CCM kujibu mapigo dhidi ya CHADEMA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM kujibu mapigo dhidi ya CHADEMA?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MPAMBANAJI.COM, May 30, 2012.

 1. MPAMBANAJI.COM

  MPAMBANAJI.COM JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  Ni kwa kasi isiyotarajiwa ya kwamba CDM inafahamika kwa kiasi kikubwa mingoni mwa watanzania huku CCM kikionekana kuwa chama cha vikundi....Katika hili tunaomba nacho/CCM kifanye mikutano Arusha, Dar na maeneo mengine yote ambayo CDM imepita ili nasi kuwaonyesha watanzania ya kuwa tupo hai na tunakubalika bado.


  naomba awepo Raisi,Katibu mkuu, Nappe na baadhi ya wabunge kama ambavyo CDM wanafanya.Hapa tutajipima vyema. Mkutano huu usiwe wa kiserikali ila wakichama katika kuhamasisha maendeleo na uelewa wa demakrasia haki na wajibu.


  AKSANTEEEEEEEEEEEEEEE


  Otherwise PEOPLES'S POWER ITATAWALA
   
 2. S

  Senator p JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: Oct 27, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Onyo!
  Msije mkaenda vijijini na mafuso ya kubebea n'gombe mkajaza wa2 kuleta kwenye mkutano,na wala msiwahonge kofia,kanga,masufulia na kuwapikia wali waachen waje wenyewe.Hapo 2taona km kwel.
   
 3. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Programme hizo zitakifilisi chama kutokana na gharama kubwa ambazo chama kitaingiia ili kushawishi watu na gharama za rais kuwepo mahali ni kubwa siyo kama Dr. Slaa.

  Chama cha Mapinduzo ndiyo kipo madarakani hakiitaji kujikita kwenye siasa za majukwaa zaidi ya utekelezaji wa ilai yake ambayo ndiyo kampeni kubwa kuliko kushinda kwenye majukwaa.
   
 4. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Nonsense....Nadhani mngehamasishana mkatekeleza ahadi na sio vinginevyo....Mikutano haiwezi kuwasaidia chochote. Maisha bora kwa kila Mtanzania yanahitajika kwa kasi zaidi, ari zaidi na nguvu zaidi......
   
 5. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Watu wataenda kula UBWAWA tu, hakuna mwenye mapenzi na CCM.

  profilepic 2012.JPG


  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
 6. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  mikutano ya ndani tu ngazi ya wilaya kwenda huko kwenye kata na matawi koram haitimii. vikao vya mikoa na taifa ndo vinatimiza koram tu kwa sababu kuna makulaji. sijui
   
 7. M

  Mbozwo Member

  #7
  May 30, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dalili zakufa izo. Kweli nimeamini kira jambo linawakati wake.
   
 8. RICARDO KAKA

  RICARDO KAKA JF-Expert Member

  #8
  May 30, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 867
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  wafuasi wa MAGAMBA wanahongwa ili waende kwenye mikutano wakati sisi CHADEMA tunaenda kwa mapenzi yetu na uzalendo wa nchi yetu.
  bila posho hakuna kada wa GAMBA ambaye atahudhuria..........!!!!!!! hii ni hadithi ya kweli ndugu zangu:israel:
   
 9. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #9
  May 30, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Baada ya Chadema kufanya mikutano ya hadhara mbalimbali katika mikoa, wilaya, kata na vijiji nchini, hali ambayo imekivuruga chama cha mapinduzi, kuna tetesi kuwa CCM nayo imeanza kujipanga kuijibu CDM kwa kupitia maeneo yote ambako viongozi wa kitaifa wamepita. Habari zinaongeza kuwa viongozii wa ngazi ya Taifa, watapita maeneo yote waliyopita viongozi wa taifa wa CDM wakati viongozi wa mikoa yote nchini, wataendesha ziara katika kila wilaya kurudisha wanachama wa CCM waliovua gamba na kuchota wanachama kutoka CDM na vyama vingine vya upinzani. Katika harakati hizo, viongozi wa wilaya nao watatakiwa kufanya ziara (baada ya viongozi wa mkoa kupita) kila kata na kijiji ili kuhakikisha CCM haiendelei kupoteza wanachama.

  Nadhani kwa mkakati huu, CCM inaweza kujaribu kurudisha imani yake kwa wananchi. Inagawaje, ni kama WAMECHELEWA

  Tusubili tuone ngoma itakavyochezwa

   
 10. M

  MAKAWANI Senior Member

  #10
  May 30, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Watakapozomewa wasilalamike!
   
 11. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #11
  May 30, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,164
  Likes Received: 1,167
  Trophy Points: 280
  kilichofanya watu kupoteza imani kwa ccm si kukosekana kwa mikutano, sababu wanaijua sana tu. Nionalo hapo ni ufisadi mwingine unapangwa na kubarikiwa, kwa kufanya mambo ambayo hayakuwa ktk bajeti. Wanaposubiri kutenda kwa kuangalia cdm watafanya nini huo ni uhayawani!
   
 12. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #12
  May 30, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  sasa wakiamua kujibu mapigo uchumi nani atasimamia, maana wao ndiyo wako madarakani, ina maana na wao ni wapinzani?????
   
 13. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #13
  May 30, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  We do encourage piracy because it will KEEPS M4C in the ears of voters.Wache wajaribu itawagharibu lakini haitawasaidia.

