CCM inang'olewa na wakati na sio UKAWA wala Lowassa

Kionambele

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
236
Reaction score
93
Kwa kifupi tu kumbukeni kejeli na kubeza kulikofanywa na kunguru wa mabadiliko wakati wa mijadala ya kuanzisha mfumo wa vyama vingi nchini. Kura zikapigwa, tukaambiwa asilimia 80 wamechagua chama kimoja. Lakini wakati ukashinda, maana wakati ulichagua vyama vingi.

Nelson Mandela ambaye alikuwa mfungwa kwa miaka zaidi ya 20 lakini wakati ulipofika alikuwa Rais wa kwanza wa Afrika Kusini mpya.

Kanali Muamar Gaddafi alikuwa kiongozi aliyeleta maendeleo ya hali ya juu kwa ustawi wa jamii ya watu wa Libya na Afrika kwa ujumla. Alifikia mahala pa kudhaniwa kuwa angekuwa Rais wa Afrika endapo Afrika ingeungana na kuwa moja. Alikuwa na ndoto ya kuleta umoja wa kweli katika Afrika.

Huyu jamaa alishindana na kupigana na wakati. Mwisho wake mnaujua vema.

Huu ni wakati wa mabadiliko Tanzania. Na sio mabadiliko wanayoyasema CCM na uongo wao wa kudanganya wapiga kura wenye ukunguru wa mabadiliko eti wananchi hawataki mabadiliko ya chama, mabadiliko tunayoyataka yanaanza na chama kilichopo madarakani kung'oka kwanza.

Huu ni wakati wa CCM kung'oka. Mabadiliko ya kweli ni CCM kung'oka kwanza na mjadala mwingine utafuata.

Subirini mjionee nyinyi mnaodhani CCM ni mungu wenu. Angalieni mjionee kama CCM inaweza kushindana na wakati.

Jiulizeni kwa nini Magufuli badala ya kuinadi CCM anajinadi yeye mwenyewe!!!!! Anajua CCM ni lazima ing'oke, anatamani angegombea kwingineko.
 
umeanza vizuri ila umemalizia kwa pumba kama wapinzani wangekuwa makini walikuwa wanaiondoa ccm mwaka 2025 lakini kitendo chao cha kutumia mafisadi ndio wamechemka inabidi waanze tena mwanzo itachukua muda mrefu kwani wamewapa nafasi ccm ya kujitazama upya
 
Naona Kama Umelala Usingizi Vile, Na Kuota Ndoto Za Abunwasi! Ccm Mwaka Huu Halita Salia Jiwe Juu Ya Jiwe, OUT.
 
Tatizo lenu mnaota ndota za mchana kweupe, nashindwa kuwaelewa wanamageuzi, mbona mnajichanganya sana hivo? Kama mda ulikuwa umefika basi ni wazi kwamba mmekosea masharti, na ulipokosea jitahidi kijisahihisha mapema, ila kwa kuwa macho yenu yamefunikwa na ukungu mkubwa, itakuwa kazi sana ccm kuondoka kwa wakati huu, hii ilianza kujionyesha mapema na mpaka muda huu hakuna dhamira ya kuiondoa ccm, sijui ww uko wapi, ccm haiondolewi kijinga hivo, wapinzani wenyewe mnasumbuana hivo ndani ya muungano huo wa UKAWA- katika hali ya kawaida ni ngumu sana, ndo maana nasema hizo ni ndoto za mchana. Nyie wenyewe mmebagua vyama vingine kuungana na ukawa yenu hiyo, itakuwaje useme muda umefika wa kuiondoa ccm? watz wamestuka kuwa wengiwao ukawa ni wapiga dili na si mabadiliko.

Mlianza kutokuaminiana tokea mlipo mchukua mamvi, mara Dr.Slaa akaondoka na Prof.Lipumba na yy akaondoka, tokea hapo hakuna umoja na utilivu ndani ya ukawa ila kwa sababu ww ni mpiga debe, timiza wajibu wako, unakuja na mifano ya kijinga kabisa. na kama mnasema ndo mwisho wa ccm mbona mnajinyeanyea kila siku oh mara tume si huru oh mara vituo vya kupigia kura ni vingi sana oh mara bado bvr zinaandikishwa, hiyo yote ni ushindi kwa ccm. Labda mjipange upya tena 2020. Na pia mwache kuokotaokota watu waliokataliwa kwenye chaguzi za vyama, na ndo unaweza kuwa mkosi bila nyie kujua.

