PostGE2025 CCM kubalini yaishe, mtamponza Mama Samia

PostGE2025 CCM kubalini yaishe, mtamponza Mama Samia

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Nani sasa wa ku-take blames kila raisi hataki jumba bovu limuangukie ataweka hata milingoti ili kumsukumia ajae and that is what they do
 
CCM ilishakufa kitambo tu. Kwa sasa kuna genge tu la wahuni wachache. Na hawa ndiyo wanaomuendesha huyo mama kama gari bovu.
Ni kweli kabisa na uzuri Watanzania wenye akili wameshaligundua. Hata wakati wa Chama kimoja Nyerere hakuwahi kufanya kufuru hii ya mauaji .Eti mtu akikosoa basi adhabu yake ni kifo? Haikubaliki kabisa😭😭😭
 
Mbona ccp yq china ipo mpaka leo
CCP ya China ni chama chenye maono na wanatumia Meritocracy yaani Uwezo wa Kiongozi unakuwa vetted na muendelezo wa matendo na akili yake kwa muda mrefu.
Wanapanga mipango yao mbele ya wakati.

CCM kwa upande wake ilikuwa wakati wa kuundwa kwake ikiwa na misingi ya kutetea Wakulima na Wafanyakazi na ikifuata falsafa ya Ujamaa. Lakini kwa Sasa imepoteza Dira, sio chama cha siasa, ni kikundi cha kutawala si kwa ushawishi bali mabavu. Viongozi wake hawana Falsafa na dira, wanalojua ni kuendeleea kushikilia dola. Njia hii inayokosa ridhaa ya Umma haiwezi kwenda umbali mrefu
 
Wengi wao si watu wakusoma nyakati, wamekariri kuongoza kwa vitisho
 
Nani sasa wa ku-take blames kila raisi hataki jumba bovu limuangukie ataweka hata milingoti ili kumsukumia ajae and that is what they do
Ilibaki kidogo limwangukie Kikwete, ila Kikwete ni mtoto wa mjini tofauti na huyu hana huo ujanja.
 
Poleni sana CCM tulikuwa nanyi siku za mateso lkn Mungu amewapenda zaidi.
 
CCM kubalini uwezo wenu wa kuongoza taifa umefikia mwisho, umegota na kila lenye mwanzo halikosi mwisho.

Ili kukinusuru chama kwa muongo mwingine ujao mshaurini Samia ajiuzulu, iandikwe katiba mpya uchaguzi urudiwe hiyo ndiyo itakuwa salama yenu.

Kuendeleza jeuri kuwa sisi ndio chama tawala mtafutika kwenye uso wa dunia na kubaki jina kama vilivyo vyama vingine vya ukombozi ikiwemo KANU.

Kuendeleza jeuri ni kumtengenezea Mwenyekiti wenu njia ya kuelekea ICC na kumshushia heshima kimataifa, mnaona hizo roho elfu 10 hazitoshi mnataka kumwongezea zingine, muwe na huruma.

Mauaji yaliyotokea October 29 si tu yamelitia doa Taifa la Nyerere bali yamekitia doa chama cha Mapinduzi CCM, yameutia doa utawala wa Rais Samia, maana haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa Tanganyika.

CCM mtambue kuwa hamuongozi kizazi cha miaka ya 60 kina Butiku mnapambana na kizazi cha 2000 ambacho hakina kitu cha kupoteza zaidi ya maisha yao.

Sioni ni kwa njia gani hili wimbi la mabadiliko yanayoshinikizwa na vijana wa Gen Z mtayazuia kwa mawazo ya kizamani ya kina Wassira, kina Nchimbi, kina Kabudi ya kutumia vitisho vya dola, udini yatafanikiwa.

Mlitumia vitisho vya polisi vijana wakaandamana, mmewaua kwa maelfu wamepanga kuandamana tena. Na kete mnayotumia ya Udini ndiyo itakayokuwa kaburi la CCM na mnamchimbia Mama kaburi lake kwa mikono yenu.

ITUNZENI HII LISTI IWE KAMA REFERENCE KWA SIKU CHACHE ZIJAZO.
Who are you
 
Who are you
IMG_20251206_120554.jpg
 
Back
Top Bottom