William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,466
- Thread starter
-
- #121
Mkuu FMES,Saluti Mkuu! Hapo juu nakunukuu ukisema "tatizo kuu ni ufisadi na likitatuliwa matatizo mengine ya taifa letu yatajiondoa yenyewe", ndivyo ilivyo Mkuu? Sio kwamba ufisadi (malfeseance) ni matokeo ya matatizo makuu ya Taifa letu tokea na kabla ya Uhuru? Sio kwamba kwa namna moja au nyingine ufisadi umetokana na mfumo wa uchumi aliotuachia mkoloni ukichanganya na mfumo aliojaribu kuujenga Mwalimu?
- Eti ufisadi ni tatizo la system yetu ya uchumi tuliloachiwa na wakoloni? Can you define this mkuu kwanza kabla sijakujibu post yako nzima? Unasema wakoloni ndio waaliotuachia tabia za kuogopana kwenye uongozi wa juu wa taifa letu ambacho ndio hasa chanzo cha ufisadi?
- Unasema wakoloni ndio waliotufundisha kutoheshimu sheria zetu wenyewe, au the respect kwa rule of our laws? Unasema wakoloni ndio walio-create system ya vigogo kina Kahama, Rupia na Bomani ndani ya political system yetu ambao sasa na wao wamekuja kurithiwa na kina Rostam, Karamagi, na Lowassa, unasema this is wakoloni fault?
- Are you serious mkuu or you are just kidding! Mkuu ukinijbu hili basi nitaichambua post yako nzima, ila kwanza niwekee muongozo hapa!
Respect.
Field Marshall Es!
Haa Hahaaaa!!! Kwi kwi!!!!! ndio maana naipenda JF. Mkuu Kishoka hapo umekata mzizi wa fitina! Ila tu heri umesema wewe kiazi, ningesema mimi mhogo ningeambiwa nina mzizi.FMES,
Mimi si CHADEMA, hivyo unanizushia uongo. Ni sawa kama ningesema wewe ni Fisadi kisa unafahamiana na Mafisadi!
FMES,
Mimi si CHADEMA, hivyo unanizushia uongo. Ni sawa kama ningesema wewe ni Fisadi kisa unafahamiana na Mafisadi!
- I can live with this bila tatizo, tena unakaribishwa anytime ukimaliza na kunihusisha na ufisadi ingawa mimi sujakuita fisadi kwa sababu ya connection ya familia yako na BOT, the oficial shule ya ufisadi Tanzania then tunaweza kurudi tena kwenye real ishus za masilahi ya wananchi wa Tanzania,
- Now let me get this straight mkuu, kama wapiganaji 11 ni mafisadi, na mimi ni fisadi tena kwa 100%, na anytime ukiwagusa wapiganaji on the ishus za upiganaji bila dataz wala facts, it is my duty kujibu na nitawatetea with every ounce of my blood bila kuogopa wala kutishika kama nilivyofanya kwenye hii thread, and in the process you can call me anything you want, lakini siwezi kuwaangusha wapiganaji, they deserve respect tena big time kutoka kwetu wananchi wa Tanzania.
- Mifano ya kisiasa iliyokwisha tokea tayari iko wazi kwamba hatuwezi kuviamini vyama vya siasa nchini kutuokoa, sasa hatuna choice ila kuendelea kuwaamini some individuals member of our society kama kina Mengi, na baadhi ya viongozi wetu kama hawa wapiganaji, maana kama sio hawa tungekua na hali mbaya zaidi kitaifa na ufisadi, Lowassa angekua bado Waziri Mkuu, Msabaha angekua bado waziri, Karamagi angekua bado waziri, Mramba angekua bado waziri, Chenge angekuwa bado waziri, Meghji angekua bado waziri, Mgonja angekua bado katibu mkuu wa wizara, taifa tungekua bado tunalipia Richimonduli.
- Wapiganaji wenye majina ya bandia kwa sababu ya uoga, hatuwezi kuwatukana wapiganaji wanao-deal na mafisadi one on one kila siku ya Mungu in the real life bila ya uoga, it is just not fair na wala sio ustaarabu ni simply kuwa na secret agenda yenye lengo la kuwahadaa wananchi ili kujipatia madaraka, lakini sio kuwajali wananchi na masilahi ya taifa.
Mungu awajalie wapiganaji, na pia Aibariki Tanzania na hasa JF.
Respect.
Field Marshall Es
CCM sasa wasema waunga mkono vita dhidi ya mafisadi
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati amesema chama hicho hakina ugomvi wala uadui na wabunge wake wanaoongoza vita dhidi ya mafisadi nchini.
Kauli hiyo imetolewa siku chache baada ya mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuondoa utata uliotokana na maazimio ya Halmashauri Kuu ya chama hicho ukionyesha kuwa wabunge wanaopiga kelele za ufisadi, wanakichafua chama na serikali yake.