Na tume imebaini majina mengi kujirudiarudia.......,,,, poleni sana.
 
Kuna msemo usemao watu hupata akili wakiwa wanaelekea kufa na kufa kunakuwa lazima ndio kinachowakuta CCM mwezi huu na ukweli ndio huo ingawa ni mchungu.
 
umeanza vizuri ila umemalizia kwa pumba kama wapinzani wangekuwa makini walikuwa wanaiondoa ccm mwaka 2025 lakini kitendo chao cha kutumia mafisadi ndio wamechemka inabidi waanze tena mwanzo itachukua muda mrefu kwani wamewapa nafasi ccm ya kujitazama upya

Jubilee jubilee jubilee jubilee jubilee jubilee jubilee
 
Tatizo lenu mnaota ndota za mchana kweupe, nashindwa kuwaelewa wanamageuzi, mbona mnajichanganya sana hivo? Kama mda ulikuwa umefika basi ni wazi kwamba mmekosea masharti, na ulipokosea jitahidi kijisahihisha mapema, ila kwa kuwa macho yenu yamefunikwa na ukungu mkubwa, itakuwa kazi sana ccm kuondoka kwa wakati huu, hii ilianza kujionyesha mapema na mpaka muda huu hakuna dhamira ya kuiondoa ccm, sijui ww uko wapi, ccm haiondolewi kijinga hivo, wapinzani wenyewe mnasumbuana hivo ndani ya muungano huo wa UKAWA- katika hali ya kawaida ni ngumu sana, ndo maana nasema hizo ni ndoto za mchana. Nyie wenyewe mmebagua vyama vingine kuungana na ukawa yenu hiyo, itakuwaje useme muda umefika wa kuiondoa ccm? watz wamestuka kuwa wengiwao ukawa ni wapiga dili na si mabadiliko.

Mlianza kutokuaminiana tokea mlipo mchukua mamvi, mara Dr.Slaa akaondoka na Prof.Lipumba na yy akaondoka, tokea hapo hakuna umoja na utilivu ndani ya ukawa ila kwa sababu ww ni mpiga debe, timiza wajibu wako, unakuja na mifano ya kijinga kabisa. na kama mnasema ndo mwisho wa ccm mbona mnajinyeanyea kila siku oh mara tume si huru oh mara vituo vya kupigia kura ni vingi sana oh mara bado bvr zinaandikishwa, hiyo yote ni ushindi kwa ccm. Labda mjipange upya tena 2020. Na pia mwache kuokotaokota watu waliokataliwa kwenye chaguzi za vyama, na ndo unaweza kuwa mkosi bila nyie kujua.

Na tume imebaini majina mengi kujirudiarudia.......,,,, poleni sana.

Kwa hiyo CCM hajaondoka yeyote?

Wewe ni mjuzi sana kuliko Mwapachu, Kingunge, Sumaye, Lowassa na wengine waliohama CCM.

Wewe ni mjuzi sana kuhusu CCM kama hao wazee niliowataja au ni mjulishwa tu kupitia stomach thinkers?
 
Dr Slaa yupo hapa mjini anakula bata daily. Kiufup now hana mchongo wowote zaidi ya kukaa home tu anasoma magazeti na kula bata coz hela anazo. Anaangalia tu Lowasaa anavyopeta
 
umeanza vizuri ila umemalizia kwa pumba kama wapinzani wangekuwa makini walikuwa wanaiondoa ccm mwaka 2025 lakini kitendo chao cha kutumia mafisadi ndio wamechemka inabidi waanze tena mwanzo itachukua muda mrefu kwani wamewapa nafasi ccm ya kujitazama upya

Sasa Rodrick, niambie mwaka 1995 baada ya CCM kutetemeshwa na Mrema walijitazamaje upya? Kwa kuuza nchi? Unajua CCM imejitazamaje tangu 1995 hadi sasa!!??
 