  Mytake: Hata wakifanya mfumo wao hautaweza kufana na wa CDM!Wakicopy hii CDM watakuja na kali zaidi coz CDM is where Creativity lies.
   
 14. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #14
  May 30, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Tatizo si CCM kufanya mikutano ni nini watakachowaambia wananchi, kwa sababu wamekuwa wakifanya mikutano kwa takriban miaka 50 sasa. Labda kama wanataka wafanikiwe waende na majibu kwa nini hali ya maisha inazidi kuwa ngumu na wanafanya nini kuboresha hali hiyo. Wakienda kuhubiri CDM ni ya kaskazini hayo siyo majibu wanayotaka wananchi, vinginevyo wajiandae kuzomewa.
   
 15. N

  NewOrder JF-Expert Member

  #15
  May 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 489
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Ningefurahi sana kuona sasa wananchi wakichukua hatua!! Ukiona gari la Waziri, Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa, Mwenyekiti wa Halmashauri au Meya - jua ni sehemu ya matumizi mabaya ya mali ya UMMA!!

  Kama viongozi hao ni viongozi wa serikali, hawapaswi kujishughulisha na siasa. Wanatumia vibaya muda wa serikali, wanajilipa pesa za kujikimu wao pamoja na madereva, mafuta na kadhalika!

  Hii itakuwa alama muhimu sana ya kutenganisha watendaji wa serikali na siasa. Mimi ni mmoja wa wanaoamini kutohitajika kwa wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa, mawaziri ambao ni wabunge wa kuchaguliwa na hata kuteuliwa. Mkanganyiko huu wa kofia hizi mbili au hata tatu ndio chanzo za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka na mali ya UMMA!!
   
 16. M

  MLERAI JF-Expert Member

  #16
  May 30, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 673
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Ccm kujibu hoja za cdm jukwaa ni kuzidi kujipotezea umaarufu wanachotakiwa ni kujibu kwa vitendo washughulikia hali ngumu ya maisha walio nayo wananchi.Kupanda jukwani na kuanza kurusha maneno bila vitendo itakuwa ni sawa mke aliyesikia mumewe anatoka nje ya ndoa badala ya kujichunguza nini kilichomfanya mumewe amsaliti nae anaanza kutoka bila kujua anazidi kuonyesha kasoro zake kwa hata watu ambao hawajui na kuambulia aibu
   
 17. j

  joeprince Member

  #17
  May 30, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Walisema wanohama ni magamba mapigo ya nini tena?
   
 18. F

  FJM JF-Expert Member

  #18
  May 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  CCM wakumbuke kuchukuwa report ya utekelezaji wa ahadi zake (kama kuna kitu wametekeleza)!

  Kwa uzuzu wao wanaweza kweli kuanza kulamba miguu ya CHADEMA kwa kupita sehemu walizofanya mikutano ya haadhara, lakini tofauti na CHADEMA CCM wanatakiwa wawaambie wananchi ni kwa nini nchi ni maskini?
   
 19. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #19
  May 30, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  CCM kama chama tawala hakiwezi kurudisha imani yake kwa wananchi kwa kufanya kazi kama chama kilicho nje ya madaraka. CCM wanaweza kufanya propaganda kwa kuwapatia watu pesa za msimu ili kionekane bado kina watu.

  CCM ikumbuke kuwa kila mara wananchi wanapokosa ajira, huduma za afya kuwa duni, elimu kudidimia, umeme kuwa kitendawili, uhalifu kuongezeka, ufisadi kuwa wa kutisha, vijana kutojua hatma ya maisha yao na matatizo lukuki kama kupanda bei kwa bidhaa basi ni dhahiri umaaru wa CCM miyoni mwa watanzania unakuwa lowest na kuone kuwa kuna haja ya kupata serikali nyingine labla mambo haya yatafanyiwa kazi.

  Njia pekee ya kurudisha imani kwa wananchi si kwa CCM kupita majukwaani na kuanza kukanusha kuwa, Maisha si magumu, ufisadi haupo, umeme unapatikana 24hours 7 days a week. Bidhaa nyingi ni affordable kwa wananchi, ajira zipo kwani wananchi wote Tanzania wana ajira nzuri tu. CCM kwa kutumia serikali yake ingeweza kuchagua eneo moja na kuwa focus kwa mwaka mzima (mfano nishati), baada ya mwaka nishati inakuwa Histori, then inakuja eneo jingine la viwanja kwa mwaka mzima, then katika kila mkoa kuna na at least viwanda 6 vyenye kuajiri watu 50,000 tu watu hawa watakuwa na uhakika wa kipato cha mwezi na hivyo ku-spend na kufanya wakulima na wafanya biashara ndogondogo nao kuwa na uhakika wa wateja.

  Huwezi kuza uchumi wa kuwapatia kazi kubwakubwa maswahiba wanaopeleka hela off shore, kama tenda za serikali zingekuwa zinatolewa kwa small business ni dhahiri hawa ndiyo spenders wa ndani siyo akina EL au RA like, ambao wakipata mafua wanapeleka hela hospitali za offshore badala ya kuzipeleka local hospital na kuongeza ajira. Kuna mambo mengi sana ya micro-economics and macroeconomics ambayo CCM ikiacha ulafi inaweza kuwaongezea umaarufu kwa wananchi na si kukimbilia majukwaani kujibu hoja ambazo zinawaumiza wananchi halafu ukaseme haziwaumizi.
   
 20. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #20
  May 30, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,982
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  nimeikubali hii.
   
Loading...