KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,601
Tumeshuhudia mara nyingi kila CCM inaposhinda lawama zote ni kwa tume ya taifa ya uchaguzi hususani wasimamizi wa uchaguzi ngazi za majimbo ambao ni wakurugenzi. Lawama hizi hazina ukweli kulingana na uhalisia. Uhalisia unaendana na mchakato mzima wa uchaguzi. Mchakato mzima wa uchaguzi kuanzia kupiga kura mpaka utangazwaji matokeo upo wazi, ni ngumu kwa mkurugenzi kushiriki wizi wa kura kwa sababu rufaa ya matokeo inaweza kukatwa.
Hofu waliyokuwa nayo wapinzani ni kuwa na mchecheto mkubwa wa kujua matokeo ilhali zoezi la uhesabuji kura na taratibu nyingine zikiwa zinaendelea na hivyo kuwa na hisia kuwa zoezi linacheleweshwa kutokana na kuchakachua matokeo. Moja ya sifa kubwa ya mshindani ni kukubali kushindwa na sio kulazimisha ushindi. Sifa hii wapinzani hawana.
Kimsingi wakurugenzi ni watangazaji tu wa matokeo ambayo yamejumlishwa na kuthibitishwa na mawakala wa vyama vyote. Kama ni lawama, vyama vya upinzani ni bora ikawalaumu mawakala wao na si tume ya taifa ya uchaguzi na wakurugenzi ambao ni wasimamizi wa uchaguzi ngazi za majimbo.
Kwa hiyo, kwa kuangazia mchakato huo kwa ufupi, naomba nikiri kusema kuwa CCM inatafuta ushindi na haipewi ushindi. Ushuhuda ni shamrashamra za kampeni na kuangazia wingi wa wanachama wake. Wanachama Zaidi ya million 12 wa CCM, wakati wa kampeni wanalengo moja tu nalo ni kusaka, kutafuta na kuleta ushindi kwa CCM
CCM inashinda kwa sababu inagharamia ushindi. CCM inagharamia ushindi kwa kuzunguka kila kijiji wakati wa kampeni wakijinadi na kuinadi ilani ya chama. Watanzania wanakubaliana na ilani yenye mipango na mikakati mizuri ya kuwakomboa kiuchumi na kuipigia kura tena na tena.
Ushindi ni gharama. Kuna vyama vingine vinaona CCM inashinda bila kugharamia ushindi huo kwa maana ya kwmba inapewa ushindi wa mezani na wakurugenzi. Mawazo kama hayo ndio yanayofanya upinzani kudai ushindi hata kama wameshindwa, nawahakikishia anguko lenu lipo karibu. Hamuwezi kushiriki mbio ndefu bila kuhakisha uimara wa afya na miguu yenu na imethibitika afya zenu haziruhusu kushiriki mbio hizo.