CCM Kufa ifikapo 2020 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Kufa ifikapo 2020

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bundewe, Jun 17, 2011.

 1. Bundewe

  Bundewe JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Chama cha magamba kwa sasa kimepoteza mvuto kwa wananchi hasa vijana. Hili halina ubishi na limeshasemwa mara nyingi. Tathmini yangu ni kwamba, ifikapo 2020, chama hiki hakitakuwepo tena au kitakua kama UDP ilivyo sasa. Kwanza kuanzia 2015 kitakua chama kikuu cha upinzani. Hii ni kutokana na ukweli kwamba makada wengi waaminifu wa chama hiki ni wazee ambao kwa kweli ifikapo mwaka 2020 ama hawatakuwepo tena au watakua wazee sana kiasi cha kushindwa kabisa kufanya siasa. Vijana wanaotegemewa sasa ndani ya chama hicho watakua wameshakihama kwa kuwa hata sasa wameshindwa kuonesha mapenzi ya kutoka moyoni kwa chama, wapo kimaslahi zaidi. Mfano ni Nape aliyekaribia kujiunga cdm/mwanzilishi wa CCJ, Januari na Ridhiwani wanavutwa na wazazi wao. Shigela na akina Malisa ni maslahi yanayowafanya wabaki. Akina Bashe na Kigwangala sio wa kuwaamini. UVCCM yenyewe ni mtifuano kila kukicha.

  Ifikapo Mwaka 2020, asilimia 75 ya wapigakura watakua hawaujui mfumo wa chama kimoja, maana watakua wamezaliwa baada ya vyama vingi kuingia. Aliyezaliwa 1992 atakua katimiza miaka 28. Wazee wanaopiga siasa sasa hivi ndani ya ccm hawatakuwepo mwaka huo, hawa ndo wazee ambao wamewajenga watu uoga wa kudai haki zao kwa maandamano wakidai yataleta machafuko. watabaki historia. Kitendo cha kushindwa uchaguzi mkuu 2015 kitakigawa zaidi chama hiki kikongwe, na kukidhoofisha zaidi, maana hata baada ya ushindi kiduchu mwaka jana tayari chama kimeyumba kwa kutafuta mchawi. Baada ya uchaguzi wa 2020, hakitapata wabunge wa kutosha kuunda kambi ya upinzani bungeni, badala yake CUF itaungana na NCCR kuunda kambi rasmi ya upinzani. Wakati huo Chadema ndo itakua madarakani.

  Ni tathmini yangu tu wadau, wakuu mnasemaje?
   
 2. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Kwani huo ugonjwa aliosema mtikila una dawa?
  Hawawezi kufika mwaka uo.
   
 3. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,550
  Likes Received: 4,675
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona umewapa muda mrefu saana hawa magamba? Labda kama wana tumia ARV vinginevyo mwisho wao hawa ni 2015.
   
 4. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Wewe ndieye uliye rithi mikoba ya shehe wa migo?
   
 5. Bundewe

  Bundewe JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Shehe alikua anasoma alama za Majini......mi nasoma alama za nyakati. 2020 CCM kwishney!
   
 6. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa, mwaka huo Mnyika ndo Atachukua urais wa nchi hii, mimi waziri mkuu.
   
 7. H

  Hache Member

  #7
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mi naona kuanzia 2016 watakua chama kikuu cha upinzani kama cuf na nccr wakiwaachia nafasi.
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Jun 17, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,467
  Likes Received: 4,126
  Trophy Points: 280
  Kwa jinsi mambo ya ndani ya chama yanavyoenda, huko ni mbali sana.
   
 9. N

  Ntandalilo Member

  #9
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nothing lasts forever mkuu.................... yatatimia tu!!! Amen.
   
 10. F

  FUSO JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,808
  Likes Received: 2,291
  Trophy Points: 280
  No, tutampa Hiza na wewe ndiyo utakuwa katibu mwenezi wake.
   
 11. Bundewe

  Bundewe JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Cuf watakua wameungana rasmi na ccm na kuunda CCF
   
 12. f

  fazili JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,192
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  yap ni kama ya Kenya na KANU
   
Loading...