CCM kuanzisha Miradi kukwepa fedha haramu, Mh!!!!!!

Njaare

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
1,081
275
Katika hatua nyingine, CCM kimetangaza rasmi kuanzisha kampuni za biashara na kuimarisha mapato kwenye miradi yake ili kuwa na nguvu ya kifedha na hivyo kujiepusha na fedha chafu zinazoweza kutoka kwa wafadhili.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisi ndogo za CCM Lumumba, Kisumo alitangaza mpango huo ambao sasa chama kitajikita katika kufufua vitega uchumi vyake.

“Kuna wafadhili ambao wamekuwa wakiichangia CCM na Chadema hadharani kama akina Sabodo, lakini wako wengine wanachangia kwa siri, sasa kuna hatari ya kupokea fedha chafu kutoka kwao,” alionya Kisumo.

Alisema chama hicho kinahitaji fedha lakini siyo fedha chafu ambazo zimepatikana kwa kukwepa kodi.


Source: Kisumo: Ngeleja, Maige wanamdhalilisha rais

Mawazo yangu,

Angetueleza kwa nini Sukita ilikufa na wana mkakati gani kuhakikisha kuwa hizo biashara hazifi tena kama sukita!!!
 
Epa,meremeta na kampuni kama hizo ndo anaongelea au.nafikiri ni wakati wa kuziendeleza kwani tayari zipo na mtaji wake si kazi kuupata na vilevile haziwezi kufilisika.
 
Wanaongelea fedha za Saboda(Soboda) kwasababu wanaona Wivu anawapa pesa zaidi Chadema

Mfa Maji haachi kutapatapa
 
Fedha chafu mh! haya maeneo walojimilikisha kwa lazima mfano uwanja wa kirumba, nayo yarudishwe serikalini kama kweli wana lengo la sivyo huo ni usanii mtupu.
 
Hivi kweli CCM inashida ya fedha mpaka ianzishe makampuni ya kibiashara? Je maegesho ya magari, viwanja vyote ambavyo wanavyo?!
 
Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisi ndogo za CCM Lumumba, Kisumo alitangaza mpango huo ambao sasa chama kitajikita katika kufufua vitega uchumi vyake.
Haya mawazo ya vyama kuwa na vitega uchumi sio mazuri ingawa nia yao inaweza ikawa ni nzuri.
  1. Tatizo la chama kufanya biashara ni pale kitakapokuwa madarakani; maana itakuwa ni vigumu sana kuhakiki mahusiano ya hizo biashara na vyombo vya serikali (conflict of interests).
  2. Sheria yetu inatakiwa iwe wazi kabisaa katika kusaidia kutenganisha biashara na siasa. Hivi viwili vimeshaonyesha wazi nchini kwetu kuwa ni sumu kubwa ya utawala bora.
  3. CCM wasiweke misingi mibaya kwa nchi wakidhani wao watakuwa madarakani daima, kwani wakiondolewa kwenye kiti cha utamu wasitegemee kuwa chama kitakachofuatia kitaondoa mambo yanayokinufaisha chama kilichopo madarakani.
 
Wezi wa kubwa wanamdanganya nani wanadhani wote hatufahamu au tuanike makampuni yao wana mapakampuni zaidi ya 200 sema sasa wanazidiane kete wezi wamekubuhu na wengene wamejanjaruka hawataki kuibua wanaona yatakuja kumwagwa hadharani Tabia ya viongozi wa CCM ni uongo sasa hivi wanadhani wanatuzuga kumbe tunajua janja yao since
 
Mwaka jana walitumia Kampuni ya Mwana dada mmoja kuwakusanyia michango toka kwa wafanyabiasha ra aje Yusufu Makamba akatae kama hatutaja hiyo Kampuni the girl she is damly rich sasa ,wamewatumia wafanyabiashara kwatika harakati za kujiokoa wanawaona midabadwa CCM are users ni sawa na viongozi wanaohamia kwao wakiwatumia huwatosa na kuwapoteza kisiasa
 
Atakataaje fedha chafu wakati wenye fedha chafu wamo kwenye chama chao (CHAMA CHA MAGAMBA)
kwa hili amepotoka........
 
Back
Top Bottom