Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Hali si shwari katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha, baada ya watiania wa udiwani zaidi ya 10 kutoka hadharani na kuwalalamikia baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa mkoa wa Pwani na wilaya ya Kibaha, kuchakachua majina ya waliopitishwa na Kamati Kuu ya CCM ili kupigiwa kura na wajumbe.
Ally Mwinyi Simba, Mtiania nafasi ya Diwani Kata ya Misugusugu kwa niaba ya watiania wenzake, amesema viongozi wa wilaya na mkoa wamegoma kuwapa majina yaliyotoka Kamati Kuu kwa madai kuwa ni nyaraka ya siri.
Simba, amesema viongozi hao wamekuwa wanawapa taarifa walioteuliwa kwa njia ya barua huku wengine wakipigiwa simu, lakini wao wanaoambiwa hawajateuliwa wananyimwa uthibitisho kuwa hawapo katika orodha hiyo.