Chiligati ndiye aliyetoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ambayo ilisisitiza kuwa vita hiyo si ya kikundi cha watu wachache bali ya CCM.
Jana, Chiligati alikuwa ni mtu mwenye kuunga mkono kikundi hicho wakati Mwananchi ilipotaka maoni yake kuhusu wabunge hao ambao wanaonekana kukaidi maazimio ya Nec, huku wakitamba kuwa hakuna anayeweza kuwafunga mdomo.
CCM haina ugomvi na wabunge wake wala mtu yeyote anayejitoa mhanga kupinga ama kupambana na mafisadi, alisema Chiligati ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Msimamo wa chama chetu ni kwamba rushwa ni adui wa haki, usichukue, kuomba wala kutoa rushwa, huo ndio wimbo wa kila mwana-CCM.
Hatuna ugomvi wala uadui na mtu yeyote anayepambana na rushwa, ufisadi, uporaji, wizi na ujambazi. Huo ndio msimamo wa CCM.
Baada ya kikao cha Nec kilichofanyika Dodoma mwezi uliopita, Chiligati alisema CCM imeunda kamati ya watu watatu, inayoongozwa na rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi kuwachunguza wabunge wenye tabia ya kuishambulia serikali nje ya vikao vya chama.
Habari za ndani ya kikao hicho ambazo baadaye zilivuja kwa vyombo vya habari, zilieleza kuwa Nec ilimweka kitimoto Spika Samuel Sitta kwa madai kuwa anaruhusu mijadala inayokichafua chama na serikali, huku baadhi ya wajumbe wakishinikiza anyang'anywe kadi ya CCM kwa kile kilichoelezwa kuwa anawapa uhuru bungeni watu wanaoishambulia serikali kwa ufisadi.
Kauli hiyo mpya ya Chiligati, inaweza kuwa imetokana na msimamo wa Rais Kikwete ambaye alisema CCM haiwezi kuwafunga midomo wabunge wake.
Katika mazungumzo yake na wananchi aliyoyafanya kwa njia ya televisheni na redio katikati ya wiki iliyopita, Rais Kikwete alisema kuikosoa serikali ni kuifanya ijiangalie na kujirekebisha na hivyo haiwezi kuwazuia wabunge kuikosoa.
Kauli ya Kikwete ilifuatiwa na ya waziri mkuu wa zamani, John Malecela ambaye alimsifu mwenyekiti wake kwa kuruhusu mijadala hiyo na kuongeza kuwa vita dhidi ya mafisadi ni takatifu kwa kuwa ilikuwapo tangu enzi za TANU.
Tangu kumalizika kwa Nec, wabunge ambao wamekuwa wakijinadi kuwa ni makamanda wa vita dhidi ya ufisadi wamekuwa wakikaririwa na vyombo vya habari wakisema kuwa hakuna mtu anayeweza kuwafunga midomo.
Wabunge hao pia walifanya mikutano ya hadhara kwenye majimbo ya baadhi yao na kusisitiza msimamo wao kuwa wataendelea na vita hiyo kwa kuwa ilani ya CCM inawaruhusu.
Rev. Kishoka;
FMES,
Jadili hoja na don't try to get personal.
Wewe umedai na kunituhumu mimi CHADEMA, nimekuuliza ni lini nimesema kuwa mimi ni CHADEMA? Ndio maana nikakupa mfano wa kusema wewe kujua Mafisadi (na ni mafisadi kweli na si hao Wapiganaji) tuanze kukuita Fisadi. Mfano, kuoana kwa mawazo yangu na Sera za CHADEMA, CUF au hata CCM hakunifanyi mimi niwe mwanachama wa chama hicho. Urafiki wako na Masha, haukufanyi wewe kuwa sawa na Masha ambaye leo hii anayuhumiwa kutumia madaraka yake vibaya na tena sera na itikadi zake haziendani na za "Wapiganaji". Je Wapiganaji wakijua kuwa una Uswahiba na Masha, na wao na Masha ni vitu viwili tofauti, itakuwa sahihi ya wao kukuita Msaliti? Je sisi hapa JF ambao tumekusikia ukimtetea Masha na urafiki wenu tukisikia leo unaandamana na "Wapiganaji" unataka tuanze kukuhoji mahusiano yako?
So please do not try to get personal here. Yes my father worked at BOT and retired in 1994 and he is a peasant right now enjoying his Tshs 25000.00, pension a month, so I am not sure what were you trying to imply here. I have never called on your parents or relatives in relationship of anything that goes in Tanzania or even insinuating anything about them here ta JF or anywhere! So keep of my family and personal life out of this, lets focus on issues.
FMES,
Tukirudi kwenye issues, ni wapi nimesema kuwa Wapiganaji ni mafisadi? Hivi kuhoji nguvu zao na dhamira ya vita hii ni kuwaita Mafisadi?
