CCM: Kiongozi atakayeshirikiana na mashirika ya kimataifa kufutwa kazi

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Chama Tawala Tanzania: Kiongozi wa serikali atakayeshirikiana na mashirika ya kimataifa nchini atapoteza kazi

Katibu Mkuu wa chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Dk Bashiru Ally amewaonya mawaziri na watendaji wa chama hicho tawala nchini humo kwa kuwataka waache kushirikiana na asasi na mashirika ya kimataifa yasiyoshirikiana na serikali na kusisitiza kuwa yeyote atakayebainika kufanya hivyo basi atapoteza kazi yake.

Dk Bashiru pia amezitahadharisha asasi hizo za kimataifa kuhusiana na kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Katibu Mkuu wa chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania ametoa kauli hiyo leo Alhamisi wakati akizungumza na wajumbe wa chama hicho mkoa wa Magharibi mjini Unguja, visiwani Zanzibar.

Ameendelea kufafanua kwamba, ni marufuku ofisi yoyote ya chama cha CCM kufanya kazi na taasisi za kimataifa zisizokua na uhusiano mwema na chama hicho tawala.

Aidha Dk Bashiru Ally ameenda mbali na kufafanua kwamba kuwepo kwa taasisi za kimataifa nchini Tanzania isiwe sababu ya kuingilia masuala ya ndani ya nchi yasiyoyahusu mshirika hayo.

Kauli hiyo ya CCM imekuja ambapo kwa mara kadhaa asasi mbalimbali za kimataifa zimekuwa zikiinyoshea kidole cha lawama serikali ya Dar es Salaam kwa kudai kuwa imekuwa ikikiuka haki za binadamu.

Katika uwanja huo katikati ya mwezi Oktoba mwaka huu, mashirika ya kutetea haki za binadamu ya Amnesty International na Human Rights Watch yaliituhumu serikali ya Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania kuwa inakiuka haki za binadamu.

Ripoti mbili tofauti zilizotolewa na mashirika hayo zilidai kuwa, tangu Rais Magufuli aingie madarakani mwaka 2015, Tanzania imekuwa ikitekeleza sheria ambazo zinabinya uhuru wa vyombo vya habari sambamba na kubana harakati za vyama vya siasa na mashirika ya kiraia, madai ambayo yalikanushwa na serikali ya nchi hiyo.
 
Huyu apuuzwe tu, anahangaika kama kuku aliyekatwa kichwa.
 
Huyu Bashiru Ally mbona alikuwa ana akili sana, sasa imekuaje?
Akina Rwekaza Mkandara aliyemtoa jalalani si watakuwa wanaona aibu sasa?
Usimlaumu
1572191514899.jpeg
 
Awamu hii hawaitakii mema hii nchi,wameweka maslahi binafsi mbele hawana cha kupoteza,wanachojali ni kukaa madarakani mpaka wafe
 
Haya ndio matokeo ya badala ya kulishana Keki wanalishana ma Sumu ccm
 
Ndo maana mm siamini ktika uchawi au ulozi!mijitu km hii unaitupia ukichaa tu iende mirembe!

Hao waloza hawawaoni km hawa nao ninkero??tutatulieni hii kero wachawi jaman!au mmtupe Madibira huko aamke amevaa bikini !atajua atarudije dar..mbaafu!
Haahahahahaahahahaah
 
Basi ndugu zangu ile hofu ya TumainEl ni dhahiri!!!maafisa usalama wa nchi mtuombe radhi watz kwa kumpigania kichaa kushika dola!!!
 
Back
Top Bottom