CCM Kahama kumsaidia JK kupambana na rushwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,293
33,078
JK%288%29.jpg

Rais, Jakaya Kikwete.



[FONT=ArialMT, sans-serif]Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, kimetangaza rasmi uamuzi wake wa kumsaidia kwa hali na mali Rais Jakaya Kikwete katika juhudi zake za kupambana na rushwa nchini. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Tamko hilo lilitolewa na Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya hiyo katika kikao chake maalum, kilichofanyika mjini Kahama Jumapili ya wiki iliyopita, kwa ajili ya kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea uongozi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, unaotarajia kufanyika nchini kote, Oktoba 25, mwaka huu. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kikao hicho kilifanyika chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo, Andrew Masanje na kilihudhuriwa na wajumbe zaidi ya 100 kutoka majimbo yote mawili ya uchaguzi wilayani humo; Jimbo la Kahama na Msalala. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa mujibu wa taarifa ya halmashauri hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari kupitia mtandao wa kompyuta wiki hii, azimio la kumuunga mkono Rais Kikwete, lilitokana na kuonyesha kwake dhamira ya dhati kupambana na rushwa nchini. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Halmashauri hiyo pia, imesifia hatua ya Rais KIkwete ya kubuni utaratibu wa kujibu na kusikiliza hoja za wananchi moja wa moja kupitia vyombo vya habari, hatua ambayo ilisema imeudhihirishia umma wa Watanzania na ulimwengu kwa jumla kwamba, serikali anayoiongoza ni ya ukweli na uwazi. [/FONT]
“[FONT=ArialMT, sans-serif]Chachu ya kutoa tamko la kumuunga mkono Rais ilitokana na jibu lake alilolitoa kwa mwananchi mmoja aliyetaka kujua ukweli juu ya madai ya baadhi ya watu kuwa, yeye Rais na chama chake Cha Mapinduzi ni swaiba wa karibu wa mafisadi, ambapo rais alitamka bayana kuwa “hakuna urafiki au undugu kwenye vita dhidi ya rushwa, wataendelea kuumbuliwa na kupelekwa kwenye vyombo vya dola,” ilieleza. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Iliongeza: “Wajumbe walitabanahisha kuwa kauli hiyo ya Mwenyekiti wa CCM ambaye ndiye kiongozi mkuu wa chama “ndiyo dira na kauli ya chama” na kwamba rais hataachwa peke yake katika mapambano dhidi ya vita hii kubwa na ya kihistoria nchini mwetu”. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Aidha, halmashauri ilitambua na kupongeza uwepo wa wabunge wa CCM ndani ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wakiwemo na wale wa mkoa wa Shinyanga, walio mstari wa mbele katika kukemea ufisadi na kutetea maslahi ya Watanzania. Wajumbe walisema ‘wabunge hawa wamekuwa msaada mkubwa kwa Rais na serikali ya awamu ya nne ya CCM. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Katika kikao hicho, halmashauri pia, iliunga mkono kwa kauli moja adhabu ya kifo iliyotolewa dhidi ya watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya mlemavu wa ngozi (Albino), marehemu Matatizo Dunia (13) aliyeuawa kikatili mwaka jana katika kijiji cha Mnyihuma, wilayani Bukombe. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Ilipongeza hukumu hiyo iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakabalila wa Mahakama Kuu ya Tanzania kwenye kikao chake maalum mjini Kahama juma lililopita, ikiwahusisha watuhumimwa Masumbuko Madata (32), Emmanuel kalamuji Masangwa (28), na kaka yake Charles Kalamuji Masangwa (42). [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kikao hicho cha halmashauri kilipongeza jinsi mahakama ilivyoendesha kwa makini usikilizaji wa kesi hiyo na kueleza kuwa ulikuwa wa uwazi mkubwa, na wa kuondoa shaka zote, ambazo zilianza kuvuma hapo awali kuwa, kesi hizo za mauaji ya albino zimegubikwa na mianya ya rushwa [/FONT]




CHANZO: NIPASHE JUMAPILI


http://www.ippmedia.com/
 
Back
Top Bottom