CCM itaendelea kupata upweke na kuendelea kumpa Lissu nguvu kutokana na kushindwa kutoa Empirical Evidence juu ya shambulio la Lissu

Mk54

JF-Expert Member
Dec 29, 2016
1,997
3,933
Ukifuatilia mikutano ya JPM na TL utagundua there is a strong dark energy flowing between these two.

IMG_2697.jpg
Na hiyo dark energy inaweza kuleta madhara makubwa sana kwa Taifa letu Teule la Tanzania, Taifa pekee hapa duniani lililoondosha Corona kwa Maombi tu.

====

Kimsingi Tundu Lissu ni mdogo sana kwa JPM kwa zaidi ya miaka 8, hivyo hakuna uwezekano wowote hawa wawili hawapatani kwa sababu wamekaribiana umri. In fact , Tundu Lissu akikutana na JPM leo, anatakiwa kusalimia. Yaani Shikamoo.

>>>>>>>>>Hata hivyo, Tundu Lissu amekuwa akimshambulia sana JPM na hakubaliani kabisa na style ya uongozi wa JPM from day one huku akiamini kwamba JPM hana Fundamental Characters Ethics za kuwa Rais wa JMT.

Halikadhalika, TL anaamini kwamba JPM ni mbinafsi na anatumia madaraka yake kunufaisha kijijini kwao, kijiji ambacho huenda kikawa ni makazi ya popo baada yake. Kadhalika , TL amekuwa akimnanga JPM kuwa hata kiswahili hajui achilia mbali Englishi , kwamba havutii hata kumsikiliza, na kusema kwamba, kama anabisha basi aje kwenye Mdahalo nae.

Kwa kauli tajwa hapo juu , ni dhahiri kwamba this is more than politics, huenda wengi wakawa wanafurahi tu wakiamini ndio siasa na kumekucha juu ya Kampeni.

===

JPM ameendelea kuamini na kutuaminisha kwamba TL ni MNAZI anayetumika na wazungu kuliharibu taifa la TZ.

IMG_2698.jpg

Katika utawala wa JPM, ukisikia neno BEBERU, basi jua huyu ni Tundu Lissu. Lakini ni TL huyu huyu aliyekuwepo kwenye utawala wa JK, kwanini neno BEBERU halikutumika dhidi yake?
===
Ni ugomvi binafsi ambao mimi na wewe hatujui sababu ya ugomvi huo, ila hakika ya bayana ni kwamba kuna ugomvi mkubwa baina ya wawili hawa na ugomvi huo umehusisha mpaka vyombo vya ulinzi na usalama na kuufanya kuwa ni ugomvi wa mtu mmoja dhidi Serikali.

Kwamba tunaambiwa mtu 1 anatumika na BEBERU kuharibu nchi yetu. Hii imeshakuwa ni Imani kwa Tanzania.

People believe what they wanna believe!
===
Moja ya kitu ambacho Serikali yangu ya Chama Cha Magufuli (CCM) itaendelea kupata upweke na kuendelea kumpa TL nguvu ambayo inaweza kutuletea shida na kumpa DOA JPM ni kushindwa kutoa Empirical Evidence juu ya shambulio la Lissu( Kijana wa Kisingida)

Shambulio hilo ndio siri ya umaarufu wa kijana huyu wa ki Singida ambae amekuwa akitumia Shambulio hilo kama fimbo ya kutuchapia kwenye vichwa vyetu.

Amepata HURUMA kubwa ya wananchi kila anapoenda huku akizidi kuwaaminisha wananchi kwamba the Assassination attempt was an inside job.

Sidhani kama Serikali na Chama Cha Magufuli( CCM) kimefikiria kwa MAPANA mustakabali wa hiki kinachoendelezwa na TL....
Hili Gap la kutowawajibisha wahusika Litazamwe kwa mapana. -------linaweza kutumiwa vibaya na watu wasiojulikana na kuzidi kuchafua hali ya Hewa.

Hivyo basi, vyombo vyetu vya ulinzi na usalama hasa TISS ambao wamekuwa wakishukiwa sana kwenye matukio kama haya visafishwe ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa mujibu wa maagizo yenye weledi.

Hakuna watu wanaofanya kazi kwa Upendo na Nidhamu kama TISS ambapo moja ya mafunzo ni kuimarisha unyenyekevu na mapenzi yenye huruma baina ya mtu na mtu.
===
Kwa Hitimisho, ni nani Tundu Antiphas M Lissu?

What is Tundu, what is Lissu in his own Language?

Is he the only person among the family members using tribal names?

What is Antiphas ? What is Mughwai?

