CCM inalipa Kodi?

Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,524
2,000
CCM ndicho chama kinachoongoza miongoni mwa vyama vya siasa Tanzania kwa kumiliki Ardhi na majengo ambayo walijikabidhi toka CCM ile ya mfumo wa chama kimoja. Lakini swali la kujiuliza ni kama CCM inalipa kodi ya Ardhi na majengo kwa majengo yake na yale wanayoyatumia kama majengo ya biashara.?

CCM ina maeneo mengi sana wanayoyatumia kama sehemu za kuegeshea magari na huwatoza fedha wanaoegesha magari kwenye maeneo hayo. Jee CCM inalipa kodi kwa fedha wanazopata kutokana na kuegeshwa kwa magari kwenye maeneo hayo?

CCM ilijimilikisha viwanja vya mpira sehemu mbali mbali nchini. Kila mechi inayochezwa ama tamasha linalofanyika kwenye viwanja hivyo CCM huwa inalipwa ama kupewa mgawo wake. Jee CCM hulipa kodi kutokana na fedha hizo wanazozipata kutokana na makusanyo hayo?

CCM inamiliki vibanda vya biashara kwenye miji mbalimbali kwenye nchi yetu. Jee CCM imejisajili kama Kampuni ya upangishaji (Real Estates Company) na kupenwa leseni ya kupangisha vibanda hivyo? Kwa mfano hapa Iringa CCM wanamiliki zaidi ya vibanda 70 vya biashara kwenye Ofisi ya CCM Mkoa wa Iringa. Jee CCM hulipa kodi kutokana na fedha wanazozikusanya toka kwenye vibanda hivyo vya biashara?

CCM inamiliki vyombo mbalimbali vya habari , jee CCM hulipa kodi kutokana na matangazo yanayopelekwa kwenye vyombo vyao hivyo vya habari? Wafanyakazi kwenye vyombo hivyo vya habari na wale wengine wa CCM huwa wanalipa Kodi itakiwavyo kutokana na mishahara wanayopewa?

Isije kuwa CCM inaoongoza Serikali kudai kodi kwa wananchi wakati yenyewe inaoongoza kwa kutokulipa kodi!
 
mbere

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
6,907
2,000
Wewe kijaaaana hayaaaa!!!
Weweeeeee!!!
Watakunyonyooooa!!!
Hayaa!!!
Hawa si waaaaatu!!!!
Haya!!!!
Ni viaaaatu!!!!
Haya!!!!
 
Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
3,866
2,000
CCM ndicho chama kinachoongoza miongoni mwa vyama vya siasa Tanzania kwa kumiliki Ardhi na majengo ambayo walijikabidhi toka CCM ile ya mfumo wa chama kimoja. Lakini swali la kujiuliza ni kama CCM inalipa kodi ya Ardhi na majengo kwa majengo yake na yale wanayoyatumia kama majengo ya biashara.?

CCM ina maeneo mengi sana wanayoyatumia kama sehemu za kuegeshea magari na huwatoza fedha wanaoegesha magari kwenye maeneo hayo. Jee CCM inalipa kodi kwa fedha wanazopata kutokana na kuegeshwa kwa magari kwenye maeneo hayo?

CCM ilijimilikisha viwanja vya mpira sehemu mbali mbali nchini. Kila mechi inayochezwa ama tamasha linalofanyika kwenye viwanja hivyo CCM huwa inalipwa ama kupewa mgawo wake. Jee CCM hulipa kodi kutokana na fedha hizo wanazozipata kutokana na makusanyo hayo?

CCM inamiliki vibanda vya biashara kwenye miji mbalimbali kwenye nchi yetu. Jee CCM imejisajili kama Kampuni ya upangishaji (Real Estates Company) na kupenwa leseni ya kupangisha vibanda hivyo? Kwa mfano hapa Iringa CCM wanamiliki zaidi ya vibanda 70 vya biashara kwenye Ofisi ya CCM Mkoa wa Iringa. Jee CCM hulipa kodi kutokana na fedha wanazozikusanya toka kwenye vibanda hivyo vya biashara?

CCM inamiliki vyombo vya habari mbalimbali, jee CCM hulipa kodi kutokana na matangazo yanayopelekwa kwenye vyombo vyao hivyo vya habari? Wafanyakazi kwenye vyombo hivyo vya habari na wale wengine wa CCM huwa wanalipa Kodi itakiwavyo kutokana na mishahara wanayopewa?

Isije kuwa CCM inaoongoza Serikali kudai kodi kwa wananchi wakati yenyewe inaoongoza kwa kutokulipa kodi!
Acha ujinga we mzee.

Chama la majizi chadema linapukutika
 
Sophist

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
4,306
2,000
Kwa taarifa ziizopo ni kuwa CCM wanalipa kodi zote. Na ninakumbuka mwaka jana JPM alilizungumzia suala hili pia.
 
Zungu Pule

JF-Expert Member
Mar 7, 2008
2,218
2,000
Maswali mazuri sana. Hawatakujibu. Na usishangae TISS wakaanza kumsumbua Maxence awasaidie kukupata.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom