Bundewe
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 400
- 141
Chama cha magamba kwa sasa kimepoteza mvuto kwa wananchi hasa vijana. Hili halina ubishi na limeshasemwa mara nyingi. Tathmini yangu ni kwamba, ifikapo 2020, chama hiki hakitakuwepo tena au kitakua kama UDP ilivyo sasa. Kwanza kuanzia 2015 kitakua chama kikuu cha upinzani. Hii ni kutokana na ukweli kwamba makada wengi waaminifu wa chama hiki ni wazee ambao kwa kweli ifikapo mwaka 2020 ama hawatakuwepo tena au watakua wazee sana kiasi cha kushindwa kabisa kufanya siasa. Vijana wanaotegemewa sasa ndani ya chama hicho watakua wameshakihama kwa kuwa hata sasa wameshindwa kuonesha mapenzi ya kutoka moyoni kwa chama, wapo kimaslahi zaidi. Mfano ni Nape aliyekaribia kujiunga cdm/mwanzilishi wa CCJ, Januari na Ridhiwani wanavutwa na wazazi wao. Shigela na akina Malisa ni maslahi yanayowafanya wabaki. Akina Bashe na Kigwangala sio wa kuwaamini. UVCCM yenyewe ni mtifuano kila kukicha.
Ifikapo Mwaka 2020, asilimia 75 ya wapigakura watakua hawaujui mfumo wa chama kimoja, maana watakua wamezaliwa baada ya vyama vingi kuingia. Aliyezaliwa 1992 atakua katimiza miaka 28. Wazee wanaopiga siasa sasa hivi ndani ya ccm hawatakuwepo mwaka huo, hawa ndo wazee ambao wamewajenga watu uoga wa kudai haki zao kwa maandamano wakidai yataleta machafuko. watabaki historia. Kitendo cha kushindwa uchaguzi mkuu 2015 kitakigawa zaidi chama hiki kikongwe, na kukidhoofisha zaidi, maana hata baada ya ushindi kiduchu mwaka jana tayari chama kimeyumba kwa kutafuta mchawi. Baada ya uchaguzi wa 2020, hakitapata wabunge wa kutosha kuunda kambi ya upinzani bungeni, badala yake CUF itaungana na NCCR kuunda kambi rasmi ya upinzani. Wakati huo Chadema ndo itakua madarakani.
Ni tathmini yangu tu wadau, wakuu mnasemaje?