CCM kuboresha maslahi ya watumishi wake

Lilombe

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
242
39
Na Jumbe Ismailly, Iramba

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinaandaa utaratibu wa kuhakikisha kinaboresha maslahi ya wafanyakazi wake kuanzia ngazi ya shina hadi taifa mara tu kitakamilisha kuboresha vyanzo vya mapato yake.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM Taifa, Bw. Lameck Mwigulu alipokuwa akizungumza na viongozi pamoja na wanachama wa chama hicho kwenye Ofisi za Kata ya Iguguno, wilayani Iramba, waliompokea kwa ajili ya kumpongeza kwa kuteuliwa kwake kushika nafasi hiyo.

Kwa mujibu wa Bw. Mwigulu katika kufuatilia ameona ni jambo muhimu
kuboresha maslahi yao kwa ngazi zote kwa madai kwamba licha ya maslahi madogo pamoja na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo kiutendaji, lakini bado wameonesha kuwa na nidhamu ya hali ya juu kuliko eneo jingine lolote.

“Tutaboresha maslahi ya wafanyakazi wa chama, wafanyakazi wa chama ni kuanzia ngazi ya juu mpaka watu wetu ambao ndugu yetu amewaimba pale, mpaka ngazi ya shina,” alifafanua Mwigulu na kuongeza:

“Tumeona hilo ni jambo la msingi sana, katika kufuatilia nanyi mtakubali wafanyakazi walio na nidhamu sana ambao sijawahi kuona wanagoma ni wafanyakazi wa CCM, nyie mlishawahi kuona wanaandamana, hawajawahi kuandamana,” alisisitiza Mwigulu ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi.


“Sasa kwa namna hiyo kwa kweli namshukuru sana mwenyekiti kwa kuliona hilo sasa, mimi kama mkuu wa kitengo hicho nitasimamia utekelezaji wake tuone tunaweza tukafikia lengo hilo,” alisema huku akiahidi pia kuangalia madai yao mengine kama vile uhamisho.

“Na namna ya kulifanya hili kuna namna mbili, kuna yale yaliyo maslahi yao na kuna yale yaliyo madai, wafanyakazi wapo wengi sana ambao baada ya kuhama wana madai yao, kwa hilo tutapunguza madai hayo mpaka tumalize na kisha tuboreshe maslahi yao,” alisisitiza.


Source; gazeti la Majira, May 2, 2011

BRAVO CCM KWA KUTAMBUA UMUHIMU WA KUBORESHA MASLAHI, ILI KUONGEZA TIJA NDANI YA CHAMA!
 
Eeehh, wataboreshea fungu gani hilo maslahi kwa wafanyakazi wake wakati hata ruzuku yenyewe imepungua sana tofauti na mahitaji makubwa pamoja na changamoto mbalimbali zinazokikabili CCM hivi sasa kisiasa nchini????????????
 
Back
Top Bottom