CCM itatawala nchi kwa karne nzima

CCM itatawala nchi kwa karne nzima

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
97,115
Reaction score
136,839
Baadhi ya watu, nikiwemo mimi, tumekuwa tukiamini kuwa mtaji mkubwa wa CCM katika ushindani wa kisiasa nchini ni ujinga wa wananchi.

Kwamba, kuna sehemu kubwa ya wananchi ambao ni wajinga ama kwa kutokutaka au kupenda kufuatilia mambo vizuri au kwa kuwa na uwezo mdogo wa kuchanganua mambo na hivyo kupelekea kurubuniwa na CCM pindi msimu wa uchaguzi unapokaribia ili wakipe kura chama hicho.

Tumekuwa tukiiamini sana nadharia hiyo kwa sababu tunaamini kuwa ni vigumu sana kwa mtu na akili zake timamu kuendelea kuiunga mkono CCM licha ya uborongaji wake.

Lakini, mimi binafsi nadhani mtaji wa kisiasa wa CCM si ujinga peke yake. Naamini pia uoga wa Watanzania nao ni bonge la mtaji kwao.

Sisi Watanzania ni waoga sana. Tunaogopa mno dola. Tukisikia tu polisi au jeshi, basi tunaanza kutetemeka.

Nyakati zingine huwa nikiangalia jinsi ambavyo watu wa mataifa mengine wanavyopambana na polisi huwa nabaki mdomo wazi.

Unakuta waandamanaji wanazipiga na polisi katikati ya barabara. Tena hawaogopi kabisa. Sasa mambo kama hayo hapa kwetu sidhani kama yanaweza kutokea. Na ndo maana huwa tukitishwa kidogo tu tunaogopa.

Hatuna kabisa ujasiri wa kuidindia serikali. Hatuna ujasiri wa kupigana na ma askari polisi kama wafanyavyo watu wa mataifa mengine.

Uoga wetu huu ndo unanifanya niamini kuwa CCM inaweza kutawala nchi hata kwa zaidi ya karne nzima.

Je, uoga tulionao nao ni sehemu ya ndivyo tulivyo ama?
 
Ukitaka kupima kiwango cha ujinga nenda mkoa wa dodoma utakubali jinsi tanzania hii inahitaji miujiza ili kuondoa ccm....chukulia jinsi wale watafiti wa kilimo walivyouawa kule dodoma kwa kuitwa wanyonya damu!!!!
Pia ccm wanajitahidi kuwapindua wananchi kwa kuwapa BORA ELIMU ilimradi watie ujinga vichwani
 
Hivi ujinga nao unaweza kupelekea mtu akawa muoga pia?
 
CCM si chama cha siasa, na kama kuna mtu ana amini hivyo atakuwa hajielewi... CCM is more of a state apparatus just like the rest..Police , etc...
Kupigana si hoja, hoja mtapigana hadi iweje... Mapinduzi?
Maana consequences za kupigana na dola ujiandae kisaikolojia kutupwa mabwepande, risasi za mchana kweupe na mengine mengi..
Siasa za CCM na za Urusi (United Russia) zinafanana sana....
KGB=TISS.

Mwalimu alikuwa muoga sana, akaishikamanisha CCM na Dolla(Japo alikuja gundua kosa hilo badae), im afraid kuitoa CCM madarakani itagharimu maisha ya wengi....

BTW hakuna haja ya kupigana na police kwa malengo mafupi ya ubunge au udiwani....(It must be something bigger and better than that)
 
Ila mzee wewe binafsi utakubali kutoka uiache familia yako uende ukapambane na hao askari jeshi kama wenzetu wanavyofanya?maana haiyumkiniki kila mtu humu kujificha nyuma ya keyboard na kuanza kutoa ushauri namna bora ya kupambana na chama dola kisha yeye asiwepo ktk kundi.
 
Nimesema sisi Watanzania ni waoga.
 
kweli lakini naamini hata mtu muoga kuna siku ataamka. nsomba uisikilize nyimbo ya " coward of the county" ya kenn rogers utaelewa ninachomaanisha.
 
Yes! Woga pia ni tatizo kubwa linalochangia CCm kuwepo madarakani hadi leo. Sijui chanzo cha huu woga ni nini. Naamini hakuna nchi yenye raia waoga kama Tanzania. Ni kama laana.
 
Ukitaka kupima kiwango cha ujinga nenda mkoa wa dodoma utakubali jinsi tanzania hii inahitaji miujiza ili kuondoa ccm....chukulia jinsi wale watafiti wa kilimo walivyouawa kule dodoma kwa kuitwa wanyonya damu!!!!
Pia ccm wanajitahidi kuwapindua wananchi kwa kuwapa BORA ELIMU ilimradi watie ujinga vichwani
daaah aisee.kweli hii nchi ujinga ni mzigo
 
Chadema ilipopata fursa ya kukamata dola ikatuletea fisadi na hivyo watu wakaamua kwa dhati na kiakili mno kuwa ni lazima waibakishe CCM.

Kwa mantiki hii CCM lazima itawale milele !

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
hapa tunajadili ujinga wa watanzania kuikumbatia ccm siyo chadema. fungua topiki yako inayohusu chadema tutakuja kuchangia
 
Hata hizo nchi unazozisifia kwamba sio waoga, walianza taratibu, na kuna vitu vilipelekea wakafikia hiyo hatua.
Naamini hata hapa kwetu kama hivyo vitu viliyopelekea watu wakapoteza uoga vikiendelea, woga utaisha na usishangae yakatokea kama yanayoendelea mataifa mengine.

Lakini kwanini uoga uangaliwe kwenye eneo moja tu la kupambana hasa kupigana na polisi au vyombo vya dola? CCM inaweza kutolewa madarakani kwa njia nyingi tu bila hata kupambana na polisi kwa mabavu.
 
Iko siku haya yana mwusho kuba kipindi kitafika na uvumivu utakuwa ni mwisho
 
Back
Top Bottom