Kwa kifupi tu kumbukeni kejeli na kubeza kulikofanywa na kunguru wa mabadiliko wakati wa mijadala ya kuanzisha mfumo wa vyama vingi nchini. Kura zikapigwa, tukaambiwa asilimia 80 wamechagua chama kimoja. Lakini wakati ukashinda, maana wakati ulichagua vyama vingi.

Nelson Mandela ambaye alikuwa mfungwa kwa miaka zaidi ya 20 lakini wakati ulipofika alikuwa Rais wa kwanza wa Afrika Kusini mpya.

Kanali Muamar Gaddafi alikuwa kiongozi aliyeleta maendeleo ya hali ya juu kwa ustawi wa jamii ya watu wa Libya na Afrika kwa ujumla. Alifikia mahala pa kudhaniwa kuwa angekuwa Rais wa Afrika endapo Afrika ingeungana na kuwa moja. Alikuwa na ndoto ya kuleta umoja wa kweli katika Afrika.

Huyu jamaa alishindana na kupigana na wakati. Mwisho wake mnaujua vema.

Huu ni wakati wa mabadiliko Tanzania. Na sio mabadiliko wanayoyasema CCM na uongo wao wa kudanganya wapiga kura wenye ukunguru wa mabadiliko eti wananchi hawataki mabadiliko ya chama, mabadiliko tunayoyataka yanaanza na chama kilichopo madarakani kung'oka kwanza.

Huu ni wakati wa CCM kung'oka. Mabadiliko ya kweli ni CCM kung'oka kwanza na mjadala mwingine utafuata.

Subirini mjionee nyinyi mnaodhani CCM ni mungu wenu. Angalieni mjionee kama CCM inaweza kushindana na wakati.

Jiulizeni kwa nini Magufuli badala ya kuinadi CCM anajinadi yeye mwenyewe!!!!! Anajua CCM ni lazima ing'oke, anatamani angegombea kwingineko.

CCM imekuwa jino? ama kuzungusha mikono ndo maendeleo?
 
Uncle Salva mbona unatoa mapovu? Anza kufunga virago, ulimharibia sana JK kazi. Tusikukute hapo, yaani pisha mwenyewe. Na hakikisha umefanya retirement zako zote za safari vinginevyo utauza lile ghorofaghorofa, ile nyumba ya bi mdogo.
 
mwaka 95 upinzani ulipotea baada ya uchaguzi 2010 upinzani ulianza kupata nguvu 2015 upinzani umeongeza msisimko kwa sababu ya makada waliotoka ccm 2010 walioubeba upinzani kwa kiasi kikubwa walikuwa upinzani wakiongezewa nguvu na wachache waliotoka ccm baada ya uchaguzi wakina lowasa hawataweza kuzunguka kujenga upinzani kwani baada ya matokeo wengi watajiuzulu siasa hivyo upinzani utaanza upya kujijenga
 
Tatizo lenu mnaota ndota za mchana kweupe, nashindwa kuwaelewa wanamageuzi, mbona mnajichanganya sana hivo? Kama mda ulikuwa umefika basi ni wazi kwamba mmekosea masharti, na ulipokosea jitahidi kijisahihisha mapema, ila kwa kuwa macho yenu yamefunikwa na ukungu mkubwa, itakuwa kazi sana ccm kuondoka kwa wakati huu, hii ilianza kujionyesha mapema na mpaka muda huu hakuna dhamira ya kuiondoa ccm, sijui ww uko wapi, ccm haiondolewi kijinga hivo, wapinzani wenyewe mnasumbuana hivo ndani ya muungano huo wa UKAWA- katika hali ya kawaida ni ngumu sana, ndo maana nasema hizo ni ndoto za mchana. Nyie wenyewe mmebagua vyama vingine kuungana na ukawa yenu hiyo, itakuwaje useme muda umefika wa kuiondoa ccm? watz wamestuka kuwa wengiwao ukawa ni wapiga dili na si mabadiliko.

