mizambwa
JF-Expert Member
- Oct 8, 2008
- 4,421
- 1,792
Baada ya Chadema kufanya mikutano ya hadhara mbalimbali katika mikoa, wilaya, kata na vijiji nchini, hali ambayo imekivuruga chama cha mapinduzi, kuna tetesi kuwa CCM nayo imeanza kujipanga kuijibu CDM kwa kupitia maeneo yote ambako viongozi wa kitaifa wamepita. Habari zinaongeza kuwa viongozii wa ngazi ya Taifa, watapita maeneo yote waliyopita viongozi wa taifa wa CDM wakati viongozi wa mikoa yote nchini, wataendesha ziara katika kila wilaya kurudisha wanachama wa CCM waliovua gamba na kuchota wanachama kutoka CDM na vyama vingine vya upinzani. Katika harakati hizo, viongozi wa wilaya nao watatakiwa kufanya ziara (baada ya viongozi wa mkoa kupita) kila kata na kijiji ili kuhakikisha CCM haiendelei kupoteza wanachama.
Nadhani kwa mkakati huu, CCM inaweza kujaribu kurudisha imani yake kwa wananchi. Inagawaje, ni kama WAMECHELEWA
Tusubili tuone ngoma itakavyochezwa
CCM ni chama Tawala kinachomiliki Dola. Hivyo hakipaswi kufanya mikutano ya hadhara ili kuwaeleza wananchi nini inakifanya.
Wanatakiwa wafanye vitu katika kutimiza Ilani na Ahadi za Chama ili wananchi waone hii inatosha.
lakini wakienda Jukwaani na kuongea, wananchi watawadharau kwa sababu watu hawataki propaganda bali vitendo.
Na uwezo wa kufanya vitendo vitakavyoonekana, CCm wanao isipokuwa wanakumbatia Ubinafsi na kukosa Fikra za kufikiria wafanye nini ili kurudisha Imani ya Chama kwa Wananchi wa Tanzania.
Ni wakati sasa kwa Viongozi wa CCM kuamka toka usingizini vinginevyo................
View attachment 54939
............ Yangu macho!!!!!!!!!!!!!
MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!