CCM ingeshinda kama Raisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM ingeshinda kama Raisi

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by mbongopopo, Apr 2, 2012.

 1. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Angesikiliza maneno ya watu juu ya aibu mbunge Lusinde aliyoyafanya kwa kuongea maneno machafu kwenye kampeni.

  Angemuomba Lusinde ajiuzulu. Na bado hajachelewa kama anapenda chama chake kiendelee

  Angemsimamisha kazi mara moja bila kusita.

  Kwa kweli sidhani kama nchi zingine wanatukana na kutumia lugha mbaya hivi mbele ya wananchi. Huyu mtu anazo kweli yaani namfikiria tangu siku hiyo sipati majibu.

  Na sijui Mkapa walimrudisha kufanya nini jukwaani akiwa ameshaharibu mwanzoni. Hawa watu. Wana washauri kweli au?
   
 2. P

  Panda Kapesi JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 284
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 60
  Unajua umenichokonoa wazo
  Mie nadhani hawa wabunge wafanyiwe mental checkup kabla ya kukabidhiwa ofisi maana ni dhahiri kabisa kuwa huyu Lusinde ana matatizo makubwa ya akili na badala ya kumlaani tu inabidi jitihada zifamnyike asaidiwe huduma ya hospitali. Si kawaida kabisa na sijawahi kuona mwakilishi wa watu akijidhalilisha kwa kutapika maneno machafu kiasi kile kwenye halaiki ya watu wenye rika na umri mbalimbali ikiwa na watoto chini ya miaka 18. Kama ikionekana kuwa alikuwa na akili zake timamu na alifanya kwa dhamira yake basi ni lazima awajibishwe na vyombo vya dola kwa kushitakiwa mahakamani. Lakini kwa jinsi vyombo vya dola vilivyokaliwa na wanasiasa wa CCM ni vigumu sana kutegemea lolote kufanyika kumwajibisha huyu mtu itabidi makundi ya wanaharakati au walengwa wa matusi yale kumshitaki huyu mtu. nawaonea huruma sana watu wa jimbo analoliwakilisha huyu mtu kwa kweli amewatia aibu sana watu wa |Mtera na Chama chake cha Magamba maana kuna ile methali isemayo "samaki akioza mmoja................"
   
 3. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Halafu hakuna hata mwana ccm hao wa juu kusaidia kutetea hata kidogo inamaanisha na wao wanaona ni sawa tu yaliyotokea...kuna tatizo kubwa ccm.
   
 4. P

  Panda Kapesi JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 284
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 60
  Unajua umenichokonoa wazo
  Mie nadhani hawa wabunge wafanyiwe mental checkup kabla ya kukabidhiwa ofisi maana ni dhahiri kabisa kuwa huyu Lusinde ana matatizo makubwa ya akili na badala ya kumlaani tu inabidi jitihada zifamnyike asaidiwe huduma ya hospitali. Si kawaida kabisa na sijawahi kuona mwakilishi wa watu akijidhalilisha kwa kutapika maneno machafu kiasi kile kwenye halaiki ya watu wenye rika na umri mbalimbali ikiwa na watoto chini ya miaka 18. Kama ikionekana kuwa alikuwa na akili zake timamu na alifanya kwa dhamira yake basi ni lazima awajibishwe na vyombo vya dola kwa kushitakiwa mahakamani. Lakini kwa jinsi vyombo vya dola vilivyokaliwa na wanasiasa wa CCM ni vigumu sana kutegemea lolote kufanyika kumwajibisha huyu mtu itabidi makundi ya wanaharakati au walengwa wa matusi yale kumshitaki huyu mtu. nawaonea huruma sana watu wa jimbo analoliwakilisha huyu mtu kwa kweli amewatia aibu sana watu wa |Mtera na Chama chake cha Magamba maana kuna ile methali isemayo "samaki akioza mmoja................"
   
 5. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Comrade watu wa arumeru hawakutazama kipara cha mkapa wala mikwara ya wanamagamba,Lowasa anataka kujifunza jins ya kuwatengeneza viongozi namkumbusha kwamba kazi hiyo ni ya Mungu na wale wachungji na maaskofu anaowatumia wote ni wapangaji tu wa Mungu leo wapo kesho anawatoa.
   
Loading...