CCM itatawala nchi kwa karne nzima

Udhaifu uliopo kwenye vyama vya Upinzani ndio utafanya CCM itawale karne nyingi.
Huwezi kufanya kampeni kwa kutafuta kura za huruma. Mie binafsi naamini na mapungufu ya CCM kwasasa Tanzania hakuna chama mbadala ambacho kinafaa kupewa madaraka
 
Karne nzima itamtawala nani wakati rais watakuwa wamekwisha kwa kupigwa risasi Na kutekwa.
 
Mwanaume kabisa unaandika mada kama hii?
 
mmmh.mzee hapo kwenye damu mtihani.
napenda nchi ifate sheria,miongozo na taratibu tulizojiwekea.lakini si kwa kushika mapanga.
ni kuamua tu kuisimamisha demokrasia na tuifate.
na kikubwa upinzani usichukuliwe kama ni uadui.
wote lengo letu ni kuijenga Tanzania.
tushirikiane.tukosoane.pia turekebishane pale tunapoona mambo hayaendi sawa.NEC NAO WATENDE HAKI
 
Ni vibaya sana kuishi kwa kubahatisha...nidhambi na niaibu kwani tumejaaliwa akili. Leo upinzani unagombea huku ukijua kwanza madarakani yupo mwenye chuki kuu nao na hataki kuwaona. Pili,usimamizi wote wa uchaguzi uko chini ya huyo anayewachukia. Wapinzani wangepaswa kudai katiba bora itayoleta usawa katika demokrasia. Leo hii huwezi laumu tena diwani ama mbunge anayehamia CCM kwani kimsingi ndiyo wenye nchi.
Yatupasa tuangalie kama kuna umuhimu tena wa hii demokrasia yakibabe na kibaguzi,twaweza ingia gharama kuubwa kufanya maigizo yakitoto na siasa za kiwendawazimu. Nikisikia tena wapinzani wanagombea mahali kwa mifumo na katiba hii nitawaona wasiokuwa na akili timamu.
 
Udhaifu uliopo kwenye vyama vya Upinzani ndio utafanya CCM itawale karne nyingi.
Huwezi kufanya kampeni kwa kutafuta kura za huruma. Mie binafsi naamini na mapungufu ya CCM kwasasa Tanzania hakuna chama mbadala ambacho kinafaa kupewa madaraka
mkuu kwani CCM kuongoza miaka yote NI KOSA?
tatizo linakuja wanaongoza vipi nchi.
KAMA WANANCHI WANAIKUBALI CCM NA KUIPENDA HATUWEZI TUKASEMA NI UJINGA.SI WANAKUBALIKA.
TATITO NI UDANGANYIFU KWENYE CHAGUZI NA KUIBA KURA.
kama CCM wakishinda kwa haki.
sisi upinzani hatutakuwa na neno si wananchi wameamua.waongozwe na CCM.kwani kuna ugomvi?
TATIZO WIZI WA KURA.
 
Watanzania sio waoga..ila WANAFIKI..Wanauwa mwizi Wa simu fisadi anachekewa
 
Hawatatenda kama unavyofikiri hata siku moja. Omba uhai
 

kwamaneno kuna njia nyingi zakuitoa ccm, kwa vitendo hakuna

kuitoa ccm ni sawa na kutoa vyombo vya usalama vyote, fikiri kama inawezekana
 
Hawatatenda kama unavyofikiri hata siku moja. Omba uhai
naamini demokrasia ya Zimbabwe na SA.IPO siku itafika kwetu.
siasa sio uadui.
SIO MPAKA TUUANE NDO TUONEKANE TUNATAKA KUIJENGA NCHI YETU.
kikubwa NEC huru.
MTU ashinde na kushindwa kihalali.
ugumu unatoka wapi?
 
Kwanini unataka kupigana na Polisi?

Polisi wanapiga kura?

Tatizo lako lipo ktk box la kura

Wapo wanaoipigia kura CCM na ni wengi.

Huwezi kushinda uchaguzi kwa kupigana na Polisi.
Nani anapigana na Polisi. Polisi ndio wanatumiwa na CCM. POLE
 
Pamoja na ujinga lakini kete kubwa ya CCM kutawala ni mabavu. Kutumia vyombo vya dola kujipa ushindi
 
naamini demokrasia ya Zimbabwe na SA.IPO siku itafika kwetu.
siasa sio uadui.
SIO MPAKA TUUANE NDO TUONEKANE TUNATAKA KUIJENGA NCHI YETU.
kikubwa NEC huru.
MTU ashinde na kushindwa kihalali.
ugumu unatoka wapi?
Si rahisi kwa ccm hawa kuachia Tume huru ya uchaguzi pna katiba itakayotoa fair kwa wapinzani wao[emoji40] [emoji23] [emoji12] !!
 
Nonsense ! Hawa wadanganyika watakapoamka kutoka usingizi wa pono na ganzi ya mwenge it will be impossible for CCM kutawala it’s just a natural law! The communist party of the then Soviet Union refused to reform matokeo yake it ruled for 70 years and it’s now distinct na hata CCM ikikaribia 70 it’s now 64 itasambaratika na makaburi ya waanzilishi yatafukuliwa na kubomolewa and itakuwa kilio na kusaga meno kwa watoto wa viongozi and they shall have no where to hide!
 
Hivi mnahamasishana kuanza kupigana na serikali! Mmechoka na amani?
 
Nakubaliana na wewe 100%. Na wanaoongoza kwa uoga ni wasomi. Intellectual prostitution.
 
Tatizo sio kutawala Karne au karne mbili. Tatizo jee itatuletea yale maendeleo tunayoyatarajia wengi?
 

Nyani Ngabu, Watanzania siyo waoga, ila Watanzania wengi hawajui haki zao na pia bado hawajafahamu kiundani kabisa maamuzi ya kisiasa yana athahri gani katika maisha yao, Wengi wanaichukulia Siasa kama mchezo wa kishabiki tu kama mpira wa Simba na Yanga kwa hiyo hawako tayari kusimama kidete katika mambo ya siasa kama vile demokrasia etc

Ila sasa polepole tunapokwenda, Elimu ya uraia inaongezeka , watu wengi sana watafahamu mwanasiasa na siasa zake zinamuathiri yeye mwananchi katika maisha yake, Watu watajua haki zao, Wakishazijua vizuri kabisa, na wakatambua maamuzi ya kisiasa yanawaumizaje basi Hii dhana ya Uoga wa Watanzania utashangaa kuwa siyo kweli!.

Kwa hiyo ni suala la Elimu tu (Education), Watanzania walio wengi siku Wakielimika ipasavyo juu ya haki zao za kikatiba, lakini pia wakielimika kwa kufahamu dhahiri kuwa Maamuzi ya kisiasa yanagusa moja kwa moja maisha yake na ya familia yake, Ogopa brother, things will never be the same again.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…