Mlianza kutokuaminiana tokea mlipo mchukua mamvi, mara Dr.Slaa akaondoka na Prof.Lipumba na yy akaondoka, tokea hapo hakuna umoja na utilivu ndani ya ukawa ila kwa sababu ww ni mpiga debe, timiza wajibu wako, unakuja na mifano ya kijinga kabisa. na kama mnasema ndo mwisho wa ccm mbona mnajinyeanyea kila siku oh mara tume si huru oh mara vituo vya kupigia kura ni vingi sana oh mara bado bvr zinaandikishwa, hiyo yote ni ushindi kwa ccm. Labda mjipange upya tena 2020. Na pia mwache kuokotaokota watu waliokataliwa kwenye chaguzi za vyama, na ndo unaweza kuwa mkosi bila nyie kujua.

Na tume imebaini majina mengi kujirudiarudia.......,,,, poleni sana.

Ila Mwapachu, Sumaye na Kingunge wapo?
 
Umeongea la ukweli
watu wameichoka CCM sio kwamba wanawapenda upinzani
wana doubts zao na wapinzani lakini CCM washaichoka
 
Tatizo lenu mnaota ndota za mchana kweupe, nashindwa kuwaelewa wanamageuzi, mbona mnajichanganya sana hivo? Kama mda ulikuwa umefika basi ni wazi kwamba mmekosea masharti, na ulipokosea jitahidi kijisahihisha mapema, ila kwa kuwa macho yenu yamefunikwa na ukungu mkubwa, itakuwa kazi sana ccm kuondoka kwa wakati huu, hii ilianza kujionyesha mapema na mpaka muda huu hakuna dhamira ya kuiondoa ccm, sijui ww uko wapi, ccm haiondolewi kijinga hivo, wapinzani wenyewe mnasumbuana hivo ndani ya muungano huo wa UKAWA- katika hali ya kawaida ni ngumu sana, ndo maana nasema hizo ni ndoto za mchana. Nyie wenyewe mmebagua vyama vingine kuungana na ukawa yenu hiyo, itakuwaje useme muda umefika wa kuiondoa ccm? watz wamestuka kuwa wengiwao ukawa ni wapiga dili na si mabadiliko.

Mlianza kutokuaminiana tokea mlipo mchukua mamvi, mara Dr.Slaa akaondoka na Prof.Lipumba na yy akaondoka, tokea hapo hakuna umoja na utilivu ndani ya ukawa ila kwa sababu ww ni mpiga debe, timiza wajibu wako, unakuja na mifano ya kijinga kabisa. na kama mnasema ndo mwisho wa ccm mbona mnajinyeanyea kila siku oh mara tume si huru oh mara vituo vya kupigia kura ni vingi sana oh mara bado bvr zinaandikishwa, hiyo yote ni ushindi kwa ccm. Labda mjipange upya tena 2020. Na pia mwache kuokotaokota watu waliokataliwa kwenye chaguzi za vyama, na ndo unaweza kuwa mkosi bila nyie kujua.

Na tume imebaini majina mengi kujirudiarudia.......,,,, poleni sana.

Baada ya October 25,2015 usijali utatumika vizuri na watu wazuri na siyo kama sasa unavyotumika vibaya.
 
Hili no tatizo LA kutaka kusikia unayoyaamini no sahihi kwako. Haijalishi aliyeko upande wa mabadiliko no msafi au mchafu kiasi gani watu wameikinai ccm kuliko unavyofikiri. Kwa taarifa yako ccm wote no mafisadi japo wanazidiana kiwango. Unabisha but muda utasema ukweli. Tusubiri
 
Hii ni kweli huu ulikua mwaka wa wapinzani lkn wamwamejichanganya wenyewe pale walipo mruhusu lowasa huku wakijua hatufai mpaka Baba wa Taifa kaacha usia kua tumuogope kama ukoma sasa hilo ndio kosa lao lkn kama angekua Dr slaa au Lipumba ccm wangeachia nchi lkn kwa huyu haiwezekani.afadhali ya mbichi kuliko kuungua.
 
Back
Top Bottom