CCM kujivua ghamba ni nini maana yake hasa?

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Nijuavyo mimi chama cha siasa chochote kile, kinaundwa na sera zake na wala siyo viongozi. Kwa mantiki hiyo sera za CCM kamazilivyokuwa zimebuniwa na waasisi wa chama hicho zilikuwa zimejikita katika kupambana na dhuluma za aina yote katika jamii. Katika miaka ya karibuni chama hicho kiligeuka na badala ya kuwa katika mstari wa mbele kupambana na dhuluma katika jamii kikawa chenyewe ndicho chanzo cha dhuluma hizo. Hali hiyo ndiyo imesababisha kipoteze mvuto wake kwa wananchi. Hivyo ikiwa maudhui ya kujivua ghamba yanayozungumzwa yanalenga katika kurejesha mvuto kichokuwa nao chama hicho huko nyuma, basi zoezi hilo halipashwi kuishia kwenye kubadilisha sura za viongozi, bali pia linapashwa liusishe na sera ya chama.
 
Nitajibu heading yako: Nyoka akijivua gamba anabaki na urefu uleule, macho yaleyale, kichwa na utumbo vilevile! Na mbaya zaidi, sumu ileile. Tofauti ni ngozi inakuwa na mng'ao mpya zaidi kuliko iliyochoka ya zamani. Lakini, WATCH OUT!! HICHO KIUMBE NI KILEKILE NA MATENDO YAKE NI YALEYALE.. Kama sivyo, subirini basi tuone maajabu ya SERIKALI YA CCM ikiwashitaki mafisadi wote akiwemo kikwete!!!!
 
kuna uwezekano mkubwa wakajivua gamba alafu ngozi mpya ikachakaa mapema, kwani matendo ni yale yale , au gamba jipya likjikwaa kwenye chunvi mzito ya ufisadi ngozi ikachakaa tena, kama ccm inamtaja tena meghj kuwania nafas muhimu ndani yachama hapo si rostamanaendelea kutesa si gamba sasa limechafuka kabla ya wiki moja
 
Byendangwero umenena vema uliposema sera. Kubadilisha watu bila sera nzuri za nchi ni upuuzi mtu maana tutaishia yale ambayo walifanya wale wanaoitwa magamba kwa sasa.
 
Back
Top Bottom