- Well, CCM tumeanza kukosa muelekeo kuanzia Mwaka 1995, tulipoanza kuminya katiba ya chama since then imekuwa tafrani tupu, tumekaribisha wafanya biashara wachafu, wezi, viongozi wasiokuwa na uwezo wa kuongoza, infact tumekuwa na viongozi ambao hata uwezo wa kufikiri hakuna, mifano mingine iliyotufikisha CCM hapa ni pamoja na:-
1. Ubinafsishaji:- it was supposed to be a good thing kwa taifa, lakini tukaruhusu viongozi kuingiza mchakato kwenye matumbo yao, matokeo yake ni kwamba karibu viongozi wote wa Awamu ya Tatu sasa ni matajiri wa kupindukia, hakuna aliyewahi kuwa kiongozi wa serikali wa awamu hiyo ambaye sasa ni masikini, hela walizoiba kwenye hili zoezi wakazitumia kutafuta nafasi za uongozi CCM na kutuharibia kabisa utaratibu na katiba za chama za mchakato wa uchaguzi.
2. Vurugu za Katiba ya CCM:- hili alilianza Mwalimu alipoingilia zoezi la mchakato wa uchaguzi wa Rais mwaka 1995, aliyefuata naye akaamua kufuata nyayo, matokeo yakawa kuundwa kwa makundi ndani ya chama kwa njia hii CCM tumewaondoa uongozini viongozi wengi wenye uwezo wa kuongoza na kuishia kujiwekea magarasha, kwa mfano kwenye uchaguzi Karatu Mkapa aliambiwa na CCM kwamba anayefaa ni Dr. Slaa, yeye kwa makusudi akaamua kumuweka mtu wake Quorro, matokeo Slaa akaingia Chadema you know the rest of the story!
2. CCM walikataa Nchimbi asigombee UV-CCM, pamoja na Idd Simba asigombee Wazazi, lakini Mkapa kwa makusudi akisahuriwa na Kingunge, akaamuwa kuwapitisha kwa nguvu na ubabe, matokeo kiongozi madhubuti kama Dr. Gama RIP, wakaishia kumtosa na kumpa Nchimbi the master of political confusion. Mama kilango alishinda kule Ubungo, wao wakatumia ubabe na kumpitisha Keenja, Rage alipoonekana kuwa tishio kule Tabora wakamfunga jela, people I can go on and on of how CCM tulifikia kuvaa magamba! Sasa mnashangaa nini ninapotoa ushauri wa namna ya kuyavua ni kwa sababu ninajua jinsi tulivyoyavaa!
3. IPTL, EPA, KAGODA, Richmond, Dowans, haya matatizo matatu sugu ndani ya CCM simply tumeletewa na mapacha watatu, na mpaka leo wanatusumbua kwa sababu ya hela walizopata toka kwenye haya matatizo, sasa utavuaje gamba kama hujui hata gamba ni nini na umelipata wapi? Hawa mapacha watatu siku zote wamekuwa na vibaraka wao na tunawajua sana, sasa hivi na wao wanajaribu kujifanya wapo na sisi kwenye kudai kujivua,
I mean CCM sasa tumefika njia panda maamuzi magumu sana yanahitajika kama tunataka kuendelea kutawala hili taifa, hakuna aliye bigger than CCM, nguvu za Mwenyekiti wa CCM sio tatizo, tatizo ni sisi wanachama wa CCM na hasa wananchi wa hili taifa ni wanafiki mno na tunapenda sana siasa za kuchumia matumbo tu, badala ya kujali taifa, kwenye kikao kilichopita NEC ninajua jinsi vijana walivyokuja juu na mpaka kuwatosa hawa mapacha, sasa tunahitaji kuwaondoa kabisa kwenye chama sio haoa mapacha watatu tu tushuke mpaka chini kwenye vibaraka wao, na wote tunawajua kama huamini nenda upekue JF utakuta wote kwani tumewajadili sana humu, sasa eti kuna wanaoshangaa kama vile nimetoa hizi habari toka Mars, ndio nianita unafiki wa ajabu sana wa sisi wabongo!
- Some of us hatukuumbwa na unafiki na uongo uongo na sura mbili, people what you see here it is me, hakuna wa kuchonga wala nini me! Sasa suka au unyoe
William @ NYC, USA.