Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa CCM mwaka huu ni kama Lowassa wa 2015, watu (watoto) wanafurika kwenye mikutano yake lakini hana cha kuwaambia

Mackanackyyy

JF-Expert Member
Mar 26, 2019
2,338
5,263
Nakumbuka 2015 nilihudhuria mikutano mitatu mikubwa ya Lowassa lakini niliishia kufedheheka sana, Huyu ni Kiongozi ambaye nilimpenda tangu nilipomwona mwaka 1994 akiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, alikuwa mahiri mno katika kuzungumza, haiba ya kuvutia na mvuto wa Ujana na pesa.

Nilihudhuria Mkutano wake wakati anatangaza nia Sheikh Amri Abeid Arusha, nikahudhuria kampeni zake Jangwani na Mwanza

Lazima niseme nilifedheheka mno, Watu walihudhuria Kampeni zake kwa Mamilioni lakini tuliishia kuhutubiwa na Sumaye na Mzee Kingunge huku Mgombea Lowassa akionekana kuishiwa maneno kabisa ya kusema, alikuwa mpole mnooo.

Fast forward 2020, tunaye Mgombea wa CCM.

Anatembea na Kitabu cha Ilani ya chama chake lakini the most anaweza kusema ni kutaja idadi ya kurasa katika kijitabu hicho, Hana akimaliza kutaja Idadi ya kurasa ya kijitabu hicho anakumbuka Madaraja yake, Flyovers zake na ndege zake, kuna shida gani hadi anakuwa fixated na Haya matofali tu?

Anapata Maelfu ya Watu(watoto na wasanii to be precise) lakini hana cha kuwaambia yani, sana sana akifungua mdomo anashia kugombana na voters na kuwatisha Badala ya kuomba kura, kheee!

Naamini kina Bashiru Watakuwa wamempiga lectures za kutosha kuhusu mambo anayopaswa kuongea, lakini Sasa anaishia tu kucheza Muziki wa Lissu. JK atakuwa anacheka mnooo.

Mgombea wa CCM come on man, wewe ni Rais eti Acha mzaha, kuwa serious kidogo kwenye Kampeni zako, BE BOLD AND REQUEST MDAHALO NA LISSU ikibidi umwage sera zako🤔
 
Lowasa acha kumtaja hadi Lisu alifika bei kununuliwa ni Slaa na Lipumba tu ndio waligoma kufika bei

Rushwa upinzani walio clean ni Lipumba na Slaa tu the rest ni crap wala rushwa wakubwa
CCM Hawatubabaihi
 
Kwahiyo una muunga mkono Slaa kwamba Lowasa alikuwa liability kwa chadema?
 
Jana akiwa kisesa kuna mtu alikuwa akisisitiza maji,maji,maji...magufuli akalopoka...sikia huyo kichaa...yani ilikuwa ni Aibu kwa mtu anaeomba kura.kwakweli anasikitisha sana.inakuaje mwananchi anaongea kelo yake ya maji halafu aitwe kichaa na muomba kura!!
Nyie watumwa hamumjui JPM. Jembe linajiamini. Kwani maji hayako katika ilani ya mwaka huu??!! Sio wajinga Fulani wanatumwa kwa makusudi kwenda kuharibu tu mikusanyiko ya JPM. Nakuhakikishia yule jamaa atampa tu kura JPM kama kweli anayataka maji.
 
Mgombea wa CCM come on man, wewe ni Rais eti Acha mzaha, kuwa serious kidogo kwenye Kampeni zako, BE BOLD AND REQUEST MDAHALO NA LISSU ikibidi umwage Sera zako
 
Nyie watumwa hamumjui JPM. Jembe linajiamini. Kwani maji hayako katika ilani ya mwaka huu??!! Sio wajinga Fulani wanatumwa kwa makusudi kwenda kuharibu tu mikusanyiko ya JPM. Nakuhakikishia yule jamaa atampa tu kura JPM kama kweli anayataka maji.
Tulia mzee ona huku babu zako wanamkubali lisu wewe ni nani upinge
IMG_20200907_210226.jpeg
 
Lowasa acha kumtaja hadi Lisu alifika bei kununuliwa ni Slaa na Lipumba tu ndio waligoma kufika bei

Rushwa upinzani walio clean ni Lipumba na Slaa tu the rest ni crap wala rushwa wakubwa
CCM Hawatubabaihi

Bwaaaahaaa bwahaaaa eti ni Slaa na Lipumba wasiokula rushwa. Yaani urubuniwe na ccm bila rushwa?

Mwaka huu nina raha ya ajabu, ni bora wapinzani tushindwe tukiwa na Lisu, kuliko tungeshinda na Lowassa ile taka ngumu toka ccm. Pia kitendo cha cdm kutokuungana na yule tapeli mwingine Lowassa wa Lindi imenifurahisha sana. Ni bora kubaki wapinzani kumi wa ukweli, kuliko kujiunga na wahuni toka genge haramu la ccm.
 
Hapo Warioba kapeleka ujumbe wa picha kuwa rais aliyepo sasa hafuati katiba wala sheria. Ukiona kiongozi anajisifu kujenga bwawa, reli nk anataka akaombewe kura na bibi wa miaka 90+ tena kwa kumlazimisha, ujue huyo ni kimeo.
Fake news!
 
Back
Top Bottom