Tundu Antiphas Mughwai Lissu

Je, ni mwana wa Mungu aliyeshinda Mauti au

ni Mjumbe wa Kimila aliyechanjia na kunuia juu ya kifo


>>Kwamba Kifo changu hakitosababishwa na Risasi,
>>kwamba Kifo changu hakitosababishwa na Bomu ,
>>Kwamba Kifo changu hakitosababishwa na ajali
>>Kwamba atakayejaribu kuniua kwa mara ya pili, kwa nuio hili atatangulia yeye kwanza kabla ya mimi kushinda Umauti kwa mara ya pili na mara nyingine tena for as long as death is a shame, a bread of a shame.
 
..kimsingi serikali ya jpm imeshindwa kuueleza umma juu hasa ya nan alikiwa nyuma ya shambulio lile...lissu ana kitu ndan yake ambacho Mungu anataka kumtumia kwa ajili ya taifa lake..16 bullets but still alive lazima uogope huyu mtu ni nani...na bado ana guts za kusema na kukosoa kwa uwazi....
 
..kimsingi serikali ya jpm imeshindwa kuueleza umma juu hasa ya nan alikiwa nyuma ya shambulio lile...lissu ana kitu ndan yake ambacho Mungu anataka kumtumia kwa ajili ya taifa lake..16 bullets but still alive lazima uogope huyu mtu ni nani...na bado ana guts za kusema na kukosoa kwa uwazi....

Yah that is one side, the other side may be not God
 
Kwani kuna mtu ambaye si mwana wa zMungu hapa duniani?
Biblia inasema tumeumbwa kwa mfano wake!

Kwahiyo Wewe ni mwana wa Mungu ? Why do you have to say Biblia imesema...., kama Biblia isingesema wewe ungekuwa ni Mwana wa nani ?
 
Kumnyima matibabu na kumvua ubunge ule ulikua ni ukatili usio na maelezo.

Na hapa ndio uwazi Ambao TL anautumia kuamikisha umma kwamba , the whole issue was an inside Job.

Nadhani Serikali yangu inatakiwa kuziba hili pengo before its too late. Huyu Kijana wa Kisingida is very much talkative. He will never get out of it . Mikutano yake yote lazima atumie huu uwazi
 
hapanaa

Ki imani tunasema ameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu

Mungu anasura gani ? Na je anamfano gani ?

Tuoneshe hiyo sura yake ili tujue mfano wake juu yetu . Thanks
 
Ukimya wa vyombo vya Dola juu ya shambulio la risasidhidi ya Tundu Lissu, lina kamilisha 100% kuwa mhusika ni Jiwe, ndiye aliewatuma kienyeji wauaji!

Hili bado halijathibitika beyond the reasonable doubt ; but ukimya wa vyombo vya Dola unachochea dhana kwamba the issue was an inside Job na ni uwazi unaotumika na TL.

Ni lazima vyombo vya Dola vijiweke kando na huu uzushi . And the only way ni kutoa taarifa Rasmi ya wale wote waliojaribu kufanya hivyo huku wakifikishwa mahakaman.

Kutuaminisha TL kuwa bado anakesi ya kujibu huku ametoka kupigania maisha yake ni muendelezo wa chuki na visasi utakaokuja kutuletea vurugu za kisiasa.

Aidha, uchaguzi wa mwaka huu serikali uwe nao makini sana. Kuna visasi na chuki ndani yake na ifahamike maadui pia hawapo mbali kuchochea kuni. Tuna hitaji hekima sana
 
Inaelekea hujui uliloandika Chief!
TAL hawezi kumwa Mwana wa Mungu (Son of God), never!
Yeye ni Mwana wa Adam ( Son of Man).
Zaidi ya hapo utakuwa unakufuru.

Kwanini TAL hawezi kuwa mwana wa Mungu?

Nini maana ya tafsiri ya Mwana wa Mungu ?
 
uzi ni mzuri na una mazingatio makubwa sana. ila sahihisha heading na oundoe neno Mwana wa Mungu. Bora Uandike " Je Tundu lisu ameletwa na Mungu kutukomboa Wa Tanzania?" n.k ila usiweke Mwana wa Mungu sio sahihi

Unaweza kuthibitisha ni kweli ameletwa na Mungu kutukomboa ? Maana mm nimeuliza swali je ni mwana wa Mungu ? Labda tuanze tafsiri ya neno mwana wa Mungu
 
Mmeshasahau Dr. Slaa mlimpamba hivyo hivyo kuliko St. Paul!

Tundu Lissu nae tutamnunua tu. Kwanza ana njaa sana muda huu. Na yeye atapewa Ubalozi. Ataacha kelele zote. Enzi ya JK walikuwa wanapewa sana Bahasha za kaki hawa watu; utawala huu hawatoi tena Bahasha za kaki
 
Back
Top Bottom