Napenda kuchukua fursa hii kuwajulisha CCM kwamba anayeweza kukinusuru Chama katika chaguzi zijazo ni Mh. Lowasa. Nayasema haya kwa kuwa chama kimekosa mtendaji na ndani ya chama mtendaji anayeonekana na kukubaliwa na wengi ni Lowasa. Ikumbukwe kuwa zao la vijana waliomaliza vyuo vikuu Tanzania kuanzia mwaka jana wengi wamesoma shule za kata ambazo mwasisi wake ni Lowasa, na wengi wapo tayari kwake. Vijana hawana ajira hatima yake wanajifanya wasanii na kutumikishwa na watu kubeba madawa ya kulevya na kwenye madanguro. CCM lazima impe nafasi Mh. LOWASA ili aweze wafikisha vijana wengi ambao hawana ajira kwenye ndoto zao maana alishawajengea msingi wa elimu hatokubali wapotee. Tafakari Mtanzania.