Hivi nilipouliza kwa nini Spika wa Bunge na Mwakyembe wanahalalisha Rushwa kwa kuwaambia wananchi wakihongwa wachukue hizo fedha kwa kuwa ni "haki yao" badala ya kuripoti Polisi kuwa wamepewa hongo nilikosea?
Previously, umedai kuwa "Wpiganaji" wameanza kazi miaka 4 iliyopita, je miaka kabla ya hapo walikuwa wapi? Hauoni coincidence ya vita vyao na matokeo ya Ugombea uongozi ndani ya CCM 2005 na matokeo yake?
Mbona hawajamwenda Rais na kumuomba ripoti ya Warioba au ripoti ya Chifupa? Sijasikia kwenye mkutano wa Bunge kuwa wamewasilisha hoja binafsi kuomba ripoti hizo ziwekwe hadharani.
Mbona hawakupinga uteuzi wa Mawaziri ambao tangu awali walijulikana kuwa wana chembe chembe za Ufisadi? watu kama Mramba, Karamagi na Chenge?
Unatutukana Wapiganaji wa humu kwa kudai kuwa tunawahada Wananchi. Je unajua ni wangapi humu ambao maisha yetu yameshakuwa hatarini na familia zetu kutokana na kuwa "wasema hovyo"? Je unajua ni sheria ngapi na miongozo mingapi imetunga ili kukabiliana na sisi Wapiganaji tusio na sura?
Je wewe si unafahamu kuwa kuna wengine wetu humu ndani tunawindwa na Mafisadi kwa kutumia dola na vyombo vya usalama kwa kuwa tumewaudhi wakubwa kwa kujua mambo mengi na kufuna siri nyingi? Je huoni kuwa hilo pia ni hatari kwa maisha yetu?
Ikiwa leo dola iliyotawaliwa na Mafisadi kutokana na mfumo mbovu wa kiutawala, inatuma makachero pande zote za dunia kujua nani ni Mwanakjiji, anafananaje, nani Mchungaji alisoma wapi, nani Fundi Mchundo, nani kampa hii habari na wengine wengi, huoni kuwa nasi tunafanya kazi kama hao "Wapiganaji" walioko mstari wa mbele?
So do not ever question my patriotism!
CCM sasa wasema waunga mkono vita dhidi ya mafisadi
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati amesema chama hicho hakina ugomvi wala uadui na wabunge wake wanaoongoza vita dhidi ya mafisadi nchini.
Kauli hiyo imetolewa siku chache baada ya mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuondoa utata uliotokana na maazimio ya Halmashauri Kuu ya chama hicho ukionyesha kuwa wabunge wanaopiga kelele za ufisadi, wanakichafua chama na serikali yake.
Chiligati ndiye aliyetoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ambayo ilisisitiza kuwa vita hiyo si ya kikundi cha watu wachache bali ya CCM.
Jana, Chiligati alikuwa ni mtu mwenye kuunga mkono kikundi hicho wakati Mwananchi ilipotaka maoni yake kuhusu wabunge hao ambao wanaonekana kukaidi maazimio ya Nec, huku wakitamba kuwa hakuna anayeweza kuwafunga mdomo.
CCM haina ugomvi na wabunge wake wala mtu yeyote anayejitoa mhanga kupinga ama kupambana na mafisadi, alisema Chiligati ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Msimamo wa chama chetu ni kwamba rushwa ni adui wa haki, usichukue, kuomba wala kutoa rushwa, huo ndio wimbo wa kila mwana-CCM.
Hatuna ugomvi wala uadui na mtu yeyote anayepambana na rushwa, ufisadi, uporaji, wizi na ujambazi. Huo ndio msimamo wa CCM.
- This is hillarious, Chiligati tena I mean Mungu Alibariki hili Taifa.
- Huyu si majuzi tu aliita wapiganaji walevi?
Respect.
FMEs!
Engineer, Kishoka na FMES;
Naombeni muwe na amani. Hasa nyie wawili FMES na Kishoka jamani tofauti zetu tulizizika kule BCS. Mbona mnaendeleza ugomvi utafikiri hamjuani?, YAP tunajuana kimaandishi na kimtazamo humu.
Ninasisitiza naombeni AMANI iwatawale.
Asanteni sana.
Acha kulia lia wewe kama kasichana ka A level...wacha wakate nondo, hapendwi mtu hapa ni hoja....na si vioroja!
Some people live because it is illegal to................them.
Masa;
Toka upate internet access basi mgogoro!.
Sio lazima uandike au useme hata kama unaruhusiwa kisheria kuandika au kusema, kabla ya kuandika au kusema lazima upime unataka kuandika au kusema nini!
I think this applies to you as well....! Nashindwa jua IQ za wengine hapa!