo wa kesi inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho, na kuumizwa vibaya na jeshi la Polisi na wengine kuvunjwa baadhi ya viungo vya mwili na kwenda kuwatelekeza baadhi ya maeneo mbalimbali huko nje ya mji, Kisarawe na Mabwepande.

Kwa uchache hayo ndio matukio yaliyotokea hivi karibuni la kusikitisha zaidi na la kuvuka mipaka ni kushambuliwa na kuumizwa vibaya mtumishi wa Mungu Katibu wa baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Padre Charles Kitima.
 
Hakuna haja ya kukifuta ila tunachotaka ni kukivote out kwenye ballot box kwenye uchaguzi HURU na HAKI.
 
Kwa technology ya Leo kila poll station iwe na cctv camera .


Kura zihesabiwe mbele ya camera .


Rais atajiuzulu URAIS siku moja kabla ya kampeni kuanza (NCHI pamoja na uchaguzi /matokeo)vitakuwa chini ya CDF ambaye NI mwenyekiti kamati ya ulinzi na usalama WA Taifa.

Ikiwa na maana kuwa wagombea wote WA kiti cha URAIS watakuwa na sifa sawa hivyo matokeo hayataegemea chama tawala ikiwa na maana kuwa wakati WA kampeni HAKUTAKUWA NA CHAMA TAWALA na kila chama kitajitegemea chenyewe kuanzia ulinzi ,gharama za uchaguzi,ushawishi Kwa wananch nakadhalika .

Mwenyekiti WA tume ya uchaguzi ataapa Kwa jaji mkuu na teuzi zozote kuhiusu tume ya uchaguzi zitafanywa na jaji mkuu akishirikiana na ofisin yake ngazi zote utumishi WA mahakama kuwapata maofisa WA tume .Hii n kuzingatia kile kigezo cha separation of power kinachosema judiciary NI dola huru .


The reform we gear .
 
Back
Top Bottom