CCM inaweza kulinda ardhi ya wanyonge Dodoma?

Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
3,434
1,985
Kabla na baada ya ujio wa makao makuu ya nchi na kupandishwa hadhi ya Dodoma kuwa jiji, ulanguzi wa ardhi ya wenyeji wa mkoa huu unahatarisha maendeleo ya watu hao sasa na siku za usoni ikiwa mambo yataachwa yaendelee kama yalivyo.

Ili kudhihirisha hoja hii ni mfano wa kinachoendelea hivi sasa Africa ya Kusini (land reform) ambako inasemekana 70% ya ardhi yenye rutuba inamilikiwa na wazungu ambao ni kama asilimia 20 ya raia wote wa SA.

Dalili zinaonyesha kuwa baada ya muda Wagogo nao watabaki na maeneo machache tu ya ardhi mbali na mji, kusiko na rutuba wala malisho ya mifugo.
Ni dalili gani hizo? Hizi ni baadhi tu:

1. Kumezwa kwa makao makuu ya Mkoa wa Dodoma ambayo sasa ni makao makuu ya Nchi.

2. Uuzaji na nunuzi wa viwanja, mashamba maeneo ya ndani na nje ya mji mpaka vijijini usiozingatia maslahi ya sasa na ya baadae ya pande mbili husika. ("win-win situation").

3. Ombwe la sera na uongozi wenye maono miongoni mwa watawala na watawaliwa wenyeji na wageni.

4. Siasa za unafiki, wivu, ubaguzi, uchoyo, fitina na ukandamizi.

5. Kinachoonekana Kama udhaifu wa wenzetu hawa Wagogo kama walivyoonekana waafrika enzi za ukoloni hapa nchini mwetu na kule South Africa.
 
Kabla na baada ya ujio wa makao makuu ya nchi na kupandishwa hadhi ya Dodoma kuwa jiji, ulanguzi wa ardhi ya wenyeji wa mkoa huu unahatarisha maendeleo ya watu hao sasa na siku za usoni ikiwa mambo yataachwa yaendelee kama yalivyo. Ili kudhihirisha hoja hii ni mfano wa kinachoendelea hivi sasa Africa ya Kusini (land reform) ambako inasemekana 70% ya ardhi yenye rutuba inamilikiwa na wazungu ambao ni kama asilimia 20 ya raia wote wa SA.
Dalili zinaonyesha kuwa baada ya muda Wagogo nao watabaki na maeneo machache tu ya ardhi mbali na mji, kusiko na rutuba wala malisho ya mifugo.
Ni dalili gani hizo? Hizi ni baadhi tu:
1. Kumezwa kwa makao makuu ya Mkoa wa Dodoma ambayo sasa ni makao makuu ya Nchi.
2. Uuzaji na nunuzi wa viwanja, mashamba maeneo ya ndani na nje ya mji mpaka vijijini usiozingatia maslahi ya sasa na ya baadae ya pande mbili husika. ("win-win situation").
3. Ombwe la sera na uongozi wenye maono miongoni mwa watawala na watawaliwa wenyeji na wageni.
4. Siasa za unafiki, wivu, ubaguzi, uchoyo, fitina na ukandamizi.
5. Kinachoonekana Kama udhaifu wa wenzetu hawa Wagogo kama walivyoonekana waafrika enzi za ukoloni hapa nchini mwetu na kule South Africa.
Wagogo? Wacha waendelee kufanywa manamba maana wao nu kimbelembele sana kuisapoti ccm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom